HALI MBAYA, CHADEMA yazidi kupukutika moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HALI MBAYA, CHADEMA yazidi kupukutika moshi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kakakuona40, Mar 7, 2012.

 1. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro kimevunja ngome ya Chadema katika Kata ya Mji Mpya katika Manispaa ya Moshi, baada ya kuvuna wanachama 75 akiwemo Katibu Mwenezi wa kata hiyo, Ludy Mlaki.

  Akipokea wanachama hao, Katibu wa CCM mkoani humo, Stephen Kazidi alisema wanachama hao wapya pamoja na ugeni wao ndani ya chama lakini pia wana haki za kuomba nafasi yoyote ya uongozi ndani ya uchaguzi wa chama.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kata hiyo baada ya kufungua mashina matatu ya wakereketwa wa CCM na kushusha bendera za Chadema katika kata hiyo, Kazidi aliwataka wanachama hao wapya wasitishwe na viongozi wa chama walichotoka.


  “Nimepata taarifa kuwa waliojiunga na CCM wameanza kupokea vitisho kutoka katika vyama walivyotoka, ninyi kuweni na amani, mkipata vitisho vyovyote toeni taarifa katika vyombo vya dola…siasa siyo vita, lakini mtu halazimishwi kuwa mwanachama,” alisema.

  Alisema chama kitawezesha matawi hayo kuwa na miradi ya kiuchumi katika kipindi kifupi kijacho kwani wanatambua kwamba vijana wanahitaji ajira na uanzishwaji wa miradi ndiyo ukombozi wao.

  Katibu huyo aliwataka wana CCM kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ndani ya chama ili kuweka safu imara itakayokisaidia chama kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2015.

  Akizungumza baada ya kupokea kadi ya CCM, Mlaki alisema amejitoa Chadema kutokana na ubabaishaji unaofanyika ikiwemo ahadi hewa na unyanyasaji dhidi ya wananchi.

  Alidai kwa kipindi chote akiwa Chadema, amekuwa akihamasishwa kufanya maandamano na kugomea shughuli mbalimbali za maendeleo bila kujali kuwa wanaoathirika ni wao wenyewe.

  Source: HabariLeo | CCM ‘yainyanyasa’ Chadema Moshi
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Habari Leo, a ghost daily tabloid
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Duh Mungu inusuru CDM isije ikawa historoa inakoelekea siko sasa !

   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Habari Leo....What a foolish!
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,272
  Likes Received: 3,947
  Trophy Points: 280
  Huu ni uthibitisho wa kupwaya
   
 6. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 1,830
  Trophy Points: 280
  Akina mama wanajazana zana ccm naona huko kuna zaidi ya siasa.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nsamburo yupo kweli?
   
 8. Sihali

  Sihali Member

  #8
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado siku za chadema zinahesabika mbowe kama hajajirekebisha tabia yake ya ubabe na dharau pamoja na unynyasaji kwa kutumia domo lake kwenye chama cha mkwe wake alicholishwa kiapo kwa kutoachia wengine kukiongoza wenye akili hawatakaa chadema. Huo ni mwanzo tuu msambaratiko uko njianiii
   
 9. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #9
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilistuka sana kumbe saurce habari leo! Habari leo, uhuru, mzalendo na tbc zote kazi yao moja tu, kufanyakazi ya kulinda magamba na ufisadi wake. Nani atoke cdm aende magamba? Hao ni watu wao wamekujanao kukamilisha zoezi na wanrudi nao.
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 33,785
  Likes Received: 8,348
  Trophy Points: 280
  Bahati nzuri hakuna asiyewajuwa wachaga kwenye dili za pesa, hayo ni maziombwe tu yanayofanyika.
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Uko kazini kuandika ulichotumwa.
   
 12. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #12
  Mar 7, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hao watakuwa wagushi hizo kadi
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,806
  Likes Received: 1,592
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona unaharibu jina la mtu: Anaitwa Ndesamburo ama Ndesapesa
   
 14. mzee wa miba

  mzee wa miba JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 763
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Don't punic najua hao walikusanywa na kugawiwa kadi za magamba wamenunuliwa na kupewa pesa ili kufanya promo katika media ,na hii ndo imekuwa kawaida ya wanamagamba,kwa porojo magamba hamjambo,wananchi walishakichoka chama cha mafisadi,hata kwa mtutu wa AK 47 hawatakubali kuramba matapishi yao,kwa taarifa yako mimi nilikuwa miongoni mwao pesa tumepata 50,000 kila mtu na zote nimeshazinunulia bati na risti ninazo na hata kikao na makada wa CCEM nilikirekodi jinsi walivyosuka mkakati kufanikisha hilo.Kama huamini nitafute ntakupa full episodes coverage,ebo hiv unafikiri tumelala?????????????????????????,huo upuuzi waambie wakafanyie Morogoro,Pwani,Mtwara,Tabora,Dodoma na Tanga vinginevyo wakija hapa nchi ya uchagani tutaendelea kuwapoteza mangi.
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Ni kweli mkuu ndio maana wakaripoti kwenye gazeti lao la chama
   
 16. mzee wa miba

  mzee wa miba JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 763
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Don't punic najua hao walikusanywa na kugawiwa kadi za magamba wamenunuliwa na kupewa pesa ili kufanya promo katika media ,na hii ndo imekuwa kawaida ya wanamagamba,kwa porojo magamba hamjambo,wananchi walishakichoka chama cha mafisadi,hata kwa mtutu wa AK 47 hawatakubali kuramba matapishi yao,kwa taarifa yako mimi nilikuwa miongoni mwao pesa tumepata 50,000 kila mtu na zote nimeshazinunulia bati na risti ninazo na hata kikao na makada wa CCEM nilikirekodi jinsi walivyosuka mkakati kufanikisha hilo.Kama huamini nitafute ntakupa full episodes coverage,ebo hiv unafikiri tumelala?????????????????????????,huo upuuzi waambie wakafanyie Morogoro,Pwani,Mtwara,Tabora,Dodoma na Tanga vinginevyo wakija hapa nchi ya uchagani tutaendelea kuwapoteza mangi.
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,447
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  hapo kwenye nyeusi mkuu hebu fanya maarifa tuipate ili Magamba yazidi
   
 18. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,266
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi cnto hama cdm hata nkibaki pekeyangu! , kwani ukwel m1 unaweza pambana na yacyokweli 200.
   
 19. mzee wa miba

  mzee wa miba JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 763
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waliokutuma waambie bado tuko makini,kila step tunayopiga mbele tunajua mahali tunapokanyaga,tuko fit zaidi isivyotarajiwa na wengi,waambie hatutasinzia na siyo kulala tu,kwakifupi tumejiaandaa kuchukua nchi by 2015,believe it or not,kama hutaki tafakari kwanini Mwal.Nyerere alimkataa Jeikei Na Tatizo uwazirimkuu,jibu siyo kwamba walikuwa bado boys,but Uwezo wa kuongoza nchi yetu na uadilifu wao ndivyo vilimpelekea mwalimu awakatae na kusemaa hawakuwanaga kauwezo ka kutuongozaga,ingawa wengi wanafikiri kuwa sababu ilikuwa ni ujana kitu ambacho siyo.
   
 20. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wandugu wala hiyo story kwenye habari leo haitutishi. moshi wanajua itikadi yetu. sisiem mtaishia kunawa tu.
   
Loading...