Sababu Nne(4) Kwanini Maisha Yanazidi Kuwa Magumu Kwa Wengine

Ibnuyawar

Member
May 6, 2020
49
149
Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbikubwa la watu linalalamika kwamba maishayamekewa magumu.
Kwa sababu hii pia watuwengi wamekuwa wakikata tamaa na kuonamaisha hayafai ni bora waishi hivyo hivyo ilimradisiku ziende.

Malalamiko ya maisha kuzidi kuwa magumuyamekuwa yakisikika sana karibu ulimwenguni kote. Na kwa hili hiyo imekuwa ikipunguza raha yakuona 'utamu' wa maisha halisi.

Si vijana wala wazee kila mtu amekuwa akisema lake juu yaugumu wa maisha.

Lakini pamoja na malalamiko hayo, kitu ambacho tunatakiwa tujiulize nini kinachopelekea kuwe naugumu wa maisha kila kukicha?

Makala haya yaleo inakwenda kukupa majibu kwa nini maishayanakuwa magumu kwa wengi zaidi.

1. KUTEGEMEA CHANZO KIMOJA CHA KIPATO

Kutokana na maisha kubadilika na gharama zamaisha kupanda karibu kila siku, suala lakutegemea kipato kimoja, ni moja ya chanzo chamaisha kuwa magumu. Watu wengi wanategemeakipato kimoja, zaidi kwa wengi ikiwa ni ajira.

Kwa bahati mbaya kipato kimoja hakiwezi kukidhi mahitaji yote hata iweje. Sasa kwa sababu hiyo yamaisha kupanda mara kwa mara, ni lazima tuugumu wa maisha uonekane. Hata siku moja usitegemee maisha yako yakawa rahisi kamabado una kipato kimoja.

SOMA;Watoto Wenye Uzito Mdogo Hawaji Kuoa.

2.WATU WENGI WANAFANYA VITU WASIVYOVIPENDA

Maisha ni magumu pia kwa watu wengi chini yajua kwa sababu wamekuwa ni watu ambao kilasiku wanafanya kazi ambazo wasizozipenda.ama unafanya kazi usiyoipenda, unategemea Nini, lazima maisha yatakuwa magumu tu.

Kufanya kazi usiyoipenda, kwa kawaida kuna kuwa kunakuchosha sana na unakuwa unaifanya tu, kwasababu eti upate pesa ya kula. Kama umechagua maisha hayo, ujue kabisa maisha hayo yatazidi kukufanya wewe uyaone magumu kila kukicha.

3. WATU WENGI WANAISHI JUU YA MATUMIZI

Ugumu wa maisha pia kwa namna moja au nyingine unachangizwa na watu kuishi juu yamatumizi au vipato vyao halali. Unatakiwa kuelewawatu wengi, wanaishi juu ya matumizi kwa sababu Ni watu ambao wanataka waonekane wamefanikiwa.
Watu hawa wanakuwa wapo tayari wakope au wafanye lolote lile ili waonekane mambo yao yako safi. Kwa msingi huo wanakuwa wanajitengenezea maisha magumu ambayo wanashindwa kuyamudu kwa urahisi na matokeo yake kuongezaugumu usio na sababu.

SOMA:Je Upo Tayari Kutoa Kitu Gani Mi Uweze kutimiza ndoto zako

4. HAKUNA ANAYEJALI SANA MAISHA YA WENGINE

Maisha ya sasa hivi naweza kusema yamekuwa ni kama ya kuishi kisiwani, watu wamekuwa hawajali sana watu wengine kwa kiasi kikubwa,ukilinganisha na zamani. Kwa sasa ukipata changamoto kubwa wewe jua hiyo ni changamoto yako tu, inabidi ukomae nayo hadi utoke.

Kutokana na hili kuendelea kudumu kunafanya maisha yanazidi kuendelea kuwa magumu sana hadi watu wanakosa msaada ambao ungeweza kuwasaidia. Ubinafsi ambao wengi wanao imekuwa ni kichocheo kikubwa sana cha ugumuwa maisha.

Mwisho, pengine ujiulize, je, maisha yanaendelea kuwa magumu kwako kila kukicha? Jibu unalo wewe, nimekupa walau sababu chache zinazoonyesha kwa nini maisha yanazidi kuwamagumu.Wewe unaamini nini, niwekee maonihapo chini.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
 
Maisha ni haya haya ,kuna watu wanakinga 20m kwa mwezi halafu uje umwambie maisha ni magumu hakuelewi....Je kama maisha ni magumu sasa,lini yalikuwa mepesi? Tambua kila awamu kuna watu wataneemeka na wengine watatambaa na besela ,cha misngi ni kujitahidi uwe kwenye chaini ya walamba asali.
 
Wewe hayajakukuta mzee
 
Point
 
Kwa miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbikubwa la watu linalalamika kwamba maishayamekewa magumu.
Kwa sababu hii pia watuwengi wamekuwa wakikata tamaa na kuonamaisha hayafai ni bora waishi hivyo hivyo ilimradisiku ziende.

Malalamiko ya maisha kuzidi kuwa magumuyamekuwa yakisikika sana karibu ulimwenguni kote. Na kwa hili hiyo imekuwa ikipunguza raha yakuona 'utamu' wa maisha halisi.

