Hali nchini Côte d'Ivoire baada ya upatanishi kushindwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali nchini Côte d'Ivoire baada ya upatanishi kushindwa

Discussion in 'International Forum' started by Mohammed Shossi, Jan 21, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hali nchini Côte d'Ivoire baada ya upatanishi kushindwa  [​IMG]Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Rais Laurent Gbagbo

  Viongozi wa bara la afrika wameingia mbioni kumshinikiza Laurent Gbagbo akubali kuondoka kwa khiari madarakani.Rais anaetambuliwa kimataifa anahimiza hata nguvu zitumike ikilazimika.

  Rais wa Côte d`Ivoire anaetambuliwa kimataifa Alassane Dramane Ouattara amesisitiza umuhimu wa kutumiwa nguvu ikilazimika,kumng'owa madarakani rais aliyemaliza wadhifa wake Laurent Gbagbo_Ouattara amesema hayo wakati wa mahojiano pamoja na ripota wa DW mjini Abidjan,
  Mbali na ripota wa DW mjini Abidjan,Alassane Outtara alizungumza pia na maripota wa shirika la habari la Reuters na kudai hatua kali zichukuliwe.Amefahamisha hata hivyo vikwazo vya kiuchumi pindi vikichukuliwa basi vimlenge Gbagbo tuu na na washirika wake na sio raia wa kawaida wa nchi hiyo inayozalisha kakao kwa wingi kabisa ulimwenguni.
  [​IMG]Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Alassane Ouattara na mjumbe wa Umoja wa Afrika Raila Odinga
  Akiulizwa kwa muda gani mgogoro huu utaendelea,na kama ukiselelea ataendelea kusalia katika Hoteli Golf,rais huyo anaetambuliwa kimataifa Alassane Dramane Ouattara amesema:
  "Hasha,mgogoro hautadumu muda mrefu.Nimeshasema na nnasema tena,lengo letu ni kuona hali inarejea kuwa ya kawaida kabla ya mwisho wa mwezi huu.Na nnaamini hivyo ndivyo itakavyokuwa.Jumuia ya maendeleo ya kiuchumi Afrika Magharibi ECOWAS imesema wazi kabisa,kwamba Laurent Gbagbo lazma ang'oke madarakani.Hayo yamesemwa tangu december 7 iliyopita-Wiki sita zimeshapita sasa.Ni sawa kwamba ECOWAS ina muongozo wake na hivi sasa pia viongozi wa kijeshi wanakutana mjini Bamako.Baadae watakuja Bouake kutuarifu.Lakini na sisi pia tunajitahidi upande wetu katika sekta ya kidiplomasia na fedha ili kuhakikisha Laurent Gbagbo anaondoka madarakani.Hawezi peke yake kushindana na ulimwengu mzima."
  [​IMG]Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Vikosi vya Umoja wa mataifa vinapiga doria mjini Abidjan
  Waziri mkuu mteule wa Côte d'Ivoire Guillaume Sorro alikwenda Togo na Burkina faso jana,katika juhudi za kuwatanabahisha viongozi wa nchi hizo wazidi kumtia kishindo Laurent Gbagbo.
  Wakuu wa kijeshi wa jumuia ya uashirikiano wa kiuchumi ya Afrika Magharibi walisema baada ya mkutano wao mjini Bamako Mali wamesema wako tayari,hata kama wanaendelea na maandalizi.
  Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika ,waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga yuko Afrika kusini kwa mazungumzo pamoja na rais Jacob Zuma baada ya kushindwa juhudi zake mjini Abidjan.
  Wakati huo huo tume ya Umoja wa mataifa nchini Côte d'Ivoire imesema wa-Côte d'Ivoire wapatao 29 elfu wamekimbilia Liberia na mkuyapa kisogo machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi kati kati ya mwezi uliopita.Watu 260 wameuwawa kufuatia machafuko hayo.
  Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/afp,reuters
  Mpitiaji:Abdul-Rahman
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Poleni sana ndugu zetu
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Sisi ilituokoa tume ya Taifa ikaona imtangaze tuu japo kashindwa maana haya ndo yangefuatia nani anataka milio ya risasi?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Jamaa anaitamani sana The Hague huyo!..
  Asipoangalia hata the Hague hataiona, maiti yake itaburuzwa Ivory Coast nzima!
   
