Hali si njema kwenye Makampuni ya Mawasiliano, Serikali iamke kutoka kwenye Usingizi wa Pono

Hao ni waongo tu.Kampuni za simu zina cash flows kubwa sana.Sijui kama zinahitaji kwenda kuongeza mtaji pale DSE au stock exchange nyingine kama makampuni mengine yanavyoangaaika.Wana liquidity kubwa sana.Mm nafikiri hizi ni siasa tu.
Serikali ya Awamu ya 5 ilichukua zaidi ya Bilioni 20 kutoka Account za Vodacom Tz plc kutoka mabenki tofauti NMB na NBC
A
 
Miezi miwili iyopita tulisikia Kampuni ya Millicom International Cellular SA (MIC) inayomiliki Tigo na Zantel imetangazaa kuwa imeingia makubaliano na kampuni ya Axian kutoka nchini Madagascar kwa ajili ya kuuza kampuni zake mbili za Tigo na Zantel kwa bei ambayo haijaweka wazi.

Mwezi mmoja baadaye nayo kampuni ya simu ya Vodacom ilimesema hakutakuwa na gawio kwa wanahisa katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia Machi, 2021.

Sababu za kutotolewa kwa gawio hilo ni hasara ya Sh30 bilioni iliyopatikana katika kipindi hicho.

Kutokana na hasara iliyopatikana baada ya kulipa kodi, bodi ya wakurugenzi imeamua kutopendekeza gawio katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha ulioishia Machi 31, 2021

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Hisham Hendi alisema hasara hiyo inatokana na namna kodi ilivyokokotolewa na kusababisha kutozwa kiwango kikubwa tofauti na mwaka uliopita.

Pia alibainishwa suala la kufungwa kwa laini milioni 2.9 za wateja wao ambao hawakukamilisha usajili liliathiri mapato na faida ya kampuni hiyo.

Ikumbukwe kuwa Katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita (ulioishia Machi, 2020) Vodacom ilipata faida halisi ya Sh45.76 bilioni ikipungua kutoka Sh90.76 bilioni iliyopatikana kwa mwaka ulioishia Machi, 2019.

Wakati hilo halijatulia, jana kampuni hiyo imetangaza kujitoa kudhamini ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2021/2022 kwa kile kilichoelewa kupata hasara ya sh30 bilioni.

Huko Airtel nalo hali si shwari wiki iliyopita tumesikia Kampuni hiyo ya Airtel imeuza minara yake ya mawasiliano wanayo imiliki kwa ubia na kampuni mbili tofauti – SBA Communications Corp na Paradigm Infrastructure Ltd kwa $175 milioni (sawa na Sh400 bilioni).

Mpaka hapa haitaji elimu kubwa sana kujua hali ikivyo mbaya kwenye sekta hii ya mawasiliano inayoingizia nchi fedha nyingi.

Tunapoelekea itakuwa mbaya zaidi, leo wanauza minara, kuacha udhamini wa ligi, kuuza kwa kampuni, kesho tutasikia wamefunga wameondoka.

Hii sio ishara njema hata kidogo niitake Serekali kukaa na haya makampuni ya simu kuona jinsi gani ya kutatua hizi changamoto haraka sana.

Naona kama serekali imelala usingizi wa pono "Haijigusi" Sjasikia Mbunge yoyote akiongela hili ili hali hizo fedha wanazolipana posho zinategemea kodi za haya makampuni.

Pia, Soma:

Uchumi bado Umekaza? Vodacom yajiondoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Nini kimeikumba Airtel? Wameuza minara yake yote na kugeuka wapangaji!

Kama hawapati faida wajitathmini sio jukumu1a serikali. Wanaweza kuangalia gharama zao. Huenda mishahara ya mameja na wakuregenzi inatisha kwa ukubwa au wanaibiwa na wafanyakazi wao etc. Ikishindikana wanaweza funga. Zikibaki kampuni chache zitakua na wateja wengi. Ndio maana ya ushindani ukishindwa unabwaga manyanga. Sio kufikiri serikali ikubebe huku gharama zako hazina tija.
 
Vodacom wamechoka ukisongesha tu wana kata pesa marambilimbili watu wengi wameibiwa hasa wenye kusongesha viwango vikubwa
Miezi miwili iyopita tulisikia Kampuni ya Millicom International Cellular SA (MIC) inayomiliki Tigo na Zantel imetangazaa kuwa imeingia makubaliano na kampuni ya Axian kutoka nchini Madagascar kwa ajili ya kuuza kampuni zake mbili za Tigo na Zantel kwa bei ambayo haijaweka wazi.

Mwezi mmoja baadaye nayo kampuni ya simu ya Vodacom ilimesema hakutakuwa na gawio kwa wanahisa katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioishia Machi, 2021.