Si vijana wala wazee kila mtu amekuwa akisema lake juu yaugumu wa maisha.

Lakini pamoja na malalamiko hayo, kitu ambacho tunatakiwa tujiulize nini kinachopelekea kuwe naugumu wa maisha kila kukicha?

Makala haya yaleo inakwenda kukupa majibu kwa nini maishayanakuwa magumu kwa wengi zaidi.

1. KUTEGEMEA CHANZO KIMOJA CHA KIPATO

Kutokana na maisha kubadilika na gharama zamaisha kupanda karibu kila siku, suala lakutegemea kipato kimoja, ni moja ya chanzo chamaisha kuwa magumu. Watu wengi wanategemeakipato kimoja, zaidi kwa wengi ikiwa ni ajira.

Kwa bahati mbaya kipato kimoja hakiwezi kukidhi mahitaji yote hata iweje. Sasa kwa sababu hiyo yamaisha kupanda mara kwa mara, ni lazima tuugumu wa maisha uonekane. Hata siku moja usitegemee maisha yako yakawa rahisi kamabado una kipato kimoja.

SOMA;Watoto Wenye Uzito Mdogo Hawaji Kuoa.

2.WATU WENGI WANAFANYA VITU WASIVYOVIPENDA

Maisha ni magumu pia kwa watu wengi chini yajua kwa sababu wamekuwa ni watu ambao kilasiku wanafanya kazi ambazo wasizozipenda.ama unafanya kazi usiyoipenda, unategemea Nini, lazima maisha yatakuwa magumu tu.

Kufanya kazi usiyoipenda, kwa kawaida kuna kuwa kunakuchosha sana na unakuwa unaifanya tu, kwasababu eti upate pesa ya kula. Kama umechagua maisha hayo, ujue kabisa maisha hayo yatazidi kukufanya wewe uyaone magumu kila kukicha.

3. WATU WENGI WANAISHI JUU YA MATUMIZI

Ugumu wa maisha pia kwa namna moja au nyingine unachangizwa na watu kuishi juu yamatumizi au vipato vyao halali. Unatakiwa kuelewawatu wengi, wanaishi juu ya matumizi kwa sababu Ni watu ambao wanataka waonekane wamefanikiwa.
Watu hawa wanakuwa wapo tayari wakope au wafanye lolote lile ili waonekane mambo yao yako safi. Kwa msingi huo wanakuwa wanajitengenezea maisha magumu ambayo wanashindwa kuyamudu kwa urahisi na matokeo yake kuongezaugumu usio na sababu.

SOMA:Je Upo Tayari Kutoa Kitu Gani Mi Uweze kutimiza ndoto zako

4. HAKUNA ANAYEJALI SANA MAISHA YA WENGINE

Maisha ya sasa hivi naweza kusema yamekuwa ni kama ya kuishi kisiwani, watu wamekuwa hawajali sana watu wengine kwa kiasi kikubwa,ukilinganisha na zamani. Kwa sasa ukipata changamoto kubwa wewe jua hiyo ni changamoto yako tu, inabidi ukomae nayo hadi utoke.

Kutokana na hili kuendelea kudumu kunafanya maisha yanazidi kuendelea kuwa magumu sana hadi watu wanakosa msaada ambao ungeweza kuwasaidia. Ubinafsi ambao wengi wanao imekuwa ni kichocheo kikubwa sana cha ugumuwa maisha.

Mwisho, pengine ujiulize, je, maisha yanaendelea kuwa magumu kwako kila kukicha? Jibu unalo wewe, nimekupa walau sababu chache zinazoonyesha kwa nini maisha yanazidi kuwamagumu.Wewe unaamini nini, niwekee maonihapo chini.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Sababu tatu za kwanza sio kweli,hata kwenye nchi zilizoendelea,sio kwamba watu Wana vyanzo vingi,ni kwamba vipato vinakidhi matumizi,sie ambao tunabeba boksi ulaya,na SA,tunaona,dereva wa uber ana pata mpunga mrefu kuliko bongo,
Nchi Haina viwanda,sekta ya kilimo imejaa Kodi kibao,ajira zitatoka wapi?
Kwa kila kilo moja ya kahawa inayouzwa 2500,Kodi peke yake ni zaidi ya 1700,mkulima atatoka vipi kwenye ufukara,sera za uchumi ni za hovyo,ccm wanaogopa sana wananchi wakiwa huru kiuchumi,watahatarisha utawala wao,ccm wanaona wapo salama wananchi wakiwa maskini,na ili uweze kutoka,inabidi uwe chawa wa ccm,
Kipindi Cha Kikwete,kulikuwa na sera ya kiimo kwanza,lakini asilimia 80 ya pesa ilitotengwa kuboresha kilimo iliishia kununua magari tu!!sasa hapo umaskini utaisha lini?lilijengwa bomba la gesi kutoka mtwara,gesi ilibidi iwe nafuu,tukapigwa,
Nigeria inachimba mafuta,lakini wananchi wanapanga foleni kununua mafuta,ni haba,makampuni ya nje yanachimba,yanapeleka kwao,yanachakata,harafu yanarudishwa nchini nigeria kwa bei kubwa
 
Back
Top Bottom