Hali MBAYA LOLIONDO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali MBAYA LOLIONDO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Apr 11, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]Baadhi ya watu waliopata tiba ya kikombe Tabora, wana hali mbaya na wamelazwa hospitali ya mkoa, huku wale wa Loliondo wakitoa ushuhuda wa....
  Source: JESUS IS LORD
   
 2. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hujaeleweka.

  1. picha ya gazeti gani la lini?

  2. Nani kawavua nguo za ndani na aliwavua ili awafanyie nini?

  malizia maelezo yako vizuri
   
 3. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hii lazima ni global publisher kama yenye magazeti mengi ya udaku pia online... Bombaaaaa
   
 4. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ushaidi wa kile unachopositi
   
 5. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ushabiki wenu wa kidini kwenye vikombe, unaendelea kupoteza raho za wa Tanzania kwa kuacha matibabu sahihi na kufuata ndoto za washirikina na ndoto za ajabu ajabu. Bibi wa Tabora na Babu wa Loliondo hao wote na watumishi wa shetani
   
 6. N

  Nguto JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,652
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Mkuu rekebisha kichwa cah habari. Kufuatana na caption yako "Hali mbaya Tabora sio Lolilndo".
   
 7. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Gazeti hili lilikuwa likiipigia chapuo dawa ya babu Loliondo. Hivyo kitendo cha kuandika negatively ni cha kuchukuliwa seriously. Pia wafuasi wa babu ndani ya JF wameyatumia saaaana kusapoti hoja ya kuwa babu anaponya. Hivyo basi habari za udaku ziwekwe pembeni. Tuwe tayari kujirekebisha. Hili ni gazeti la wiki hii.

  Ijumaa Wikienda limepokea ushuhuda wa watu sita waliodai wamekunywa kikombe cha Babu Loliondo, watano wamethibitisha kwamba hali zao ni mbaya, huku mmoja akisema hajielewi.

  Aliyesema hajielewi ni mnenguaji ‘baabkubwa' Bongo, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy' ambaye amerejea Dar hivi karibuni akitokea Kijiji cha Samunge, Loliondo kwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi'.

  Suzy alisema: "Sijielewi, nipo kama nilivyokwenda, sijaona tofauti yoyote kabla na baada ya kunywa kikombe."

  Hata hivyo, Monica Stephano wa Ukonga, Dar es Salaam aliliambia gazeti hili kuwa tangu anywe kikombe cha Babu Ambi hajapata choo, hivyo ana wasiwasi mkubwa na afya yake.

  "Nina wiki tatu tangu nitoke Loliondo. Nakula vizuri bila wasiwasi lakini sipati choo, hii sijui inaashiria nini. Tatizo langu la pumu ambalo ndilo limenifanya niende Loliondo bado lipo pale pale," alisema Monica.

  Husna Bwile wa Tegeta, Dar es Salaam alisema kuwa, alipokunywa dawa Loliondo alikuwa mzima kwa dakika 20 kabla ya kuanza kusumbuliwa na kizunguzungu sambamba na maumivu ya kichwa.

  "Nilipofika Dar nilikwenda hospitali, nikaambiwa nina Malaria. Nikadhani hiyo hali ilisababishwa na Malaria lakini nilikunywa dawa, nikapona ila bado kizunguzungu na maumivu ya kichwa yako pale pale," alisema Husna.

  Kwa upande wa Jennifer Kubaja wa Makongo Juu, Dar alisema kuwa mapigo ya moyo yanaenda mbio tangu amekunywa dawa ya Babu wa Loliondo.

  "Moyo pia unauma, yaani mapigo hayashuki. Nafikiria kurudi Loliondo nikamlalamikie Babu ili ikiwezekana aniombee, maana kikombe chake kimeshindwa kunisaidia," alisema Jennifer.

  Wanandoa, Peter na Stela Samidi walidai kupoteza furaha ya nyumba yao kutokana na hali iliyowapata baada ya kutoka Loliondo.

  Akizungumza na mwandishi wetu, Peter alisema kuwa tangu apate kikombe nguvu za kiume zimepotea, wakati mkewe kila siku analalamika tumbo linamsokota.

  "Mimi sijui lakini nguvu zangu hazipo na sijui tiba yake ni nini? Tatizo pia lipo kwa mke wangu, kila siku tumbo linamsokota. Wakati mwingine akianza kulalamika usiku hatulali," alisema Peter.

  Miujiza Loliondo kwa sasa ni kama nyumbani na tukio jipya ni la wanawake wawili waliokodi hema na kulala pamoja, kujikuta wakiwa wamevuliwa nguo zao za ndani.

  Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Esperanse, raia wa Kenya alimweleza mwandishi wetu kuwa, tukio hilo limewaogopesha na hajui kama ni la kishirikina au ni wahuni wamewachezea.

  Alisema: "Mimi na mwenzangu tulikubaliana kuchangia hema moja, tukalala. Nashangaa tulipoamka tukakuta hatuna nguo zetu za ndani.

  "Mbaya zaidi hazipo kabisa, yaani aliyetuvua ameondoka nazo. Mimi binafsi nilijikagua na sikuona kama nimebakwa ila mwenzangu anasema anahisi ameingiliwa kimwili."

  Akitumia lafudhi ya Kikenya, Esperanse aliongeza: "Kwa vyovyote vile tunaweza kupata dawa leo (Alhamisi iliyopita), kwa hiyo kitakachofuata hapo ni kuondoka hapa haraka, maana naona panatisha.

