Hakuna Tozo ya Usajili wa vikundi vidogo vya Kifedha-BoT

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Benki Kuu ya Tanzania BOT imesema hakuna tozo yoyote ya vikundi vidogo vya kifedha vya kijamii (VICOBA) vinavyoendesha shughuli zake, na kwamba hakuna kikundi chochote cha kifedha kinachomilikiwa na Benki hiyo.

Benki hiyo pia imesema vikundi vya kifedha vya Kijamii ni mali ya Wanachama na kwamba hakuna kikundi kinacholazimika kuwa chini ya makundi mengine kama SACCOS na Taasisi za kifedha.

Hayo yamebainishwa na Meneja Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za fedha na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, wakati akitoa mada katika Semina kwa Waandishi wa Habari za Fedha, Uchumi na biashara inayofanyika Mkoani Mtwara.

“Hakuna fedha inayotozwa na Benki Kuu ya Tanzania-BOT kwa ajili ya uendeshaji wa kikundi vya kifedha, na hakuna sheria yoyote inayotaka vikundi hivyo vitoe tozo kwenye Taasisi nyingine yoyote, vikundi ni mali ya wanachama na wanaotoza vikundi hivyo kwa ajili ya uendeshaji wanakosea” alisema.

Aliyasema hayo baada ya Waandishi wa Habari kumwambia kuwa kuna baadhi ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa wanatoza vikundi hivyo Shilingi elfu 30 kama gharama za uendeshaji wa vikundi.

“BOT tuliwaambia Mamlaka za Halmashauri za Wilaya kuwa, mnaposajili kundi dogo la kifedha, hakuna kutoza pesa yoyote, kama kuna kundi lipo linatozwa fedha sh elf 30 za usajili watuambia, na sisi tutachukua hatua kwa sababu sio utaratibu tuliowapa”alisema

Alisema kutokana na kuona kuna umuhimu mkubwa wa makundi hayo ya Kijamii kujikwamua kiuchumi kupitia mzunguko wa fedha zao wenyewe, BOT iliamua vikundi hivyo visajiliwe bure na kusisitza kuwa Halmashauri za Wilaya wanalifahamu jambo hilo.
 
Huyo meneja yuko vizuri sana na kaekeza vizuri mno. Vicoba ni mali za wanachama kusajiliwa ni vizuri kunasaidia kutatua changamoto ikitokea viongozi maruhuni wakiingia mitini na pesa za wanachama.
 
Benki Kuu ya Tanzania BOT imesema hakuna tozo yoyote ya vikundi vidogo vya kifedha vya kijamii (VICOBA) vinavyoendesha shughuli zake, na kwamba hakuna kikundi chochote cha kifedha kinachomilikiwa na Benki hiyo.

Benki hiyo pia imesema vikundi vya kifedha vya Kijamii ni mali ya Wanachama na kwamba hakuna kikundi kinacholazimika kuwa chini ya makundi mengine kama SACCOS na Taasisi za kifedha.

Hayo yamebainishwa na Meneja Usimamizi wa Mabenki ya Huduma ndogo za fedha na maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Bw. Victor Tarimo, wakati akitoa mada katika Semina kwa Waandishi wa Habari za Fedha, Uchumi na biashara inayofanyika Mkoani Mtwara.

“Hakuna fedha inayotozwa na Benki Kuu ya Tanzania-BOT kwa ajili ya uendeshaji wa kikundi vya kifedha, na hakuna sheria yoyote inayotaka vikundi hivyo vitoe tozo kwenye Taasisi nyingine yoyote, vikundi ni mali ya wanachama na wanaotoza vikundi hivyo kwa ajili ya uendeshaji wanakosea” alisema.

Aliyasema hayo baada ya Waandishi wa Habari kumwambia kuwa kuna baadhi ya Halmashauri za Wilaya na Manispaa wanatoza vikundi hivyo Shilingi elfu 30 kama gharama za uendeshaji wa vikundi.

“BOT tuliwaambia Mamlaka za Halmashauri za Wilaya kuwa, mnaposajili kundi dogo la kifedha, hakuna kutoza pesa yoyote, kama kuna kundi lipo linatozwa fedha sh elf 30 za usajili watuambia, na sisi tutachukua hatua kwa sababu sio utaratibu tuliowapa”alisema

Alisema kutokana na kuona kuna umuhimu mkubwa wa makundi hayo ya Kijamii kujikwamua kiuchumi kupitia mzunguko wa fedha zao wenyewe, BOT iliamua vikundi hivyo visajiliwe bure na kusisitza kuwa Halmashauri za Wilaya wanalifahamu jambo hilo.
Hii tozo hakuna tangu lini?maana mimi nimesajili kikundi changu mwezi 11 mwaka jana na nikalipia hiyo 30,000 manispaa na risiti ninayo
 
Back
Top Bottom