Sababu za kutotolewa kwa gawio hilo ni hasara ya Sh30 bilioni iliyopatikana katika kipindi hicho.

Kutokana na hasara iliyopatikana baada ya kulipa kodi, bodi ya wakurugenzi imeamua kutopendekeza gawio katika kipindi hicho cha mwaka wa fedha ulioishia Machi 31, 2021

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Hisham Hendi alisema hasara hiyo inatokana na namna kodi ilivyokokotolewa na kusababisha kutozwa kiwango kikubwa tofauti na mwaka uliopita.

Pia alibainishwa suala la kufungwa kwa laini milioni 2.9 za wateja wao ambao hawakukamilisha usajili liliathiri mapato na faida ya kampuni hiyo.

Ikumbukwe kuwa Katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita (ulioishia Machi, 2020) Vodacom ilipata faida halisi ya Sh45.76 bilioni ikipungua kutoka Sh90.76 bilioni iliyopatikana kwa mwaka ulioishia Machi, 2019.

Wakati hilo halijatulia, jana kampuni hiyo imetangaza kujitoa kudhamini ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2021/2022 kwa kile kilichoelewa kupata hasara ya sh30 bilioni.

Huko Airtel nalo hali si shwari wiki iliyopita tumesikia Kampuni hiyo ya Airtel imeuza minara yake ya mawasiliano wanayo imiliki kwa ubia na kampuni mbili tofauti – SBA Communications Corp na Paradigm Infrastructure Ltd kwa $175 milioni (sawa na Sh400 bilioni).

Mpaka hapa haitaji elimu kubwa sana kujua hali ikivyo mbaya kwenye sekta hii ya mawasiliano inayoingizia nchi fedha nyingi.

Tunapoelekea itakuwa mbaya zaidi, leo wanauza minara, kuacha udhamini wa ligi, kuuza kwa kampuni, kesho tutasikia wamefunga wameondoka.

Hii sio ishara njema hata kidogo niitake Serekali kukaa na haya makampuni ya simu kuona jinsi gani ya kutatua hizi changamoto haraka sana.

Naona kama serekali imelala usingizi wa pono "Haijigusi" Sjasikia Mbunge yoyote akiongela hili ili hali hizo fedha wanazolipana posho zinategemea kodi za haya makampuni.

Pia, Soma:

Uchumi bado Umekaza? Vodacom yajiondoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara

Nini kimeikumba Airtel? Wameuza minara yake yote na kugeuka wapangaji!

Hizo janjajanja za kukwepa kodi, kila kampuni sasa hivi inatangaza haitoi gawio.

Magufuli aliwabana

Aliwabana au alikuwa anapora fedha zao? Kuna yale makampuni ya serikali yalikuwa yanatoa gawio hewa ili kuhadaa umma kuwa wanapata faida. Ila ripoti ya CAG imemuumbua.
 
Airtel inayumba sehemu zote iliyopo Afrika na wameshatangulia kuuza minara kwenye nchi nyinginezo, Tigo wameamua kuondoka Afrika nzima na wameshauza hisa zake nchini Ghana. Kampuni za simu zilimeenjoy high time kwa muda mrefu, ni muda kujiadjust kuendana na hali. Kama serikali ikifikiria wa kuwanasua nadhani waanze na wadau walio kwenye sekta ya Utalii ambao tangu covid ishamiri wako juu ya mawe.

Wakijaribu tena kuja na vifurushi vipya yatawakuta ya last time na mama hana msuli wa kuwakazia wananchi kama mtangulizi wake.
Mama atawakazia nini ndugu yangu angali huyo mtangulizi unayemsema kukaza kwake unreasonably ndio kumetufikisha hapa? Mama kachukua nchi wakati tumeshafikishwa sakafuni.
 
Kipindi cha Magufuli makampuni yamebambikiwa kodi kubwa sana..matokeo yake ndo haya
Kiongozi, huu mchezo wa kubadili jina la kampuni ili kukwepa kodi wewe ni mgeni nalo? Tulikuwa na ile grace period ya miaka 4 kwa hawa wawekezaji, baada ya hiyo miaka 4 waanze kulipa kodi, wakawa wanasema wamepata hasara, wanauza kampuni kwenye ule mwaka wa 4, rejea Sheraton Hotel mpaka kufikia Serena Hotel, Bulynhulu to Accacia n.k

2019 walipata faida ya 45bn, 2020 wana hasara ya 30bn, nani anawakagua kujua kisemwacho ndio ukweli wenyewe?

Au hii michezi ilibanwa kipindi fulani, sasa wameona fursa tena kwahiyo wanarudi kwenye asili?

Waliweza vipi kumudu na kutengeneza faida kwa miaka 5 ya kwanza ya JPM ambaye anazungumzwa kuwa chanzo cha hasara hizo?
 
Back
Top Bottom