Hali halisi iliyopo nchini...

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,948
...pamoja na matusi, kejeli na kashfa zinazotolewa dhidi ya CHADEMA na viongozi wake ukweli unabaki pale pale kuwa maisha yanazidi kuwa magumu. Wale wote wanaoisifia ccm hapa ukumbini na kwingineko wanaweza kusema watakalo na kwa muda mrefu watakavyo lakini reality inabaki pale pale: maisha ni magumu na yanazidi kuwa magumu.

Hadithi ya kuwa matatizo ya uchumi yapo nchi zote (wakati hata Burundi wanapiga hatua kwenda mbele huku sisi tukirudi nyuma) haitabadilisha reality kuwa maisha ni magumu na yanazidi kuwa magumu. Kuwatukana na kuwakejeli CHADEMA hakuwezi kuleta mabadiliko.

Maisha yatazidi kuwa magumu zaidi na zaidi kwa kuwa serikali haijui inachokifanya na wizi uliokithiri unazidi kukithiri na kukithiri. Kina Zomba (alipaswa kujiita Zoba) and the likes watabwata weeee hapa ukumbini lakini reality inabaki pale pale, kuwa maisha ni magumu na yanazidi kuwa magumu.

Hoja na zisizo hoja za serikali zitaungwa mkono "kwa asilimia 100 na zaidi" lakini reality itabaki pale pale kuwa maisha ni magumu na yanazidi kuwa magumu. Bahati mbaya kwa watawala ni kuwa mtaji wa ujinga wa watawaliwa haufai tena maana ujinga haufumbi ukweli kuwa maisha ni magumu na yanazidi kuwa magumu kwa watawaliwa.

Watawala kabilianeni na hali hii halisi kama mnaweza, mengine yooote ni bure maana reality itabaki kuwa maisha ni magumu na yanazidi kuwa magumu. Na ndicho kifo chenu 2015!
 
kweli mkuu nakubaliana na weye kwa asilimia zote kasoro moja...tatizo ni mfumo mzima wa kiutawala...kuna haja ya kuufumua wote na kuweka mpya
 
Ni kweli kabisa, hao wabunge wapiga porojo tu, badala ya kujadili mambo ya msingi! Ni kwa nini mbunge apinge na aishie kuunga mkono jambo kwa asilimia 200.
 
Bila kushabikia itikadi yoyote kisiasa, uchumi unaosemwa kupanda haujatafsiriwa katika maisha ya kawaida kwa maana ya kuongeza ajira, kuongeza ubora wa maisha nk. Ni jamabo gumu sana kusema hali ya sasa ni nzuri kuliko ya miaka 5 iliyopita kwa mwananchi wa "kawaida".

Hivi ni kweli kipimo kwa ubora wa maisha katika urefu wa kilometa za barabara, majengo na idadi ya shule na vyuo vikuu, ni bora zaidi kuliko afya (chakula na matibabu), kiwango cha ufaulu, ajira endelevu na savings for the future??

Tafsiri ya maendeleo iko upande!!
 
Back
Top Bottom