Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Ligi Kuu ya Tanzania kwa mzunguko huu wa lala salama, hakuna Klabu ya mpira yenye uwezo wa kuifunga Simba SC kutokana ubora wa kikosi.
••Watafanya Nini Sasa Uwezo Hamna
Simba SC imekuwa ikitandaza gozi la ng'ombe vema kabisa kwa viwango vya juu, huku wakipiga pasi za maana zilizothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) na kusababisha Simba SC kupata matokeo chanya.
Klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi wao wanachokifanya ni kutiririka tu kwenye mtelemko wa kuzoa pointi tatu kila mchezo, Yanga kachukua kidude 1-0 Uwanja wa Taifa, African Lyon kagaragazwa 3-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Azam FC kachapwa 3-1 Uwanja wa Taifa, klabu ambazo kidogo zilikuwa zikitegemewa kuleta upinzani wa kupata walau sare, kwa mukhadha huo hakuna kwa sasa timu ambayo itaifunga Simba SC kwenye TPL.
••Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa
Katika mwendelezo wa kukusanya pointi tatu tatu kila sehemu, kwa sasa kituo kinachofuta ni Ipogolo mkoani Iringa ambapo Lipuli watalazimika kushuka katika eneo lao nakuacha pointi tatu huku safari ya Watakatifu Simba ikiendelea.
Klabu ya Simba imeondoka leo kuelekea mkoani Morogoro ambapo leo jioni watafanya mazoezi kisha kesho asubuhi wataanza safari kuelekea mkoani Iringa ambako Jumanne itakipiga na Wanapaluhengo Lipuli FC.
Niiii Ghazwat kwa niaba ya sembo OKW BOBAN SUNZU Shunie King Ngwaba Sapta Sapta Tui tunawaambia watani zetu Sibonike Mwana Mtoka Pabaya Shadeeya Prince Kunta Kila timu ishinde mechi zake..!
Sent using Jamii Forums mobile app