Hakuna sababu ya kuzuia kumsherekea Mwokozi wa Ulimwengu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
HAKUNA SABABU INAYOZUIA WATU WASIMSHEREKEE MWOKOZI WAO

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Imani zipo tofauti, kila mtu anaamini katika kila anachoona ni sahihi. Linapokuja suala la dini serikali lazima iwe makini hasa, sio serikali, mtu yeyote yule awe makini sana.

Mimi ni Msabato kwa asili, nililelewa hivyo, nilifundishwa na kuamini kuwa ni marufuku kufanya kazi siku ya Sabato kwani ni siku ya kupumzika na kumuabudu mwenyezi Mungu. Kama amri za Mungu zinavyosema katika kutoka 20:8

Nikiwa chuoni pale Udsm wapo baadhi ya Ma-Dr na Maprofesa walikuwa wakitoa mitihani siku za sabato. Wengine walikuwa wakaidi licha ya kuwaelezea, lakini nilichokigundua ni kuwa imani ni kitu kingine kabisa. Huwezi amini, nilikuwa tayari hata kusimamishwa masomo au kuacha Chuo kama baadhi ya wakufunzi wangu waliokuwa wakinitisha kupima msimamo wangu. Bahati nzuri sikuwa pekeangu, walikuwepo na wengine.

Sio chuoni tuu, hata mtaani linapokuja suala la Mungu wangu hakuna mtu wa kuniambia chochote, yaani uniambie chochote dhidi ya aliyeniumba, big noo!

Sasa tamko la kutosherekea kufufuka kwa Yesu kwa kweli aliyeifikiria ajitafakari kabla aliyemuumba hajamtafakari yeye na kizazi chake. Najua kuna kukosea, lazima tuseme aliyetoa hilo tamko amekosea pakubwa sana kwa waamini wa dini za Kikristo.

Pengine hawamjui huyo Yesu anayeshangiliwa ni nani, kama kwako sio kitu kwa wenzako ni kitu;

1. Yesu ni Mungu kwa mujibu wa Imani ya Kikristo
2. Yesu ni Mkombozi wa Ulimwengu, kakukomboa wewe na mimi.
3. Yesu ndiye pekee aliyeshinda kifo
4. Yesu ndiye njia ya kumfikia Mungu mkuu
5. Yesu ndiye Uzima
6. Yesu ndiye atakayekufufua wewe na mimi utake usitake.

Watu waliosema watu wasimshangilie Yesu hawakuanza leo, tunasoma katika Luka 19:
37. Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;
38. Wakawa wanasema: “Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana. Amani mbinguni, na utukufu juu mbinguni!”
39. Hapo baadhi ya Mafarisayo waliokuwako katika lile kundi la watu wakamwambia Yesu, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako!”
40. Yesu akawajibu, “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, hakika hayo mawe yatapaza sauti.”

Anayeshangiliwa katika sikukuu ya Pasaka sio Taikon, sio Rais,sio waziri, sio jemadari au mtu yeyote, bali ni MKOMBOZI WA ULIMWENGU, Hilo lazima kila mtu alijue.

Anayeshangiliwa ndiye atakayemfufua Hayatti Magufuli,
Anayeshangiliwa ndiye atakayemfufua Hayatti Nyerere
Anayeshangiliwa ndiye atakayemfufua Hayatti Mkapa
Anayeshangiliwa ndiye atakayekufufua wewe na mimi.
Anayeshangiliwa ndiye atakayefufua watoto wetu
Ndiye atayefufua wake na waume zetu, alafu unaanza kuthubutu kusema mtu wa namna hiyo asifanyiwe shangwe, nderemo na shamra shamra.

Nafikiri hata Hayatti Magufuli mwenyewe angekuwepo asingefikiri kwa namna hiyo, yaani watu wasishangilie kwa Mungu atakayemfufua.

Hata hivyo siku yenyewe ni siku moja tuu, na hata ingekuwa wiki nzima, haizuii watu kumshangilia mwokozi wao.

Nawaasa ninyi viongozi wa kisiasa, jeshi la polisi na watu wote wenye dhamana ya uongozi, kuna mambo sio yakuyaendea kwa pupa kwa kutaka utukufu wa wanadamu, badala ya utukufu wa Mungu, gharama yake ni kubwa.

Lazima hili niwaambie wazi wazi pasipo kificho, kanuni ni ile ile, "Ya kaisari mpe Kaisari, na ya Mungu mumpe Mungu"
Ingekuwa ni sikukuu ya kiserikali tungesema hapo sawa, lakini sikukuu za kidini ambazo watu huamini wanafanya kwa ajili ya Mungu wao, hapo ni Big Noo.
Sasa wewe jitie kihere here na mwenye kiburi cha uzima kwa cheo cha mkopo hicho au pesa za kuazimwa ukajisahau kuwa wewe sio lolote na sio kitu bila kumcha Mungu.

Watu lazima washerekee iwe iwavyo, kumsherekea Mungu sio kosa kwa vyovyote vile.

Lakini hapa pia niweke sawa, utararibu wa kusherekea sherehe za kiroho unafahamika, watu wale chakula kizuri, wanywe vinywaji halali, wasikilize muziki wa kiroho, waimbe na kumtukuza mwokozi wao.

Lakini sio zile sherehe haramu, za kuliza miziki ya kidunia, kunywa pombe, kuweka madisko kwenye makumbi ya starehe ya kidunia, kufanya uashereti, huko sio kusherekea sikukuu za Kiroho.

Hivyo Polisi mipaka yao ni kuzuia sherehe na shamra shamra zisizo za kiroho, na naungana nao kwa asilimia mia moja.

Lakini siwezi kuungana nao kwa vyovyote vile, wakizuia shamra shamra na kushangilia kuliko ruhusiwa kidini. Watu wapike wavae vizuri, waende kanisani, wakirudi wale chakua kizuri, wanywe, wacheze na kumuimbia Mwokozi wao.

Hata hivyo, siku hiyo inaweza kutumika kumuombea Hayatti Magufuli kwa Mwokozi wa ulimwengu ambaye yeye ndiye atamfufua siku ile ya kutisha itakapofika

Mungu ndiye Mtawala, huyo ndiye tunamtumainia na ndiye nguzo yetu.

Ulikuwa nami mwana kutoka Nyota ya Tibeli

Robert Heriel
Taikoni wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hvi Easter ndo Pasaka? Ndo kufufuka Kwa Yesu? Sometyme muwe mnatumia akili bas...hata kufanya reasoning mmeshindwa
 
Usitumie akili kwenye imani za watu, tumia akili kwenye imani yako. Hii itakuepusha na Migogoro

Wewe una reasoning ipi ukijitathmini mkuu, uniambie humu?
Fanya reasoning kwenye Easter kuitwa Pasaka , usiwe mvivu wa kufikri
 
Fanya reasoning na wewe usiwe mvivu wa kufikri

Nimeshakuambia fanya reason kwenye imani yako sio imani za wenzako, kama ungekuwa na reason ingetosha kuelewa nasema nini, ila bado unanifanya nikufikirie tofauti.

Reason fanyie kwenye mambo ya imani yako
 
Bwana Yesu si ndio Wengine wanamuita Issa, Basi haina budi kumuheshimu, maana Wanajua mamlaka aliyo pewa Duniani na Mbinguni, Mwenye Masikio na asikie na Mwenye Macho aone.
 
Back
Top Bottom