Hii ni hotuba yangu kwa wananchi wa nchi ya wadanganyika mara baada ya kula kiapo;
- Ndugu wadanganyika;ukiona kulipaswa kuwepo maridhiano kabla ya kuchaguana na kisha hayo maridhiano ya wadanganyika hayakufanyika na yakatokea ya kutokea na sasa kuna utaratibu wa kulazimisha maridhiano na baadhi ya wanaotakiwa kufanya maridhiano wanawindwa na kufichwa mjue hali ni mbaya.
- Mkiona kuna kila jitihada za kuwanyamazisha wakosoaji (sio wa kutukana) na kila anayejaribu kuibuka kujaribu kusema haki ifuatwe na kuzuia vyombo vya habari kuripoti yanayojiri isipokuwa ya mfalme Zumaridi mjue hali ni mbaya.
- Mkiona mtu anasema vyombo vya ndoa ni vyake na vyombo vilivyotajwa kwenye harusi mbele ya Mc Polepole havisemi chochote juu ya kumilikiwa na aliye vitaja na anavitumia anavyotaka mjue hali ni mbaya
- Mkiona viongozi wa dini wanataka kuwaombea waliopoteza maisha wakati wa kupora mali na kuchoma biashara za watu; wanalaumiwa na watu mbali mbali akiwemo sheikh mmoja Mnyakyusa mla kitimoto mwenye kibali cha kuongea anavyotaka kwa sababu yupo juu ya sharia mjue hali ni mbaya.
- Mkiona bwana Tabasamu yupo kimya kwa sababu ana makusudi makubwa ya kutengeneza historia ya kijana wake kurithi kiti cha kifalme kwa gharama yoyote bila kujali hatima ya nchi ya Danganyika mjue kwamba hali ni mbaya.
- Mkiona tume,tume,tume,tume,tumeeeee zikundwa na zinapewa mambo ya kufanya na wananchi wa danganyika wanakwepa kukutana nazo mpaka kwa promotion mjue hali ni mbaya
- Mkiona mhimili wa kugawa haki unapokea na unapewa maelekezo ya kufanya na kijana wetu Abdala mjue hali ni mbaya. Kiujumla hali ni mbaya kona.