k_u_l_i
Senior Member
- Jan 26, 2010
- 122
- 2
Miaka kumi iliyopita nyumba zimepanda bei bila ya kiasi hasa kwenye miji mikubwa kama vile Dar. Ni kweli sababu kubwa ya tatizo la uchumi ninaloendea duniani limeanzia kwenye mijengo kupanda bei mno katika miji mbali mbali duniani . Afadhali kwa sasa miji mingi bei zimepoa kidogo na zinaendea kupungua lakini Bongo imegoma. Kwa kawaida waTz hununua nyumba kwa cash hivyo kuifanya hadithi yetu kuwa tofauti. Hata hivyo kila kinachokwenda juu inabidi kirudi chini. Kwa vyovyote vile bei ya mijengo inabidi ishuke au itulie hapo hapo kwa miaka kadhaa ijayo. Je hii ni ndoto yangu ya mchana au yuko anayefahamu mwelekeo wa hili soko la nyumba bongo?
¬K
¬K