MR.NOMA
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 338
- 502
Mvua zinazoendelea kunyesha zimeendelea kudhihirisha kuwa usafiri wa Mwendokasi bado hauwezi kutatua changamoto za usafiri jijini Dar! Leo asubuhi tangu saa moja kasoro mpaka sasa saa 3 mamia ya raia wanaendelea kusota kituoni huku wengine wakiamua kughairi na kutoka nje ya kituo kutafuta usafiri mwingine.
Adha hii ya usafiri inasemekana ipo pia kituoni Kimara na vituo vingine.
USHAURI- Mamlaka zinazohusika zifanyie kazi changamoto hii ikiwemo kuruhusu gari zingine ziweze kusafirisha raia wawahi kazini. Hii kukaa kituo cha basi masaa matatu inazorotesha uzalishaji na kuongeza umasikini kwa kuwa shughuli za kiuchumi zinaathirika pia.