Hakuna Tume Huru, hakuna uchaguzi utakaokubalika nchini Waziri Selemani Jafo awajibike kwa kuharibu uchaguzi

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
MSIMAMO WA ACT-WAZALENDO;

“HAKUNA TUME HURU, HAKUNA UCHAGUZI UTAKAOKUBALIKA NCHINI” WAZIRI SELEMANI JAFO AWAJIBIKE KWA KUHARIBU UCHAGUZI.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Imetolewa leo Tarehe 11/11/2019

1. Mchakato wote wa Uchaguzi uanze upya: Lazima yote yaliyofanyika chini ya utaratibu wa sasa yafutwe, uchaguzi uahirishwe na mchakato wa uchaguzi uanze upya.

2. Wasimamizi wa Uchaguzi wote walioharibu mchakato wa uchaguzi huu wawajibishwe ili kukomesha tabia hii inayoharisha amani ya nchi.

3. Zitungwe Kanuni Mpya za Uchaguzi kwa maridhiano na makubaliano na Wadau wote hususani vyama vya siasa.

4. Iundwe Kamati Huru ya kusimamia Uchaguzi: Lazima maamuzi katika hatua zote za Uchaguzi yawe ya maridhiano na makubaliano ya vyama sio TAMISEMI, ambao hawana uhuru, uwazi na wala uwezo wa kutenda haki.

5. Waziri Selemani Jafo aitishe kikao cha pamoja cha vyama vyote vya siasa ili kukubaliana juu ya namna ya kusonga mbele Kwa utekelezaji wa mapendekezo yetu hayo. Kinyume na hivyo sisi ACT Wazalendo hatutashiriki Uchaguzi huu wa Tarehe 24 Novemba, 2019.

6. Kutokana na O-TAMISEMI kuwa Wizara iliyopo chini ya OFISI YA RAIS, tunamtaka Rais Magufuli afikirie upya kuiondoa ofisi hii Ikulu na kuirejesha kwa Waziri Mkuu kama ilivyokuwa awali ili ‘TAASISI YA URAIS IEPUKANE NA KASHFA ZA UHARIBIFU WA DEMOKRASIA NCHINI’

7. Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya Siasa kutokubali hadaa ya Waziri Jafo na kutumia nafasi hii kuwa pamoja kudai Tume Huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi wa mwaka 2020 usiwe na dosari tulizoshuhudia sasa. Bila Tume Huru ya Uchaguzi pasiwe na Uchaguzi wowote nchini. Viongozi wa Kitaifa wa vyama watoke na tamko la pamoja kutaka TUME HURU YA UCHAGUZI.

HITIMISHO

Ndugu wanahabari, ni wazi mchakato wa uchaguzi huu wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, hauwezi kuendelea kwa haki hasa baada ya wananchi kuonyesha hisia zao za kuichoka CCM katika hatua za awali katika uandikishaji wapiga kura. Serikali ya CCM itaendelea na gilba zake kuhakikisha inapoka demokrasia ili kujihalalishia ushindi kwa kutumia mabavu ya dola na mtandao mpana uliowekwa kwa kazi hiyo. Ndio maana vitisho vya waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola na DCI Robert Boaz vinaendelea kila uchao.

Tunaendelea kusisitiza msimamo wetu wa kujitoa kwenye uchaguzi na kuwataka wanachama wetu wote nchi nzima kuendelea kutekeleza agizo la Chama la kuandika barua za kujitoa kwenye uchaguzi. Aidha tunatoa wito kwa wanachama wetu kubaini wagombea bandia wa CCM waliopewa fomu kwa kugushi mihuri na barua za utambulisho maeneo kadhaa nchini ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.”
….
Joran Bashange
MWENYEKITI WA KAMATI YA KAMPENI NA UCHAGUZI TAIFA.
 
CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimetoa masharti matano kwa serikali, ili kishiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Anaripoti Regina Mkonde.

Masharti hayo yametolewa leo tarehe 11 Novemba 2019, jijini Dar es Salaam na Joran Bashange, Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi ya Uchaguzi.

