Hali si hali: Magufuli ana uungwaji mkono kiasi gani ndani ya chama?

Nikiwa kwa mtu fulani hapa hapa Dar nilisikia habari kuwa wale wakubwa wa awamu ya nne wana mpango wa kumfanya JPM awe rais wa kipindi kimoja.

Baada ya kuisikiliza hii clip nimegundua kuwa zile habari siku ile zilikuwa ni za kweli.
Na sasa ndio nimeelewa kwanini Lowassa na Rostam wamejiunga na bwana mkubwa, amehakikisha kabla ya 2020 anaimarisha timu yake ya ushindi.

Waliokula bata awamu ya nne wanataka kuendelea kula bata, nasikia hata wale jamaa wenye makombati ambao vidole vipo tayari kikazi, ni jamaa kutoka kwa Mzee Kagame.
Daah
Mpaka Naogopa Rafiki yangu...Mambo Mazito haya
 
2016 alikuwa major general......
2016 hiyo hiyo akapandishwa akawa Luteni Jenerali..... Umepinduka huo mwaka kapewa UJENERALI... Kulikuwa na makamanda wengi waliomzidi lkn wakaachwa akawa anapandishwa yeye faster faster ili aje awe CDF.
HAPENDWI JESHINI MAANA AMECHAGULIWA KISIASA SIO KIPROTOKALI, HATA SIRRO NAE KAPITIA NJIA HIYO.
Unahisi sehemu yoyote ya ulaji utapendwa na wote?
 
Hiyo voice clip kwangu mimi naona ni genuine! Bila kujali sana sauti lakini mtiririko na maudhui ya mazungumzo yananishawishi kusema siyo ya kughushi. Na inalekea ni ''kambi ya Musiba'' umeivujisha! Na imeivujisha kwa sababu ya mkakati maalum. Nashawishika kuhisi siyo hii voice clip tu ila ''kambi ya Musiba'' wana ushahidi ''mnono'' sana utakaowaweka kambi ya Kinana kwenye hali mbaya...... tena kwenye vikao vya CCM na mbele ya ''wazee'' wa CCM! Muda utaamua!
Nafikiri ccm yote itakuwa na hali mbaya si hao wastaafu tu, maana wana wafuasi ambao ni viongozi mpaka mitaani na inaelekea wote hawaridhishwi na mambo yanayoendelea (uongozi wa mwenyekiti wao)
 
Kwa namna alivyoiharibu nchi yetu nitafurahi sana kama atakuwa ametengwa kweli,kwa mtazamo wangu huyu mtu hafai si Msikitini,si kanisani wala kwa shetani

Nchi imeharibika kiasi gani kwani?

Mimi mbona sioni huko kuharibika..
 
hapa Sasa ngoma imefika patamu
🌶🌶🌶

Wamakonde hao hao "Ukikimbia nchale na ukisimama nchale"

Cc yetu machoooo

Wagombanapo marafiki......
 
Nani anamwelewa huyu Mkigoma?? Ila huyu kaka ni zaidi ya mnafiki!!! Eti anaomba baraza la wazee liingilie swala hili nchi inaelekea kubaya!!

Kama mpinzani alitakiwa afurahi hawa wazee kukaa kimya ilifukuto lizidi, mabadiliko hayawezi tokea kama chama tawala hakitapasuka!

Au anahisi lengo la watawala kukifutilia mbali ACT litakufa kwa sababu anatoa ushauri kwa sisiem!
 
HUYO NDO ACHUMAN NGABANGA!

NA HII NI TAFAKURI BAADA YA HABARI:
Sijui ni utani au vipi, lakini kuna visa vingi vya kuchekesha vinavyowahusu watani zangu wamakonde, na kifuatacho ni kimoja kilichotaka kuhatarisha mbavu zangu !

Jamaa mmoja alipotea porini na baada ya kutangatanga sana humo porini, jioni, akafika kwenye mji wa wamakonde katikati ya pori na baba mwenye nyumba akamkirimu mgeni wake ipasavyo.

Ulipofika muda wa kulala mwenyeji akamuonesha mgeni chumba cha kulala huku akimtandikia huyo mgeni chini, lakini mgeni alipolalamika kwanini anatandikiwa chini mwenyeji wake akamwambia "humu kuna vitanda viwili tu, kimoja nalalia mimi na chemeeji yako na hicho kingine analala mwenyewe Achuman Ngabanga."

Mgeni bado hakuridhika:"Sasa mbona kitanda cha Achuman Ngabanga kikubwa tu na kinatosha kulala watu wawili? naomba tuchangie kitanda na Achumani."

Mwishowe mwenye mji akamruhusu mgeni achangie kitanda na Achuman Ngabanga ambaye mpaka hapo alikuwa hajarudi nyumbani.
Usiku wa manane mgeni akahisi kuna kitu kama mnyama kinambugudhi kitandani na alipoamka akajikuta ana kwa ana na mbwa mkubwa ambaye naye anataka kulala hapo kitandani, na hapo sasa ikawa tena apiga yowe kumuamsha mwenyeji wake na kulalama "huyu mbwa vipi hamjampa mafunzo, mbona anataka kulala na binadamu kitandani?"

Jibu la mwenyeji lilimuacha hoi mgeni:
"HUYO NDO ACHUMAN NGABANGA MWENYEWE AMERUDI, UNAMPUKUCHIA NINI CHACHA? ....ACHA KUMPUKUCHAPUKUCHA ACHUMAN NGABANGA NAYE ALALE"


SASA WAZEE WETU KULIALIA KOTE KWANINI TENA? HUYO NDIE GAMBA WA MAGAMBA MWENYE GAMBA LAKE IN ACTION!

NDUKI ‍♂️‍♂️‍♂️‍♂️!
Achuman Ngabanga
 
Katiba ya CCM ina mapungufu, kwa hiyo hata wakilalamika au kupiga kelele namna gani, Mwenyekiti ndiye ndiye ana power yote: Mwenyekiti huyo ni Magufuli. Ni kama ambavyo Lowasa alilalamika lakini Kikwete akamzika.

Ukija uchaguzi huko mitaani, bado Magufuli ni maarufu sana kuliko kiongozi yeyote anayeweza kusimama dhidi yake. Kwa hiyo, (a) hahawezi kuzuia jina lake lisitoke CCM, halafu (b) hawawezi kuzuia wanachi wasimchague.Time will tell.

Watu wenye busara walisema usipoweza kumshinda adui, basi shirikiana naye. Naona kama Nape na Ngereja ambao bado ni vijana ambao walifaidi ile CCM ya zamani wanafanya makosa kujaribu kutumia jeshi la zamani kupigana vita ambayo hawatashinda. Wao walitakiwa wajenge truce na mamlaka ya sasa ili wasiathir political future yao badala ya kukimbilia mamlaka za zamani ambazo hazina dola; sijui busara zao zinawatumaje.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Nchi imeharibika kiasi gani kwani?

Mimi mbona sioni huko kuharibika..

Kwa sababu kuna watu wanaona kuwa wao ndio wanastahili kunufaika nayo, na wengine wanastahili kuwa wasindikizaji tu. Yaani taabu za wengine wakati wao wanakula ice cream, wao ndio furaha yao. Wanaona kuwa wao ndio wanastahili kuwa na madaraka, na wengine hapana. Kwamba umaskini ni kitu cha kawaida kwa walio wengi, na neema kwa selected few ndio sahihi.

Kaka hapo ndio kuharibika wenyewe.
 
Back
Top Bottom