Mzee Kikwete alikuwa akikimbia nchi kila inapopata skendo, Rais Samia anarudi nchini kila hali inapotaka kuwa ngumu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
882
4,125
Mfumo wa Utawala wa JK ulikuwa wa safari nyingi nje. Nyingi ya safari zake zililenga zaidi kukimbia presha ya kisiasa ndani ya nchi sambamba na ugumu wa maisha. Pale alipobaini patatokea hoja ngumu ya yeye kusimama kama mwenye nchi kuamua alifafanya vyovyote iwezekanavyo awe nje ya nchi kupisha upepo.

Matokeo yake waliokuwa chini yake waliobaini ni mwoga wa kutoa maamuzi wakaamua wao kuanza kutengeneza hoja na kuzimaliza bila kuzifikisha kwake. Kila waziri au katibu mkuu au mkurugenzi aliyekuwa na jambo lake aliliweka kwenye mfumo ambao si lazima apate idhini ya baraza la mawaziri.

Maafisa na watendaji waandamizi waligeuka kuwa kila kitu katika maeneo yao. Finally, wenye nia mbaya na wapigaji wakatumia hiyo opportunity kupitisha mambo yao na kuifilisi nchi kwa kuuza kila walichotaka kuuza.

Mhe. SSH amekuwa na safari nyingi nje, awali zilikuwa zinalenga kuifungua nchi ila kadri siku zinavyokwenda malengo yanabadilika. Kutokana na safari zake nyingi nje kila jambo limegeuka lawama kwa watawala.

Wanaolalamika siyo wananchi wa kawaida bali watumishi wa umma wameamua kutumia mitandao ya kijamii kama watoa taarifa yaani whistleblower? Kila idara inamalalamiko ambayo ukifuatilia yana ukweli na yanapikwa kutoka chumbani kabisa.

Napata mashaka na namna mambo haya yanayolalamikiwa yanavyofanyiwa kazi. Hakuna kukemea maovu wala kuchukua hatua kunakofanyika. Ukimya huu umepelekea sasa kila mtu kula urefu wa kamba yake. Ubaya wa ulaji wa sasa ni kwamba unafanyika wakati ambao idadi ya watu imeongezeka, Duniani kuna umaskini wa rasilimali , hakuna ajira na pesa imekuwa ngumu.

Kuendelea kupuuza malalamiko na kuwekeza kwenye safari za nje linatupelekea kuwa na jamii ya watawala inayojiendesha kwa kila mmoja anavyojisikia. Hakuna accountability na matokeo ya haya ni kuwa na kundi kubwa la watu wasio na haki huku wachache wenye connection wakihesabiwa haki wasiostahili.

Sipingi safari za nje ila tuzibe kwanza mianya iliyopo ndani. Tuanze kukemea kwani tuliowapa uhuru wameamua kuchukua na madaraka hata yasiyokuwa yao .

Tusiwe taifa lakuamini kwa wageni, tutengeneze taifa lakuwategemea zaidi wazawa. Kila mgeni tukimkumbatia tutazalisha manamba na watumwa hapa nchni. Kumbukeni ajira hakuana
 
Wamtengezee Samia cheo kipya Balozi wa kudumu asiye na mipaka awe anaenda nchi zote kutuwakilisha. Urais, mambo magumu kama kuwasikiliza wananchi huko vijijini, kutatua kero zao amwachie mtu mwingine kama Majaliwa. Majaliwa apewe mamlaka ya Rais, Urais.
 
Mimi ninachojua jk alikua, ikitokea skendo yoyote ovu kwenye utawala wake, anawaachia kazi Vijana wake kina zito wakiongozwa na mwakiembe wanalisongesha bungeni kwa sayansi ya hali ya juu.
Akirudi mtu keshezaririshwa vya kutosha. Anawaachia kazi nyingine anakwea pipa.
 
Hivi Mama hana WASHAURI? au hata kusoma maoni ya wapigakura wake mitandaoni??..inashangaza ,kila siku kiguu na njia,HACHOKI??
 
Mfumo wa Utawala wa JK ulikuwa wa safari nyingi nje. Nyingi ya safari zake zililenga zaidi kukimbia presha ya kisiasa ndani ya nchi sambamba na ugumu wa maisha. Pale alipobaini patatokea hoja ngumu ya yeye kusimama kama mwenye nchi kuamua alifafanya vyovyote iwezekanavyo awe nje ya nchi kupisha upepo.

Matokeo yake waliokuwa chini yake waliobaini ni mwoga wa kutoa maamuzi wakaamua wao kuanza kutengeneza hoja na kuzimaliza bila kuzifikisha kwake. Kila waziri au katibu mkuu au mkurugenzi aliyekuwa na jambo lake aliliweka kwenye mfumo ambao si lazima apate idhini ya baraza la mawaziri.

Maafisa na watendaji waandamizi waligeuka kuwa kila kitu katika maeneo yao. Finally, wenye nia mbaya na wapigaji wakatumia hiyo opportunity kupitisha mambo yao na kuifilisi nchi kwa kuuza kila walichotaka kuuza.

Mhe. SSH amekuwa na safari nyingi nje, awali zilikuwa zinalenga kuifungua nchi ila kadri siku zinavyokwenda malengo yanabadilika. Kutokana na safari zake nyingi nje kila jambo limegeuka lawama kwa watawala.

Wanaolalamika siyo wananchi wa kawaida bali watumishi wa umma wameamua kutumia mitandao ya kijamii kama watoa taarifa yaani whistleblower? Kila idara inamalalamiko ambayo ukifuatilia yana ukweli na yanapikwa kutoka chumbani kabisa.

Napata mashaka na namna mambo haya yanayolalamikiwa yanavyofanyiwa kazi. Hakuna kukemea maovu wala kuchukua hatua kunakofanyika. Ukimya huu umepelekea sasa kila mtu kula urefu wa kamba yake. Ubaya wa ulaji wa sasa ni kwamba unafanyika wakati ambao idadi ya watu imeongezeka, Duniani kuna umaskini wa rasilimali , hakuna ajira na pesa imekuwa ngumu.

Kuendelea kupuuza malalamiko na kuwekeza kwenye safari za nje linatupelekea kuwa na jamii ya watawala inayojiendesha kwa kila mmoja anavyojisikia. Hakuna accountability na matokeo ya haya ni kuwa na kundi kubwa la watu wasio na haki huku wachache wenye connection wakihesabiwa haki wasiostahili.

Sipingi safari za nje ila tuzibe kwanza mianya iliyopo ndani. Tuanze kukemea kwani tuliowapa uhuru wameamua kuchukua na madaraka hata yasiyokuwa yao .

Tusiwe taifa lakuamini kwa wageni, tutengeneze taifa lakuwategemea zaidi wazawa. Kila mgeni tukimkumbatia tutazalisha manamba na watumwa hapa nchni. Kumbukeni ajira hakuana
Dume linakimbia matatizo
 
Wamtengezee Samia cheo kipya Balozi wa kudumu asiye na mipaka awe anaenda nchi zote kutuwakilisha. Urais, mambo magumu kama kuwasikiliza wananchi huko vijijini, kutatua kero zao amwachie mtu mwingine kama Majaliwa. Majaliwa apewe mamlaka ya Rais, Urais.
Hahaha kwa utaratibu upi sasa
 
Back
Top Bottom