Hakuna tatizo miradi mikubwa ya kimkakati kuelekezwa Chato

Serikali inajenga hospitali ya rufaa Chato,wafuasi wa upinzani wanazodoa na kupinga.
Mimi pia nimetafakari kauli yako. Hao wanaozodoa umejuaje kama ni wafuasi wa upinzani? Mbona nchi hii hakuna wapinzani? Chama tawala kimepata uungwaji sehemu zote nchini, sasa iweje tusikie tena kwamba kuna wapinzani? Mimi nashauri ufanye utafiti wa kutosha ili ujiridhishe kujua wanaozodoa hasa ni nani
 
Hospitali ya rufaa kanda ya ziwa iko Bugando Mwanza.
Kanda ambazo hazina hospitali za rufaa za kanda ni:
1. Kanda ya magharibi: mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi (hata Tabora ni mbali na Dodoma na Mwanza)
2. Kanda ya kusini mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma

Nilitarajia kama hospitali za rufaa za kanda ni kipaumbele, basi zingeanzia katika kanda hizo ambazo hazina
Hospital ga kanda ya kusini hiyo mzee inajengwa
images%20(19).jpg
images%20(17).jpg
images%20(18).jpg
 
Ama kweli wachato mmebarikiwa nyrere alikuwa lofa Sana.

Airport chato
Referal hospital chato...
Na ukiangalia taarifa ya habari wananchi wanafyeka poli na kudai hawana shule ya wasichana hitimisho mkuu wa mkoa anaunga juhudi tunajenga shule hapa sabsbu wana tabu.

Mara unaweza kuta habari ya soko sijui limeungua hitimisho linakuwa miundombinu hii imechoka inabidi tubadilishe.Yaani kwa sisi tunaoangalia habari channel zote(saa moja na nusu usiku hadi saa tatu,tbc,itv,utv,startv,zbc,cloud na etv ndio tunaona vihabari ambavyo hitimisho ni kujengwa shule, barabara, hospital na ni maeneo ya polini na wanaolalamika hao wananchi hawavuki 200.

Nahisi ni wanachama wa CCM waliopangwa kwenye haya matukio ya kudai maendeleo katika hatua ya kata,au kijiji.Halafu Mh yeye anaweka kubwa kubwa mnazopigia kelele.
 
Nimekaa nakutafakari sasa tunakoelekea sio pazuri.

Serikali inajenga hospitali ya rufaa Chato,wafuasi wa upinzani wanazodoa na kupinga....
Labda kwa ufafanuzi anayejua zaidi. je hii ni Hospitali ya RUFAA YA MKOA au ni ya RUFAA YA KANDA?
 
Kumbuka watumishi wa umma wanaingia mwaka wa sita na mshahara ule ule wa July 2015.
I have no Problem with this trust me, Hali ya mfumuko wa bei ikoje kwa sasa?, Kuna muda kama wananchi lazima tupite vipindi vigumu ili tuweze kukaa sawa na kuimarika kama nchi. Kwa upande wangu na Maoni yangu kamili kabisa sioni shida kwa kua yapo mambo ya msingi yanaendelea so acha tuteseke ila tuendelee kuzaa ili watoto waje kukuta mambo mazuri.
 
Nimekaa nakutafakari sasa tunakoelekea sio pazuri.

Serikali inajenga hospitali ya rufaa Chato,wafuasi wa upinzani wanazodoa na kupinga...
Hakuna anayepinga, kimsingi bali wanahoji na hoja zinahitaji kujibiwa kwa hoja zenye mantiki na uhalisia wa mambo.
Mfululizo wa yanotendeka chato kipindi hiki tena kwa kasi ndio msingi wa hizi hoja. So kujadili ni jambo zuri tu.
 
