Hali ni mbaya:: Nimepanda basi kutoka dar kwenda Arusha Abiria hatuzidi 20

Ushabiki wa kijinga sana huu, hali mbaya, hali mbaya, hali mbaya,...miaka yote Watanzania maisha yao ni haya haya tu, ni lini Watanzania walisikika wakisema sasa hali ni nzuri? Tokea mimi nimezaliwa sijawahi kusikia watu wakisema hali ni nzuri. Tuache unafiki na ushabiki wa kisiasa usiokuwa na tija.
 
mhhh.somo linatakiwa lipite vijijini.wanajitia wanajua wakati hawajui.wana macho lakini wanajitia vipofu.wataisoma namba bora mjini hatulali na njaa.watanzania mnafurahia mziki ooo ni ile ile .ipi ? poleni wana vijiji vya mtakuja.badilikeni.
 
Wastani wa abiria dar to arusha kwa daraja la kati 35 elfu mara 20, mafuta km zaidi ya 600 posho ya dereva na konda, ushuru wa stendi kila wilaya itakayopitwa,kipande cha bosi, ya kubrashia viatu kwa wenzetu! aya bwana.
 
Sijui ata uongozi wa nchi una mikakati gani kushibiti hii hali tete katika hii nchi..!?
 
Hili jambo limenishtua kwa kweli, mpaka nimejiuliza huu ni mwezi wa saba au ni wa kumi na mbiliView attachment 442642
Miaka mingine watu walikuwa wanasafiri kwa mazoea hasa katika msimu wa sikuu wawe na likizo au la kulingana na mazoea. Mwaka huu/awamu hii ni tofauti hakuna kufanya kazi kwa mazoea utaenda unapotaka kwenda kama unalikizo na si vinginevyo. Dhana ya uwajibikaji imeshika kasi
 
Haya ndio maisha yetu! mambo ya bongo movie kushney! habr za kufanya kaz moro unaishi dar kisa nauli 7000 ndio byee!
 
Wakati mwingine namshukuru Mungu Watanzania tumefikia kipindi tunaanza kuzitumia akili zetu zilizokuwa zimelala kwa miaka mingi na sasa kila mtu anaishi kwa kutumia kila kipaji alichojaaliwa na maanani. Kila mmoja akubali kusota vinginevyo utaiba vya watu na watakutia petrol, kumbuka kuchomwa moto bado ni dawa rasmi ya wezi na wadokozi.
 
Dah...mijizi ina hali mbaya sana
Wametiwa kitanzi mpaka basi, mwisho watoto watauliza baba nini? watafichwa lakini ipo siku wataelewa kumbe u mwinyi wa mshua ilikuwa ni ujanja ujanja na wizi.

Msiache kuwaambia ukweli wanenu na itakuwa ni sehemu yenu ya toba kwa Mungu
 
.....njoo kwanza na id yako ya kila siku;
..huwezi kuwa umejiunga JF ili uanzishe huu utumbo!
.utatusumbua mbeleni!
 
Kama hali ni mbaya then hao 20 ni wakenya au?

Miaka yote takwimu zinaonesha wabongo tunaishi chini ya dollar moja mbona hakuna aliyehoji watu waliwezaje kusafiri December?
 
Haaahaaaa!! Daladala za mbagala, gongo la mboto na mbezi ya kimara siku zikiacha kujaa nitajua kweli hali ngumu. Haya maneno ya kuongezeana stress yanachosha kwa kweli. Watu wanajiombea ufilisikaji wa taifa. Angalia maisha ya wasudan,waethopia, wasomali walio wengi ndipo tutapoacha kujichulia!!!
 
Back
Top Bottom