HALI MBAYA, CHADEMA yazidi kupukutika moshi

Haa haa haaaaaaa haaaa!!! Sina mbavu mie!! Haki ya kweli wewe ndugu yetu Kakakuona40 unamoyo, duuhhh!!

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro kimevunja ngome ya Chadema katika Kata ya Mji Mpya katika Manispaa ya Moshi, baada ya kuvuna wanachama 75 akiwemo Katibu Mwenezi wa kata hiyo, Ludy Mlaki.

Akipokea wanachama hao, Katibu wa CCM mkoani humo, Stephen Kazidi alisema wanachama hao wapya pamoja na ugeni wao ndani ya chama lakini pia wana haki za kuomba nafasi yoyote ya uongozi ndani ya uchaguzi wa chama.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kata hiyo baada ya kufungua mashina matatu ya wakereketwa wa CCM na kushusha bendera za Chadema katika kata hiyo, Kazidi aliwataka wanachama hao wapya wasitishwe na viongozi wa chama walichotoka.


“Nimepata taarifa kuwa waliojiunga na CCM wameanza kupokea vitisho kutoka katika vyama walivyotoka, ninyi kuweni na amani, mkipata vitisho vyovyote toeni taarifa katika vyombo vya dola…siasa siyo vita, lakini mtu halazimishwi kuwa mwanachama,” alisema.

Alisema chama kitawezesha matawi hayo kuwa na miradi ya kiuchumi katika kipindi kifupi kijacho kwani wanatambua kwamba vijana wanahitaji ajira na uanzishwaji wa miradi ndiyo ukombozi wao.

Katibu huyo aliwataka wana CCM kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ndani ya chama ili kuweka safu imara itakayokisaidia chama kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Akizungumza baada ya kupokea kadi ya CCM, Mlaki alisema amejitoa Chadema kutokana na ubabaishaji unaofanyika ikiwemo ahadi hewa na unyanyasaji dhidi ya wananchi.

Alidai kwa kipindi chote akiwa Chadema, amekuwa akihamasishwa kufanya maandamano na kugomea shughuli mbalimbali za maendeleo bila kujali kuwa wanaoathirika ni wao wenyewe.

Source: HabariLeo | CCM ‘yainyanyasa’ Chadema Moshi
 
Hata mimi walinifata wakanishawishi nipokee hela na kurudisha kadi ya chadema na kuchukua ya ccm nikawatoa na panga, nawahakikishia wana jf kuwa katika miji yenye wafuasi wengi wa chadema wasioipenda ccm na wasiodanganyika na njama za ccm ni MOSHI.
 
Moshi siyo kwa mafala, hao wataliwa pesa zao na wataachwa pabaya, hawaijui Moshi, ndo maana siamini hizi habari, kwanza "mji mpya" ndo wanazungumzia kama ndo Moshi?Ni sawa na kusema pasua ni Moshi,hivyo ni vitongoji tu, wanaweza wakawa wameenda kukusanya wanywa gongo just for publicity purposes.
 
kweli mfa maji haachi kutapa tapa. yaani ccm wamefikia hatua ya kuhangaika kutafuta watu na kuwahonga fedha ili tu, waonekane bado wanapendwa? Kazi kweli kweli. Game limekuwa baya, hata Nnauye simsikii tena. JK pamoja na makubwa ambayo yanatokea katika nchi yetu, yupo kwenye shughuli za anasa na starehe. yaani ni kama vile anasubiri 2015 ifike asepe. atakayefuata CCM 2015 atajijua mwenyewe.
CCM kwishney....!!! CDM Oyeeeeeeeeeee.........!!! Uzushi tu, hakuna mtu mjinga kiasi cha kurudisha kadi ya CDM na kuchukua jembe na nyundo. Wamekosa kazi ya kufanya....!!!!!


 
na bado siku za chadema zinahesabika mbowe kama hajajirekebisha tabia yake ya ubabe na dharau pamoja na unynyasaji kwa kutumia domo lake kwenye chama cha mkwe wake alicholishwa kiapo kwa kutoachia wengine kukiongoza wenye akili hawatakaa chadema. Huo ni mwanzo tuu msambaratiko uko njianiii

mpumbafu. Gamba wee!
 
Don't punic najua hao walikusanywa na kugawiwa kadi za magamba wamenunuliwa na kupewa pesa ili kufanya promo katika media ,na hii ndo imekuwa kawaida ya wanamagamba,kwa porojo magamba hamjambo,wananchi walishakichoka chama cha mafisadi,hata kwa mtutu wa AK 47 hawatakubali kuramba matapishi yao,kwa taarifa yako mimi nilikuwa miongoni mwao pesa tumepata 50,000 kila mtu na zote nimeshazinunulia bati na risti ninazo na hata kikao na makada wa CCEM nilikirekodi jinsi walivyosuka mkakati kufanikisha hilo.Kama huamini nitafute ntakupa full episodes coverage,ebo hiv unafikiri tumelala?????????????????????????,huo upuuzi waambie wakafanyie Morogoro,Pwani,Mtwara,Tabora,Dodoma na Tanga vinginevyo wakija hapa nchi ya uchagani tutaendelea kuwapoteza mangi.

Wewe Meku ndio nini kutuumiza macho na marangi rangi ya ajabu ajabu?

Kwani ungetumia font za kawaida na size za kawaida usingeeleweka?
 
CCM siku hivi ni jinga liliwalo,kama vipi changanya na za kwako.
 
Back
Top Bottom