Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,411
- 114,363
Yawezekana labda ni mimi tu. Labda ni hisia zangu tu. Labda ni jakamoyo langu tu.
Natamani akili yangu iwe inanihadaa [my mind playing tricks on me...shout out to the Geto Boys. RIP Bushwick Bill].
Kinachoendelea sasa hivi nchini kimeanza kunipa wasiwasi.
Huyu mtu aitwaye Musiba naona kaibua mengi. Au labda niseme kasababisha yaibuke mambo ambayo yananipa hofu.
Yote yaliyotokea kabla ya hii kanda ya sauti inayodaiwa kuwa ni ya Nape Nnauye na Abdul Kinana, nilikuwa napuuzia tu. Kusema ukweli zile sauti zinafanana sana na sauti zao.
Wawili hao wanadaiwa kumteta Rais Magufuli.
Hii kanda imenifanya nijiulize mengi sana.
Najiuliza Magufuli anaungwa mkono kiasi gani na viongozi wa juu wa chama chake, wastaafu na waliopo madarakani.
Kama haungwi mkono na wengi, je, hii serikali yake ni dhoofu kiasi gani?
Manake sioni ni kivipi anaweza kuongoza na kufanya kazi kwa ufanisi kama atakuwa anapingwa kwa kiasi kikubwa na walio wengi kwenye uongozi wa chama chake.
Isije kuwa tuna raisi ambaye katengwa wenzake!