 5. L

  Leornado JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huyu Ouatara ana roho mbaya sana na nimemshtukia haitakii mema Ivory coast, yaani anasisitiza matumizi ya nguvu kumuondoa bagbo bila kujali ni wananchi wangapi watauana wao kwa wao?? Aache kimbele mbele cha kuingia ikulu. Subira huvuta heri.
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Tatizo viongozi wengi wanapenda kutawala viwiliwili vya wananchi na si mioyo yao "Ukimiliki nyoyo za watu hupendeka"
   
 7. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ghagbo anaungwa mkono sana na watu wa eneo la kusini mwa nchi hiyo, hatua zozote za kumtimua kwa nguvu zitaleta umwagikaji mkubwa wa damu, kama Serikali ya Gbagbo ilivyoshindwa kulitawala eneo la Kaskazini kuna uwezekano mkubwa pia wa Serikali ya Quattara kutoweza kulitawala eneo la Kusini.

  Hili kuliepusha hilo na kujenga taifa moja nadhani ni vyema waendelee na mchakato wa mazungumzo mpaka muafaka upatikane ata ikiwa ni kwa kurudiwa kwa uchaguzi utakaosimamiwa na Umoja wa Afrika au kuundwa kwa serikali ya pamoja.
   
 8. CPU

  CPU JF Gold Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Demokrasia ya Afrika ni uwepo wa upinzani tu, lakin sio upinzani kushinda
   
 9. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kwa analizo lako.
   
 10. S

  Subira Senior Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  oh mungu wangukwa nini sisi wafrica jamani uelewa wetu maskini ni mdogo na kupenda madaraka ili tuishi kizungu, kula kizungu na hata kuoa au kuolewa na mzungu tu ndiyo tunayowaza,

  uingereza dakika moja tu wamekubaliana huyu anashuka anakuwa chini nchi inaendelea na mamabomuhimu
   
 11. B

  Blessy Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HIV NI KWANN VIONGOZ WENGI AFRI A HUPENDA KUNG'ANG'ANIA MADAKA?au kuna maslahi binafsi wanay kiac cha kuhofia wakiachia madaraka waweza adabishwa.
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  The bottom-line is alishindwa kwenye uchaguzi- period, na kwa mujibu wa katiba ya Ivory Coast anatakiwa kukaa kushoto...
  Hiyo Negotiation ya kuleta amani ya kusini na kaskazini itaanza kwa kusimamiwa na watu wengine...
  Wewe bado unamwona ni mtu credible hata baada ya kumwaga damu za watu wapatao 30 sofar?
  Huyu panapomstahili ni hukooo ICC, maana ameshindwa kuwatii hata viongozi waafrika wenzie!
  Ni kibri ya madaraka tu, si kupendwa wala nini!
   
 13. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  That's Afrika Mkuu.

  Lakini ukiangalia vizuri, Gbagbo pia ana hoja ya msingi katika kuyakataa matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi.

  Katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo yanayokaliwa na Waasi waliokuwa wanamuunga mkono Quattara katika kinyang'anyiro cha urais, hakukuwa na wawakilishi wa Gbagbo katika kuhakikisha uhalali wa kura zilizopigwa, na matokeo yameonyesha uwepo wa kura nyingi kutoka eneo hilo kuliko idadi ya watu waliojiandikisha na hii ndiyo hoja iliyoifanya mahakama iyafute baadhi ya matokeo ya eneo hilo na kumtangaza Gbagbo kuwa mshindi.

  Na kwa mujibu wa katiba yao, mahakama ndiyo yenye uamuzi wa mwisho kwenye utangazaji wa matokeo ya uraisi.
   
 14. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Makuu subira gani unazungumzia hapa. Mtu ameshindwa uchaguzi halafu hataki kuachia madaraka wewe bado unamtetea? Acha ang'olewe kijeshi na damu za watu zikimwagika, ajue The Hague will be his next destination. Jumuia yote ya kimataifa imemkubali Ouatara kuwa mshindi halali sasa huyu jamaa atatawala vipi nchi? Mimi namwona kama hatumii akili vile!!!

  Tiba
   
 15. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu!!

