Hakuna uganga wa kweli!

Hakuna uganga wa kweli!

cool d

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,754
Habari wanajamii wenzangu.

Nimeamini hakuna uganga wa kweli huku usukumani maana katikapitapita zangu kwa hawa wanaojiita waganga kila unayekwenda kumuona anakuambia umpe matatizo yako sasa kwanini asikupime yeye mwenyewe alafu akakuambia ukweli.

Na mbona anakuambia vitu ambavyo havipo na kibaya zaidi kazi unayompa haileti matokeo ya kweli.Hasa hapa Mwanza ndo kabisa wanakupa story tu. Naomba tuchangie kama hawa waganga kuna ambaye alishafanikiwa.
 
Huku kunasehemu hata makanisa yalishakimbia siku nyingi sana
 
nia yako nini kuelekezwa kwa mganga mzuri au ?
 
jf waganga wapo pia ila mganga mkuu ni Mungu wako hao unajitafutia nuksi kwenye maisha yako
 
Huwa siamini uganga aka uchawi hata siku moja, waganga ni watu wajanja saana, wanacheza na akili za watu tu, hakuna lolote.
Yaani wanachofanya ni kukuhoji tena kwa undani juu ya tatizo lako, mfano kuna jamaa yangu aliojiwa ye shida yake ni kupata utajiri, uone waganga walivyowajanja, alichofanya ni kumpa dawa na masharti tena ya ovyo tu.
Lkn akamwambia asafiri aende maeneo fulani anunue plot na alime vitunguu,jamaa akalima vitunguu vikakubali, akauza na kupata hela za kutosha, mambo yakawa mazuri akatajirika. Sasa ukiangalia hapa ni kwamba mganga alisoma tu mazingira na jamaa aka practice mambo yakawa lkn si kwasababu ya yale masharti au dawa alompa bali ni ule ushauri wa kumtaka akalime, ushauri ambao hata mtu mwingine angempa tena bila masharti, lkn wasiochanganya na za kwao wataamini ni dawa ndo imesaidia.
 
Na kwakuwa wanajua watu wanatabia ya uvivu, cha kufanya wanakupa hayo masharti tena mengine ya ajabu na ya kushangaza mfano anaweza kukwambia umuuwe mzazi wako au ufanye nae mapenzi n.k na dawa ili uamini, lkn hakuna lolote hapo na mbwe mbwe nyingine zote ni ili umpe mpunga wa kutosha basi, wkt ungetumia njia nyingine ungefanikiwa bila gharama yoyote.
 
Umeenda kwa waganga feki nenda kwa waganga original uone utajua kweli Africa tumeendelea kwa science ya nidesign ila zambi voo
 
Waganga wa kienyeji ni watumishi waaminifu wa Shetani. Shetani hana uwezo wa kuponya. Natofautisha tiba za kupiga ramli kupandisha maruhani na dawa za miti shamba. Hizo za kupandisha mashetani na kupiga ramli zinakuwa chini ya Shetani mwenyewe. Kwa hiuo mganga wa kienyeji anakuwanna majini ya utambuzi lakini haya yiba. Sana.sana watakuwekea jini kubwa kuliko lililokuwa limekuingia na ndiyo maana wakati mwingine hutulia kwa muda lakini baadaye hali yake huwa ni mbaya kuliko mwanzo. Waogopeni waganga wa kienyeji kama ukoma. Ni mawakala wa Ibilisi.
 
Cool njooo tanga a cha mdomo

Kwa mchuzi wa nyoka,kwa msisi au, hata huko wapo feki. Tatizo sijui kwanini watu wanapenda kufamya sili haya mambo kama unamjua mganga wa kweli si umtaje kwani anatibu bure?si analipwa kwa kazi yake sasa uficho wa nini
 
Habari wanajamii wenzangu.

Nimeamini hakuna uganga wa kweli huku usukumani maana katikapitapita zangu kwa hawa wanaojiita waganga kila unayekwenda kumuona anakuambia umpe matatizo yako sasa kwanini asikupime yeye mwenyewe alafu akakuambia ukweli.

Na mbona anakuambia vitu ambavyo havipo na kibaya zaidi kazi unayompa haileti matokeo ya kweli.Hasa hapa Mwanza ndo kabisa wanakupa story tu. Naomba tuchangie kama hawa waganga kuna ambaye alishafanikiwa.



hivi mpaka leo bado unakumbatia ushirikina? achana na mambo hayo. mganga wa kweli yupo na yeye ndiye kiboko. Anapatikana mitaa kwetu na hata kwenu. Anaitwa Mungu. yeye anatibu ugonjwa wowote unachotakiwa ni kimtumikia katika kweli na haki pia uweke imani juu yake. '" Ole wake amtumainiye mwanadamu kuwa kinga yake maana hukumu i juu yake"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom