Elections 2010 Hali halisi kabla ya kutangazwa matokeo majimbo ya Dar

Ahsante Mkuu, furaha iliyoje kwa kushinda Mnyika chaguo la wengi, na hasira yangu ya jana pale Kituo cha Kilungule Kimara imepoa maana niliwahi kituoni kabla saa 12 lakini tulichelewa kuanza mpaka saa 1 na nikasumbuliwa kwa kwasabau ya kukosewa kwa jina langu na namba ya usajili lakini nashukuru nikapiga kura, hivyo kwa matokeo hayo machozi yanatoka kwa furaha kwa yule niliyempa kura yangu kama nilivyoaahidi hapa JF!

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na mmoja wa makampeni meneja wake, Edward Kinabo,mpaka sasa katika kata 14, Mnyika anaongoza kwenye kata 12 kwa kumzidi mgombea wa CCM, Hawa Ng'umbi kura 16,732.

Matokeo ya kata 2 za Saranga na Kibamba bado yanaendelea kujumlishwa na timu yake inayotumia fomu za matokeo halali ya kila kituo yaliyotolewa na NEC.Wakati huo huo wagombea udiwani wa Chadema kata ya Ubungo, Sinza, Saranga, Goba, Mbezi, Makuburi na Kibamba wanatarajiwa kutangazwa washindi wakati wowote kuanzia sasa baada ya kuongoza kwa kura nyingi.

Matokeo rasmi ya ubunge yanatarajiwa kutangazwa leo baada ya Nec na vyama vyote kukamilisha ujumlishaji unaoanza alfajiri hii Mabibo katika ukumbi wa shule ya sekondari Loyola.


Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mnyika mwenyewe
 
Mjengoni eeee! Patachimbika...Kushoto Mnyika kulia kabwe! Tutamkosa Slaa (Dr wa kweli of course)
 
Halima mdee wa CHADEMA ameshinda KAWE kwa mbali sana matokeo rasmi punde, matokeo ya udiwani yamechakachuliwa maana CHADEMA walikuwa wanaongoza vituo 90 kati ya 27 ila ndio hivyo tena diwani kata ya Kawe kashinda wa CCM
 
Heko, vipi wengine kina mboe, lema arusha na karatu

Nafurahi sana na habari hizi njema!!! Vip huko Hai... Mzee mzima Mbowe yukoje????? Please anyone with information please...:israel::israel::israel::israel::israel: Iam so glad.. niko kwa ofisi lakini kazi haziendi kabisa.. Leo sio blue monday kwangu ni hot monday:israel::israel::israel:
 
Back
Top Bottom