Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,988
- 42,280
Afrika inadumaa kwa sababu hatujitambui. Hatujui hata priorities. Vitu vidogo vya kijinga tunavipa umuhimu mkubwa, matatizo makubwa tunayapuuza.
Tatizo kubwa la kwanza na msingi la Afrika ni mifumo mibaya ya kiutawala. Mifumo mibaya ya kiutawala imesababisha umaskini usioisha, vita vya wenyewe kwa wenyewe kugombania kidogo kinachozalishwa, matatizo makubwa ya ajira, uwekezaji mdogo, na uwepo wa viongozi matapeli na wevi wakubwa wa mali za umma.
Lakini kwa uduni wa akili tunageuza kama vile ushoga ndiyo tatizo kubwa la Afrika wakati hakuna anayelazimishwa kuwa shoga. Katika maisha yangu yote ya kuzunguka Tanzania, ni mara mbili tu nilioneshwa vijana wawili, kama miaka 10 iliyopita, nikaambiwa hao ni mashoga. Walikuwa wamejipodoa, wamekata nyusi, ukiwaona huelewi kama ni wanaume au wanawake. Nikauliza kama walikuwa wasanii, ndipo nikaambiwa kuwa ni mashoga. Hao niliowaona mie ni wawili, lakini hakuna siku ambayo itaisha usikutane na Watanzania maskini kabisa ambao hawajui leo jioni au kesho watakula nini.
Kwanza, kama kweli kuna watu wanaupigia promotion ushoga, kwa watu walio maskini kabisa, ni rahisi kushawishika na kukubali kama jambo hilo litampa kipato kizuri na cha uhakika. Siku hizi tunaambiwa kuwa wapo mpaka vijana watanashati kabisa waliokubali kuwekwa kinyumba na baadhi ya akina mama wenye kipato. Na kichocheo cha hayo ni umaskini, na mtindo wa baadhi ya vijana kupenda maisha mtelemko.
Twende kwenye mambo makubwa na ya msingi, ingawa hatutakiwi kuyapuuza mambo madogo kama ushoga, pia.
Unashangaa spika anakataa kujadili ubadhirifu wa pesa ya umma, wenye athari kwa Watanzania wote, halafu anakubali kujadili ushoga ambao unawaathiri watu wachache. Kwa nini mambo madogo tuyape uzito mkubwa lakini makubwa, kwa sababu yanawahusu au yanawagusa ndugu na marafiki zao, yanapigwa teke?