SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,079
- 7,976
Hata mkitaka kuhamishia Bunge la Tanzania Chato hakuna TATIZO.
Nimekaa nakutafakari sasa tunakoelekea sio pazuri.
Serikali inajenga hospitali ya rufaa Chato, wafuasi wa upinzani wanazodoa na kupinga.
Kwani hii Hospitali haitawahudumia Watanzania?
Kwani kujengwa Chato ndio tatizo?
Mfano, mkazi wa Dar es Salaam akiwa Runzewe anaendesha truck kwenda Rwanda,ghafla anapata ajali,Je hawezi kupelekwa Chato na kupata huduma za tiba? Huu ni mfano.
Nini hasa kinawafanya mzodoe na kupinga ujenzi wa hii hospitali muhimu? Rais JPM kuwa ametokea Chato?
Nadhani ni kipindi muafaka Askofu Bagonza na Askofu Mwamakula kuwaombea hawa vijana waliokengeuka kisiasa ili uzalendo uwarudie na kuipenda nchi yao.