Hali Halisi-Nina VVU

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
10,272
8,022

Ninaogopa....
Ninajiogopa mimi mwenyewe, ninauogopa ugonjwa nilionao.-
Kwani itatokea lini, itatokea lini?
Kifo cha taratibu, au labda cha haraka na bila maumivu?
Watu...
Wale wasionionyesha upendo
Wale wasionipa ulinzi ninaohitaji.
Tatizo la kifedha...
Ambapo hakuna msaada unaoweza kuonekana
Hufanya maumivu kuwa makali zaidi.
Wote wananitazama na kutikisa vichwa vyao...
“Hata hivyo unaenda kufa”
“Hatujui mbele hali itakuwaje”
“Una bima ya maisha?”
“Sithubutu kukupenda, Je kama ukifa na kuniacha!”
“Je ukiniambukiza?”
Ninataka kujiua...
Nitafunga kamba kuzunguka shingo yangu
Nitajirusha
Nitameza vidonge,
lakini labda kesho,
katika makutano ya barabara
au ndege ya kijeshi kuangukia katika sebule yangu
Hapana....
Nimetahadharishwa.
Tahadhari ambayo watu wachache tu hupata.
Je inanifanya mimi kuwa wa pekee?
Kitu cha pekee?
Inanifanya niogope
- lakini pia mwenye furaha.
Imenifundisha kupenda maisha
Na kuyathamini
Badala ya kuishi tu.
Sasa nahitaji kuishi
Nahitaji kuujua upendo.
Nahitaji kujua usalama.
Niamini....
Nifanye msikivu
Sikiliza sauti yangu ya ndani.
Sauti.
Hufanya ninyenyue kichwa changu juu
Na kutabasamu juu ya hatima yangu.
Inanifanya niishi kwa matumaini
Na kuniambia ni vyema,
maisha yangu yatakuwa mafupi kuliko ya wengine
Lakini labda mazuri zaidi?
Ninatumaini....​
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom