Hakuna taifa linaloweza endelea kwa kuongeza tozo bali kwa kuchochea uzalishaji

Kwenye ATM sasa kutakuwa na foleni. Kamakutoa 400,000 CRDB kwa njia ya ATM nakatwa 1,000. Kwanini nihangaike na simu!
Maendeleo hayana chama lipa kodi wapinzani walituchelewesha sana
 
Wewe mleta mada sio kuwa umetumwa na Mwigulu ili njia zetu mpya nazo mzibanie...

Hatuuzi ramani ya vita ng'oo
 
Hili jambo limetufika wote na linatuathiri sote hawa watu wamedhamiria kutufanya tuzidi kuwa masikini huku wao wakineema.Dunia nzima Hakuna tozo kama hizi,tupeana maujuzi zaidi jinsi ya kukwepa dhuluma hizi tutumie nini sasa kufikisha pesa tutumie uber, bodaboda, parcel,mtu,konda, haingilii akili tozo za ajabu kabisa hizi,hata Magufuli asingezikubali achilia madhaifu yake zenye lengo la kuwafanya watz wazidi kuwa masikini,hali inajulikana kuna matumizi mabaya Sana ya Kodi pasipo tija kwa mlipa kodi.
Hawa watu waliokosa ubunifu awaelewi kwamba tozo hizi zinakwenda kuuwa ajira na uchumi wa wengi.Mtza anakamuliwa haswaa tozo za simu bei juu,mafuta bei juu,mbolea bei juu yaani wamelenga mle mle panapogusa maisha ya hali ya chini Ili kuwadidimiza.
Hakuna taifa linaloweza endelea kwa kuongeza tozo bali kwa kuchochea uzalishaji Ili export ikue.
Tumetoka kuisoma namba leo tunazikwa kabisa hawana huruma kabisa hawa.
Kuna mtu alikuja na uzi jana Mods wakaufungia haraka sana sijui kwanini ila uzi ule pia ulielekeza kujiunga kwenye netwok fulani kisha unapata kutuma fedha bila gharama
 
Alafu utasikia makampuni ya mabilioni yanasamehewa kodi
Itoshe kusema Tanzania ni failed state. Tunaendelea kuthibitisha hilo kila uchwao.
Tuna "mavi"ongozi yanaongoza nchi.
Mwigulu ni mbaya sana!! Yaani siku hizi naonekana kama boda boda vile! Gari kitambo nimepaki tu! Yaani mimi ndiyo wa kupanda Shambalai na Vuga line kweli!!!
tatizo ni serikali, majiniasi wameshaleta mobile money, serikali imeleta tozo.
Tatizo ni Msoga Family
 
... wataidhibiti hiyo kaka! Ni suala la muda.
Sio rahisi,walishindwa ile ya ile hela tuma kwa namba hii ndo wataweza hii ya kutuma float maana wakala anakusanya pesa anapeleka bank anajaziwa float na mwingine nae anaenda bank kutoa float communication ndio zinatembea.
Sijui kama hawa jamaa wanajua hata Sheria na kanuni za kodi? Kodi ikiwa kubwa ni lzm itakwepwa tu.
Waliosema toza kidogo ukusanye kingi walishafanya study.
Na kichaa kweli niwape elf 30 kutuma na kutoa pesa kwann nisimpe wakala kula elf 5 hamisha float.
Hii fursa kwa mawakala kupiga pesa sasa.
 
hivi watanzania hatuwezi kubuni "bitcoin" yetu?
Nipo njiani natoka Shinyanga kupeleka hela, nimeokoa gharama za Mpesa na chenji ya bia juu, jamaa niliyekuwa nampelekea nimemsaidia kufungua akaunti benki... kwaheli MPESA!
 
Dawa ni kupunguza tu matumizi ili hayo makadirio yao yasitimie. Mimi kwa sasa natumia pikipiki muda wote! Bora niitwe bodaboda. Nikisafiri napanda Shambalai kudadeki!

