Hali si hali: Magufuli ana uungwaji mkono kiasi gani ndani ya chama?

..tatizo anaweza kufanya mambo ya kikatili mpaka yeye mwenyewe na watu wake wakaogopa kuondoka madarakani.

..ndiyo yaliyotokea Zimbabwe. Mugabe alianza kwa matumaini makubwa, ila akazidisha ukandamizaji kiasi kwamba akahisi kuondoka madarakani siyo salama.

..au yaliyotokea ZANZIBAR. hofu ni kwamba chama kingine kikishika madaraka watakwenda kufukua records za attrocities zilizotokea miaka iliyopita.

Magufuli sidhani kama atang’ang’ania madarakani.

Zama zimebadilika sana.
 
Kama Musiba tulimpuuza na sasa tuameanza kumkubali vipi smartboy Msando na ukaribu wake Ikulu?
sisi wengine tulitambua kwamba Musiba anatumika tangu mapema sana , na kwamba hata Msando mtu aliyeteuliwa na Magufuli kwenye kusimamia mali za chama atakosaje kutumika pia ?
 
Kama Musiba tulimpuuza na sasa tuameanza kumkubali vipi smartboy Msando na ukaribu wake Ikulu?
Copied kutoka kwa account yake ya Instagram akimjibu Zitto Kabwe

"@zittokabwe we will resist any attack and disrupt the plans. Watu wafanye siasa lakini sio kutaka kufifisha jitihada zinazofanyika. Maneno “huu ni mwanzo mzuri” tells a lot. Kama hawajaongea watoke wakanushe na tutathibitisha. Hatutakuwa swayed in anyway. A spade is spade."

"
 
Ina maana mazungumzo ya watu [hususan hao viongozi] yanakuwa tapped?

Kwa upande mwingine, how could Nape and Kinana be that reckless?
Swali sio kwanini wamezungumza hayo. Ila tujiulize nani yuko salama. Nashukuru sina namba zao , na kuanzia leo nafuta ama sipokei simu za mwanasiasa yoyote hata awe ndugu yangu. Aka simo
 
..tatizo anaweza kufanya mambo ya kikatili mpaka yeye mwenyewe na watu wake wakaogopa kuondoka madarakani.

..ndiyo yaliyotokea Zimbabwe. Mugabe alianza kwa matumaini makubwa, ila akazidisha ukandamizaji kiasi kwamba akahisi kuondoka madarakani siyo salama.

..au yaliyotokea ZANZIBAR. hofu ni kwamba chama kingine kikishika madaraka watakwenda kufukua records za attrocities zilizotokea miaka iliyopita.

Uko sahihi kabisa, lakini uovu haudumu.
 
Huyo Musiba bado sijamsoma vizuri aisee!

Ni mtambo kweli au ni mzima kabisa kichwani
Ukifatilia kipaza sauti cha musiba, waye wake ulikotokea, huwezi amini! Ni kheri tukae kimya tuone yanayokuja mbele yetu!

Ni mkakati wa kuharibiana balaa! Pia timu maembe ina evidence nyingi kuliko team wazalendo!!! Tusubiri, muziki soon utaingia kwenye korasi
 
What goes around comes around...

Ndiyo hapo Rais wetu aone zile mbwembwe zote za watendaji wake kumsifia sifa kuhusu juhudu za serikali ya awamu ya tano za kinafiki... watu wanamengi ila ndiyo yamezibwa midomo...

Cc: mahondaw
 
Kwa kuwa inadaiwa kwamba awamu zilizopita *ziliachia (ruksa)*, basi ni lazima baadhi ya viongozi kwenye hizo awamu waguswe vinginevyo itaonekana ni uzushi!
 
Kama Musiba tulimpuuza na sasa tuameanza kumkubali vipi smartboy Msando na ukaribu wake Ikulu?

Mkuu naona ni kama hujaelewa hata kinachoendelea, hapa hakuna anayemkubali Musiba, bali watu wanashabikia ili kukoleza moto ili utokee mpasuko vizuri. Hao wote wanaotuhumu na wanaotuhumiwa wote ni wachafu, hivyo kinachofurahisha hapo ni ugomvi wa wazandiki.

Huo unaoitwa uimara wa ccm ni katika kufichiana madhambi, hivyo mpasuko baina yao utakuwa ni afya kwa Taifa. Katiba mpya na kutetea madaraka makubwa ya rais ilihujumiwa na wanaccm kwa maslahi yao binafsi. Je leo wanaccm wenye mtazamo tofauti na rais bado wanaunga mkono madaraka makubwa ya rais? Mfano mrahisi ni hao akina Makamba na waraka wao.
 
Back
Top Bottom