Hakuna wa kumtoa huyu mbunge

Nimeshawahi kufika Tabora siku za karibuni ikiwemo Urambo. Kaliua haijawa Wilaya bado ila wako kwenye mpango huo. Tabora kwa ujumla wake kuanzia Tabora mjini,Sikonge,Urambo,Igunga na Uyui bado sanaaaaa.Pamoja na historia kubwa iliyonayo katika nchi hii Tabora bado wana safari ndefu kimaendeleo.Ukiangalia pale manispaa no aibu tupu. Kaliua napo pako nyuma sanaaaaaaaaaaa. Amkeni
 
Kawafanyia nini? huyu aliyekuwa anapokea sitting allowance za RA bungeni? huoni aibu mwanaume unakuwa unpokea posho ya mwanaume mwenzako? Haya tueleze kawafanyia nini?[/QUO

hana lolote, me nilikua kaliua october mwaka jana ni sehemu ya ajabu very primitive sijawahi ona katika nchi hii. walichonacho ni umeme tu kwa sababu kuna kituo cha treni, usalama sufuri, maji hakuna, kuna guest 3 na zote za kapuya ukichelewa utalala kwenye gari. Usalama sufuri. Wana umwinyi mbaya, yaani sijui nisemeje tu lakini ni sehemu mbaya mbaya mbaya sana jamani. Sina hamu napo
 
Huyu mbunge Kapuya sijui ni Prof wa nini kwa kweli mie binafsi namuona kama ni mzigo kwa taifa!

Uwa nashangaa Prof mzima eti anamiliki bendi, Acudo Impact.
 
Kuna wabunge wengi wapo matumbo joto wakihofia kupoteza majimbo yao mwaka 2015 lakini sio kwa Prof JUMA ATHUMANI KAPUYA mbunge (CCM) wa URAMBO MAGHARIBI(Wilaya mpya Kaliua) hakika Kapuya ametutoa mbali na kamwe hatutamtosa amefanya mazuri mengi na bado anaendelea. Ni mbunge ambaye hana maneno mengi zaidi ya vitendo. MUNGU MBARIK KAPUYA NA IBARIK KALIUA.

Kweli na ndio maana ameanzisha bendi ya AKUDO hapa Dar kutuburudisha wanannchi wa Kaliua!!! Huyu jamaa hafai na katika nchi zilizostaarabika angekuwa jela kwa kubaka mfanya kazi wake; true testament!!
 
Mta mada acha upotoshaji. Mie natokea kaliua kijiji cha Igagala ndio home kwetu hasaaa. Kaliua bado iko nyuma sana kimaendelea, hakuna huduma ya maji ya uhakika, barabara mbaya na ni eneo ambalo halijui kitu lami inafananaje, walau simu ambazo ni biashara ya makampuni ndio unaweza kusema zipo kwa sasa kaliua na umeme pale mjini tu, otherwise hali ya vijiji vya Urambo Magharibi ni mbaya sana.

Angalia vijiji vya Igwisi, Imalamihayo na hata Kasungu ambapo ni jirani na Kaliua mjini, hali sio nzuri hata kidogo na pamoja na ukaribu wake lakini kunafikika kwa taabu kutokana na ubovu mkubwa wa barabara. Tena nenda sasa hivi kipindi hiki cha masika utajuta kuzaliwa!

Ukienda njia ya Mpanda maeneo ya KM 20 hadi ufike KM 60 ambapo panaitwa Ukumbi Siganga, hali ni mbaya na usafiri ni taabu sana kwenda huko. Tuwe wakweli wa dhamira zetu walla sio chuki. Kapuya hajafanya lolote la maana kwa miaka yake yote aliyokaa katika ubunge kwenye jimbo hilo. Inabidi wapatikane watu makini watakaoweza kuitoa Kaliua mahali ilipo sasa iweze kusonga mbele.

Mbaya zaidi, mtoto wake Kapuya amekuwa kama ndio mbunge maana haguswi hata na vyombo vya dola kwa makosa lukuki anayoyafanya. Kumbuka aliwahi kumpiga mtu risasi na polisi walimkamata na baada ya siku moja wakamtoa hadi leo anatamba mitaani kuwa hakuna anayemuweza. Vijana wavuta bangi wenzake wamekuwa wakiwashambulia kila wanaoonekana kumpinga Kapuya na kuwaumiza vibaya lakini polisi wanaangalia kwa kumuogopa babake.

Naijua vizuri Kaliua na kama nilivyosema ni mwenyeji wa kule huwezi kudanganya umma hapa kuwa eti kapuya kaitoa Kaliua mbali. Ukweli ni kwamba hakuna cha maana chochote alichokifanya.

Nawasilisha
 
Nimesahau moja, kwa ushirikina Kapuya hakuna anayemuweza KALIUA! Hapo nakubaliana na wewe 100%!!!
 
Nadhani mnaoongozwa na kapuya bado mnaishi kipindi cha zama za mawe

Hongereni saana na nadhani anawafaasaana,
ni vema mkamtangaza Mbunge wa maisha atawapeleka mbali
Kila la heri, hivi ile kesi ya mwanae aliyeua mlimsahehe?????????

Prof Kapuya hongera saana hakuna kitu kizuri kama kuongoza wajinga
 
mmh, hata kama ni upambe, kwa hili umechemsha. unaweza kuwandanganya watanzania wengine lakini sio wana-Urambo mabaya yanayozidi mazuri yake (Kapuya) na u-Mungu mtu aliojipa mtoto wake Baraka. Tafadhali kajipange upya kwa hili "umetokosha"
 
Sijawahi kuona pumba kama hizi. Kwa ufupi huna pointi kajipange upya. Ama huyu hapa kwe picha ni dada yako??? mana umesema kakutoa mbali.
 
Duh! Huyu jamaa mwenye sifa ya Ushirikina, kutembeza mpini, kula jani na wizi/ufisadi bado tu anakuwa mdini??! Sidhani,! Huyu ni pagani tu hawezi kuwa mdini

kwani dini za siku hizi wanatafuta hela au wanarudisha kundini wapotevu? Sikiliza mahubiri yao,yamekaa kisadaka sadaka tu. Ndo maana limekuwa kimbilio la wanyonyaji. Wengine ukiwanunulia daku tu,watakuabudu kama mtume wao!
 
Back
Top Bottom