Hali mbaya sana Muhimbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali mbaya sana Muhimbili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sizinga, Jun 26, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kuna siku nilienda kumetembelea Aunt angu pala Mwaisela..pembeni kulikuwa na binti mmoja aged 20+ anahema vibaya!!
  manesi hawashughuliki nae zaidi ya mama mmoja(ndugu yake). badae kidogo yule mama akampa maji ya kunywa...haikupita muda yule binti kakata roho mbele yetu. Nesi kaja kamshika mshipa wa mkono katoka zake tunaona watu wa vitanda wanaanza kukunjakunja na kuufunika mwili.

  Bahati nzuru nilikutana na mshkaji angu mmoja palepale anapiga field final yr, akaniambia hii ni hali ya kawaida kwa hapa Muhimbili na akanipa statistics kwamba kwa siku zaidi ya watu 40 wanakufa pale Muhimbili...!!
  Sasa kama hii ni data za kweli basi hali ni mbaya sana. Sijaangalia bado Amana, Mwananyamala, Hindumandal...mahospital mengine nk....na nadhani baada ya Babu wa Samunge hope idadi inaweza ikazidi kipimo. Duh maisha hayana thamani tena Bongo hii.
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana, utakuta hao Manesi walikuwa wanampa shinikizo huyo mama ndugu yake Marehemu ili awape kitu kidogo kabla hawajaanza kumhudumia mgonjwa wake..
   
 3. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hali ni mbaya hospital zote kwa ukweli hatuna serikali inayojali maisha ya Watanzania zaidi ya kutafuna kodi zetu. Wao wakiumwa huwa wanapelekana India, UK na South Africa, tena siku hizi wanapelekana sana South Africa utafikiri wanaenda kutibiwa bure, kumbe wanakwenda kutumbua Kodi za watanzania wanokufia Muhimbili tena na mpaka posho wanalipana wakienda huko. Inasikitisha sana kuona nchi yetu kila idara inakufa kwa Ari ya Mpya Kikwete, Kasi Mpya ya Kikwete na Nguvu Mpya ya Kikwete kuua idara zote kwa upeo wake mdogo. Yeye akili zake amezielekeza kwenye Ndege na ana bahati siku hizi ajali za ndege zimepungua
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nipo nchi moja ughaibuni wanaJF, huwezi kuamini nilikutana na dogo mmoja (Girl) katika kupiga piga stori za hapa na pale basi tukawa tunaulizana historia za hapa na pale, kagusia home kwetu ( my family), nikampa habari ya mama yangu kuwa alisha fariki! akashtuka sana. Akasema kwa nini? Alikuwa kazeeka sana au ajali? Nikasema aliugua tu ndo akafariki, alishangaaa sana. Na akasema hapa kwao, ni nadra kukuta mtu kafa kwa sababu ya magonjwa yanayotibika, watu wanakufa sababu ya uzee au ajali ndo vyanzo vya vifo vilivyozoeleka.

  Nachotaka kusema hapa wanaJF ni kuwa, bado mifumo yetu ya kiutawala inaabudu mabepari, mabwanyenye na mijitu iliyojilimbikizia mali nyingi harafu ndo imekuwa miungu watu, ndiyo inaamua kwa fulani wale nyama au maharage. Inasikitisha sana binadamu wenzetu wanapofanya mambo ya ajabu pasipo kujua huo uongozi ni fursa ya kufanya mema kwa ajili ya wengi.

  We still need to define our own rules and not to keep following other countries rules. How? Nikuwatolea uzembe viongozi wetu, na wakishautema uongozi tuwawajibishe kwa uzembe.
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mi niliishi India miaka 4...pale kitaa waliofariki ninaowajua hawazidi 5...naa wote ni vikongwe japo mmoja mwanacollege alipata ajali...hamna magonjwa ya kizembezembe namna hii hapa Bongo, tena siku hizi vibinti 23+ vikishika mimba ya kwanza tu kujifungua salama ni bahati....wengi wanafariki!! dah
   
Loading...