Amesema, sharti la kwanza ni uchaguzi huo kufutwa na mchakato wake kurejewa upya, ambapo la pili ni kanuni za uchaguzi huo zitungwe upya sambamba na kuahirisha tarehe ya uchaguzi huo.

“Mchakato wote ufutwe na uanze upya, tukitaka kutenda haki kweli. Waahirishe tarehe, hakuna uchaguzi. Zitungwe kanuni za kuondoa watu, ziwekwe mpya na zifanyike kwa maridhiano na wadau wote hususan wanasiasa,” amesema Bashange.

Sharti la tatu ni uundwaji wa Kamati Huru ya Uchaguzi na isisimamiwe na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambapo shatri la nne ni Seleman Jafo, Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuitisha kikao cha maridhiano na vyama vya siasa, juu ya namna ya kushiriki uchaguzi huo.

“Iundwe kamati huru ya uchaguzi na isisimamiwe na Tamisemi ambayo haina Uhuru wa kusimamia uchaguzi huu. Baada ya kupewa maelekezo ya Rais John Magufuli. Tuwe na chombo huru kamati huru,” amesema Bashange na kuongeza;

“Aitishe kikao cha pamoja na vyama, ili kuweka makubaliano na maridhiano ya namna gani uchaguzi huu ufanyike kwa haki.”

Wakati huo huo, Bashange ametoa wito kwa vyama vya siasa vya upinzani kutoa tamko la pamoja la kudai Tume Huru ya Uchaguzi.

“Tunatoa wito kwa vyama vya siasa, kukaa kikao cha pamoja ili kutoa tamko la pamoja kudai Tume Huru ya Uchaguzi. Pasipo hivyo, ghiliba na bao la mkono litaendelea,” amesema Bashange.

Amesema, Jafo ameweka mpira kwapani na kuondoka nao, na kwamba wao hawako tayari kumkimbiza.

“Tunasisitiza msimamo wetu na kuwataka wanachama nchi nzima, kwamba waendelee kuandika barua za kujiondoa mpaka pale mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi. Maazimio ya vikao vyetu hayawezi kupanguliwa na matamko ya Jafo,” ameeleza Bashange.

Bashange ameeleza, bila mapendekezo yao kufanyiwa kazi, tabia ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupoka haki ya wananchi kuchagua viongozi wao, haitakoma.

“Hulka hii mbaya ya CCM ya kuendelea kupoka haki ya wananchi ya kuchagua viongozi wao, na kuwapanga viongozi wanavyotaka wenyewe, wakome.

“Tunaitaka serikali ikomeshe utaratibu huu. Sisi hatuwezi kuvumilia, tamko letu liko palepale. CCM imevuka mstari wa demokraisa, tusilaumiane,” amesema Bashange.
 
Mbona wanamaelezo mengi ,sisi wananchi TUNATAKA KATIBA MPYA itakayo kuwa na tume huru
IMG_20191027_131122.jpg
 
Wapinzani walinusa dalili za kushindwa

Wakaamua kijiondoa kukwepa aibu
FYI
Maeneo mengi sana wagombea kutoka upinzani walikatwa kipuuzi kabisa. Kwa mfano mtu kakosea jina la mtaa (Living stone yeye kaandika Living tone au living stones). Hili jambo mtu angeelekezwa tu na sio kukatwa jumla.

Watendaji wengine walifunga ofisi zao siku karibia tano kuelekea tarehe ya mwisho ya kurudisha form ili kukwepa tu kuchukua form za wapinzani.

Sio kwamba wapinzani wamejitoa bila sababu eti kuogopa aibu. Acha upotoshaji
 
Na kusipokuwepo na tume huru je? Zitto hebu acha longolongo njoo na suluhisho..hii ni serikali ya mabavu anza kutumia mabavu pia, bila maandamano yasiyokoma hata wewe mwakani utakua raia kama mimi tu..Africa haijawahi kuwa nyepesi ya longolongo za mtandaoni!
 
Very good Zito

Chadema nao wanamsimamo huohuo

Naimani NCCR na wengine lengo letu liwe moja tu.
 
Back
Top Bottom