  Kwa mujibu wa katiba yao, matokeo ya mwisho yanatangazwa na mahakama ya katiba baada ya kuyapitia malalamiko/mapingamizi kama yapo na matokeo yatakayotangazwa na mahakama hiyo ndiyo matokeo rasmi ya uchaguzi wa Rais na ni mahakama hiyo ya katiba iliyofuta matokeo ya baadhi ya maeneo kutokana na udanganyifu(kwa mujibu wao) na kumtangaza Gbagbo kuwa mshindi wa uchaguzi ule.

  Hivyo kwa mujibu wa katiba ya Ivory Coast, Gbagbo ni Rais Halali.
   
 16. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 244
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Samahani sana bwana, umokosea kidogo. Mahakama ya katiba haina nguvu ya kubadilisha matokeo (article 64). Mahakama ya katiba inaweza kufuta matokeo yote na kutanzangaza uchaguzi upya ndani ya siku 45.
  CEI (electoral commission) ilifuta matokeo kwenye maeneo yaliyodaiwa kuwepo udanganyifu. Matokeo yake Allasane Ouattara alipata 54% na Gbagbo 46%.
  Rafiki yake Gbagbo kwenye mahakama ya katiba, kinyume cha sheria akaamua kufuta kura zaidi ya 600,000 za kura 800,000 ambazo zilipigwa kaskazini ya nchi. Ni sawa sawa na kufuta kura zote mkoa wa Mwanza kwa udanyifu uliofanyika eneo la Kisesa. Zaidi ya hapo, Paul Yao Ndre, mkuu wa mahakama ya katiba, akaamua kufuta kura zote kwenye kaskazini. Ni sawa na kufuta kura Tanzania za Mikoa Mwanza, Mara, Bukoba, Shinyanga na kwa uchokozi kidogo, Mkoa wa Kilimanjaro.

  Pili, kwenye makubaliano ya Pretoria, Gbagbo na wote walikubali kwamba ni UN itahalalisha kura, sio mahakama ya katiba.

  Tusisahau vile vile kwamba zaidi ya 70% ya kura za Allasane Ouattara zilitokea kusini mwa nchi, "kwa wakristu"... Ivory Coast imejichanganya kama Tanzania, hatuwezi kusema kwamba Dar es Salaam ni kwa waislamu na Mbeya kwa wakristo. Kusema kusini kwa wakristo ni uwongo wa akina Gbagbo wa kutishia dunia kwamba akiondoka Cote d'Ivoire hakutakalika....
   
 17. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 244
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Samahani tena Mzee.... Gbagbo alituma zaidi ya wanajeshi 4,500 kwenda kaskazini kusimamia uchaguzi. Walirudi kusini baada ya kura bila hata lalamiko moja.... Kutokuwepo na wawakilishi wa Gbagbo kwenye kura kaskazini sio kweli. Walikuwepo sehemu nyingi likini sio zote. Kwenye sehemu za kura 22,000 hawakuwepo kwenye sehemu 2,000 tu. Na hizo sehemu 2,000 zilikua vijijini ambapo hata Gbagbo mwenyewe anajua asingepata kura hata moja.

  Hizo kelele za kuwepo kura zaidi za wapiga kura mpaka leo hazijathibitishwa. Mpaka leo hii (22.01.2011), hata mahakama ya kangaroo ya katiba haijaweza onyesha uthibitisho wa kuwepo kura zaidi ya wananchi. Hata kama akina Allasane Ouattara wengetaka kudanganya kwenye kura wangekua wajinga kiasi cha kuzidisha kura kuliko wapiga kura wakati, UN/EU/ECOWAS/AU/Carter Centre wote wanatazama? Sio hivyo bwana. Juzi juzi Ouattara aliuliza watu kwa nini ajaribu kuiba kura kwenye sehemu ambazo anajua atashinda mikono chini?
   
 18. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  juzi si wamerudi wapatanishi baada ya kushindwa kufiakiana muafaka, na mbaya zaidi kwa sasa kumekuwa na kutoelewana kati yao na KENYA sababu Raila Odinga alikuwa alimwambia wazi gbagbo aachie madaraka lakini akaaendelea kukaataa, na wamesema hawataki kumwona tena Odinga akikanyaga nchini kwao..
   
 19. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 244
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Niliwaonyeni kuhusu huko nyuma!

  Jamaa ni kibaraka na nchi nyingi za kiafrika zinaongozwa na vibaraka........umefuatili statement ya Zuma alotoa hivi karibuni?
   
Loading...