Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,255
- Thread starter
-
- #21
mwandishi umetumia lugha gumu sana,hebu nidadavulie kidogo............
Mh!mkuu kifaranga siyo mtamu!Vipi kula kula kuku na kifaranga?
Mh!mkuu kifaranga siyo mtamu!
Acha kujivunia aibu yako
Acha kula kuku na watoto
Acha kuku, kula mayai tu
Acha ubabaishaji wako
Acha, nasema wacha kabisa!
Halahala usimle kuku na mayai yake!
Visingizio vyako nimevikataa kabisa
Katu siafiki huo utetezi wako
Kamwe sitabariki uzandiki huo
Eti yote ni halali yako pia!
Nani kakudanganya hivyo?
Halahala usimle kuku na mayai yake!
Ukitaka maisha marefu, usimle kuku
Ukitaka amani, usimuibe kuku wa watu!
Ukitaka heshima, tafuna yai lake tu!
Ukitaka jina, mwache akutagie mengine
Ukitaka suluhu, mnusuru kuku akutagie
Halahala usimle kuku na mayai yake!
Wanaokula kuku na mayai yake wamelaaniwa
Wasiomwonea huruma kuku ni walafi hao tu
Wasiomjali kuku wamejikosesha mayai yake
Wasiomlinda kuku kututoka kabla ya siku zao!
Wanaoabudu matumbo yao humeza kila kitu!
Halahala usimle kuku na mayai yake!
Waliomtafuna kuku na mayai yake ni wafu!
Kama bado wako hai basi wanasuasua tu!
Kama wako barabarani basi wanachechemea tu!
Kama hawachechemei basi wanameza tunguri tu!
Kama hawamezi ndunga basi ni teja wa mengineyo!
Halahala usimle kuku na mayai yake!
RUTA kila kimoja kina ladha yake tofauti, kuku mtamu jamani, umkaange, uunge mchuzi, wa kuoka, wa kuchoma.... alimradi kila mapishi anafaa, yai hali kadhalika, lina utamu wake, ukikosa jutia lakini ukifanikiwa kulipata yai na kuku kula vyote tu kwani tatizo ni nini? mama ana ladha yake na mjuzi wa mambo mengi lakini na mwana nae damu changa afaa pia kwa kuliwa... kibaya ni kuwaweka "sahani" moja!!!!!!!!!!:cheer2:Last edited by muhanga; Today at 13:21. Reason: typing error
Kuku uliwa na mayaie, hiyo haina haramuie,
Kuku na yai ni ile ile, hakuna tofautile,
Kula ni kula mayaie, yote kula ni sawie,
Nyama ya kuku ni tamu, kula ukipata nafasi.
Mayaie ni maarufu,uliwa kwa stahilia,
Uliwa kwa mchemsho, uliwa naviazi mbatata,
Wengine upenda jicho, chips pia yai uitwa,
Wengine uagiza spanishio, wachina ula na bwabwa.
Mayai ya kuku safi, wengi uweka na keki,
Shababi ula omleti, mayaie ni egi chopi,
Mayai ya kuvuruga, ya faa sana kwa ugali,
Mayai ni mazuri, kula na kuku si dhambi.
Kula kuku na mayai, kwa stahili ni sawia,
Kuku upakwa mayai, huyu ni wa kukaanga,
Kuku wa kuchoma na yai, udenda utoka kabla,
Kuku uliwa na yai, kwa staili ni sawia.
Grili ya kuku na yai, na atasaza ugali,
Rosti ya kuku na yai, haya mayai ya tumboni,
Nani atasaza wali, kwa rosti kuku na yai,
Kuku uliwa na yai, kwa staili ni sawia.
Kuku uliwa na yai, kwa staili ni sawia,
Ruta kula kuku na yai, kwa staili ni sawia
Kuku uzaa yai, yai ni kuku pia,
Kuku uliwa na yai, kwa staili ni sawia.
muhanga ukimla kuku waachie wengineo nao wale mayai yake.................usiwe mlafi.......................kuhusu sahani moja ni kilekile tu kama umeonja huruhusiwi kuendekeza tamaa yako......ridhika na mojawapo