  "Inawezekana na mwenzangu naye hajabakwa ila hisia tu za kujikuta amevuliwa nguo ya ndani ndizo zinamfanya ajione kama vile amebakwa."

  Mwenzake na Esperanse aligoma kutaja jina lake kwa mwandishi wetu kwa madai kwamba yeye ni mke wa mtu na mume wake hajui kuhusu safari hiyo ya Loliondo.

  KUNA WABAKAJI?
  Tukio la Wakenya hao kudai kuvuliwa nguo za ndani Loliondo, limekuja baada ya Queen Suzy kuripotiwa na gazeti ndugu na hili la Ijumaa (toleo la Ijumaa iliyopita) akisema kwamba kuna wabakaji Loliondo. !!!!?????????? (emphasis mine)

  Suzy alisema kuwa kuna wanaume wamekuwa wakiwabaka wanawake wanaokwenda peke yao, hivyo aliwataka watu kuwa makini wanapokwenda Loliondo.

  Mwenye masikio na asikie.

  Zaburi 20 : 7
  "Hawa wanataja magari na hawa wanataaja farasi; bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu"
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Dah! Kama ni kweli hizi habari, basi hali ni mbaya............na ukweli muda si mrefu utajulikana.
   
 9. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona Mrema hajakutwa na hayo?
   
 10. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Hawa walienda kujaribu nguvu za Mungu. Walikuwa na imani HABA!
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  mbona jina la gazeti kama limefichwa vile....sio yale ya kutunga habari kweli?
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Watanzania tumekuwa na akili za kushikiwa kabisa.Kwa kweli suala zima Loliondo ni kama mchezo wa kuigiza ingawa bado watu na akili zao timamu wanapoteza pesa na muda kwenda huko..Sijui hii hali itakwisha lini jamani?:mmph::mmph::angry:
   
 13. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Tukiangalia fedha iliyoripotiwa kukusanywa na babu ina maana zaidi ya watu laki moja wameishapata kikombe. Kuwahoji watu sita tu na kutoa gazetini sio sahihi also not professional. Inatakiwa ufanyike uchunguzi wa kiukweli na objective ili majibu yake yasidie watu kutoenda au kwenda Loliondo. Haya mambo ya yule kapona, huyu hajapona hayatawasaidia wagonjwa wa Tanzania.
   
 14. s

  sha Senior Member

  #14
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  MWENYE MASIKIO NA ASIKIE,BABU HAMTUMIKII MUNGU BALI mungu wa dunia hii a.k.a shetani,
  HUWEZI KUBEZA UCHUNGUZI WA HAO WATU SITA WAKATI WATANZANIA HATA KWENDA TU HUKO NI KWA KUJIFICHA SEMBUSE KUKUBALI KUTOA USHUHUDA????!!!!!!!! UKIPENDA AMINI HUPENDI ENDELEA LAKINI UKWELI HAUTAKAWIA KUWA BAYANA, USILAUMU MTU."WEWE UMEWAONA WENGI KUPITIA KUPIGWA PICHA UNAFIKIRI MAPAPARAZI HAWAJAWAHOJI?????? KALAGA BAHO.
   
 15. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mtoto wangu alikuwa na tatizo la kifafa, alikunywa kikombe tarehe 18 march na tarehe 24 march tulisitisha dawa zake za kila siku. Hadi sasa ninapoandika bado kifafa hakijamrudia. Kwa kawaida ilikuwa ukikosea muda wa kumpa dawa anakamatwa! Nimejipa muda wa miezi miwili kujiridhisha kuwa amepona au la, hivyo ikifika tarehe 24 May nitakuwa na la kusema. Kwa sasa maendeleo ndiyo hayo.
   
 16. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,064
  Likes Received: 1,104
  Trophy Points: 280
  mungu gani huyo unayemwongelea anayewatesa watu wake namna hiyo? Kazi ya kutesa ni ya yule mwovu tuu, Mungu ninayemjua mimi ni mwema sana anataka tuokoke ili tuweze kuonana nae siku ya mwisho. Ni Mungu aliyemtuma mwana wake wa pekee ili aje kutuondolea dhambi zetu zote. Ni Mungu mwenye wivu anayetaka kuabudiwa na kutukuzwa Yeye mwenyewe milele na milele.

  Sasa niambie kama huyo babu anamtukuza Mungu huyu ninaye mwongelea. Kama hafanyi hayo basi lazina ana mungu wake na atahukumiwa kwa kuwapoteza wana wa Mungu ambao Yesu alikuja kuwaokoa.

  Ndugu yangu nakuomba usome maandiko, soma nyaraka za mtume Paulo ili uelewe, soma injili, hata kama hautaelewa roho wa Mungu atakufunulia na utaelewa na Mungu atafungua kinywa chako na utaanza kuwa hubiria wengine.

  Mungu akubariki sana.
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,319
  Likes Received: 5,643
  Trophy Points: 280
  Ndugu waachen watanzania wapone jamani
  kama mtu anaponya achen kuweka udini wekeni utu kwanza msikimbilie oohh kisa mnakosa daka ..kupungua kwa sadaka hii ni mungu kutonyesha mko kimwili zaidi kuliko kiroho watu amekwenda makanisa mengi kutaka uponyaji na imeshindikana sasa waachen watu waponywe msiangalie kama mtakimibiwa ama lah
   
Loading...