Miamala nitafanya ile isiyokwepeka tu! Iliyobaki yote, bora nimpe mtu hela kwa mkononi.
Bora uitwe bodaboda, una maana gani
 
Mwenye nyumba wangu anaishi km 10 kutoka nilipopanga. Huwa natuma Kodi kwa MPesa lakini leo nimeamua kupanda daladala kwenda 400 kurudi 400 ili nimpelekee kodi yake!
 
Hawa wachawi wa kupenda kodi wasitolea jasho wapo wengi. Kitakachofuatia wataanza kutunga visheria vya kula sahani moja na wakala na kampuni za simu. Ilasina shaka chochote kilichoundwa na binadamu kina weakness, tutakula nao sambamba hizo kodi za ujamaa sijui uzalendo wakaziongee kwenye vikao vyao.
 
Kuna mtu alikuja na uzi jana Mods wakaufungia haraka sana sijui kwanini ila uzi ule pia ulielekeza kujiunga kwenye netwok fulani kisha unapata kutuma fedha bila gharama
Na hawa humu sina imani nao tangu 2016 nilishaacha kujadili mambo mazito humu ni muda tu wataanza kutuchomea kwa wenye nchi kwa kugawa data zetu.
 
Na hawa humu sina imani nao tangu 2016 nilishaacha kujadili mambo mazito humu ni muda tu wataanza kutuchomea kwa wenye nchi kwa kugawa data zetu.
Asante mkuu hii ni alert nzuri
 
Ni bora kumpa wakala elf 5 ale akuhamishie float kwa wakala mwenzake kisha ampe mtu wako kuliko kuwapa hawa elf 35 yote ya nini.
Kumbe nyie ndio mnatuibiaga ATM
Mna elimu ya uchumi kuliko Madelu.
Bongo ni Bongo FLOT SERVICE!
 
Nimejaribu jana kutuma kwa bodaboda ila nilimwambia ukweli kuwa hii bahasha ina hela na slip fulani ya bank, sema roho inakuwa juu kidogo!
Jf members wote muwe mnanituma mim il roho zisiwe juu juu
Mimi bodaboda ni mwaminifu mno, hata ukiniacha na mkeo week nzima utamkuta salama kabisaaah!
 
P
Kama ni mfanyabiashara wateja zako wote wa mikoani wape account # hela zipite humo (mimi toka jana hata 50,000/= mawakala wa NMB wametapakaa kila mahali nimewaambia wateja waweke pesa humo nitazitoa kwa wakati wangu la kama mtu anaona hawezi nimetengeneza kiji-chart kinachoonyesha bei mpya za kutoa pesa namtumia picha kisha yeye aangalie kiasi anachotuma kama ataweza atume na ya kutoa hiyo pesa hawezi tuvunje biashara)

Kama biashara yako inakulazimu kununua mzigo wa mteja nje ya kitengo chako jenga utaratibu kila wiki kwenda kukaa foleni utoe kama 3mill kwenye teller ikae tu karibu ili hela ya mteja ikishaingia kwenye acc unanunua mzigo unatuma,waajiriwa yale mambo ya kuhamisha hela kutoka bank then ukatoe kwa wakala kwa sababu ATM machine za bank yako ziko mbali sasa achana nayo tembea na ATM card yako ukitaka kwenda kutoa pesa piga kabisa hesabu zako pesa unayoenda kutoa iwe na ziada ya siku nne mbele kimatumizi.

Kuishi Africa hasa hizi nchi zinazoongozwa na vyama kama ccm inakutaka utumie akili sana,ni vile sisi yanatufika leo kuna wenzetu haya wameshayazoea wanaishi nayo.picha chini ni muamala alifanya mteja wangu jana yupo Ilula aliniwekea hela kwenye acc nikaenda kuitoa ATM cost yake haikuzidi Tsh 4,180/= wakati tozo za mchemba zikinitaka niitoe kwa Tsh 15,200/=View attachment 1855668
Mnajianika. Pesa za njia ya mtandao wakala kwa wakala nazo zitapigwa tozo tuone. Mmetusaidia kujianika serikali haishindwi kitu.
 
Back
Top Bottom