Lazima iunganishwe, haiwezekani kila kitu chato, tena fast track
Kanuni za uongozi zinagoma kuendekeza ukabila,ukanda,kujipendelea kwenu pasipo ulazima wa tija coz ni sumu mbaya sana upandwa ktk taifa kesho ataingia mwingine nae atapendelea kwao na kutelekeza maeneo mengine
 
Kwani lazima kila mradi wa maendeleo ujengwe makao makuu?
Let people question tusitake kujenga taifa la watu wa ndio kwa kila kitu.
Watu si wajinga kihivyo. Why/why not; Butiama, Kisarawe, Msolwa, Chato etc. Yote haya yanahusishwa na wenye mamlaka!
Huu ni ulimwengu. Sio mbingu ili watu wote waimbe "utukufu kwa Mungu juu.. "
Kwa nini tumeamua kuimba " utukufu kwa mtu aliye juu..
Mnaoimba endeleeni lakini hamtaiona mbingu maana mnayemwimbia sio mkuu wa mbigu na Mungu wetu ni mwenye wivu...
 
Mkuu ili kufungua hospital kwabwa namna hiyo somewhere kuna factor nyingi unaconsider and one of them inaweza kuwa accessibility etc.Chato inaweza isiwe na sifa hata moja kati ya hizo
Sifa kubwa na ya pekee ni makao ya mfalme
 
Kanuni za uongozi zinagoma kuendekeza ukabila,ukanda,kujipendelea kwenu pasipo ulazima wa tija coz ni sumu mbaya sana upandwa ktk taifa kesho ataingia mwingine nae atapendelea kwao na kutelekeza maeneo mengine
Mwafrika akiwa kwenye nafasi kupapendelea kwao hiyo ni jambo la kawaida
Asipopapendelea napo mtakuja mlaumu na kumsema+kumcheka
Kuna mwingine yuko kwenye nafasi kubwa lakini kwao hapafanyi lolote huo ni ubinafsi

Nyumbani kwanza kwa maisha ya badaye

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nimekaa nakutafakari sasa tunakoelekea sio pazuri.

Serikali inajenga hospitali ya rufaa Chato, wafuasi wa upinzani wanazodoa na kupinga.

Kwani hii Hospitali haitawahudumia Watanzania?

Kwani kujengwa Chato ndio tatizo?

Mfano, mkazi wa Dar es Salaam akiwa Runzewe anaendesha truck kwenda Rwanda,ghafla anapata ajali,Je hawezi kupelekwa Chato na kupata huduma za tiba? Huu ni mfano.

Nini hasa kinawafanya mzodoe na kupinga ujenzi wa hii hospitali muhimu? Rais JPM kuwa ametokea Chato?

Nadhani ni kipindi muafaka Askofu Bagonza na Askofu Mwamakula kuwaombea hawa vijana waliokengeuka kisiasa ili uzalendo uwarudie na kuipenda nchi yao.
Mbona viongozi wote waliomtangulia hawakuthubitu kufanya hivyo? Nenda Butiama licha ya Mwalimu kukalia kiti kwa miaka 24, nenda kwa Mzee Mwinyi, Lupaso tulipashuhudia wakati wa mazishi ya Ben, JK licha ya kupenda bata nenda Msoga uone.

Huyu kila kitu ni Chato, imekuwa "too much" sasa!
 
Nimekaa nakutafakari sasa tunakoelekea sio pazuri.

Serikali inajenga hospitali ya rufaa Chato, wafuasi wa upinzani wanazodoa na kupinga.

Kwani hii Hospitali haitawahudumia Watanzania?

Kwani kujengwa Chato ndio tatizo?

Mfano, mkazi wa Dar es Salaam akiwa Runzewe anaendesha truck kwenda Rwanda,ghafla anapata ajali,Je hawezi kupelekwa Chato na kupata huduma za tiba? Huu ni mfano.

Nini hasa kinawafanya mzodoe na kupinga ujenzi wa hii hospitali muhimu? Rais JPM kuwa ametokea Chato?

Nadhani ni kipindi muafaka Askofu Bagonza na Askofu Mwamakula kuwaombea hawa vijana waliokengeuka kisiasa ili uzalendo uwarudie na kuipenda nchi yao.
Hivi kule Butiama kuna jengo gani au taasisi gani kulinganisha na hiyo miradi iliyopo hapo chatou?
 
Ipo kwenye ilani ya CCM, ni utekelezaji wa ilani ya chama chetu!

Someni ilani ya chama ya Serikali inayotuongoza ili muwezi kujua ni nini kilifanyika na nini kinatakiwa kufanyika.
Screenshot_2021-01-12_101046.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom