Waziri Silaa ameweka jiwe la msingi Shule ya Sekondari Sekoutoure iliyogharimu zaidi ya Shilingi bilioni moja

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,825
13,584
Waziri Habari, Mawasiliano na Teknilojia ya Habari, Jerry William Silaa ameweka jiwe la msingi Shule Mpya ya Sekondari Sekoutoure iloyopo Kata ya Ilongero Wilaya ya Singida kuashiria uzinduzi rasmi wa shule hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni moja.
WhatsApp Image 2024-10-25 at 18.12.40_17432d7d.jpg

WhatsApp Image 2024-10-25 at 18.12.36_fae36dfa.jpg
Shule hiyo mpya iliyojengwa ililenga kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule ya sekondari Ilongero na kuwapunguzia adha wanafunzi kutembea umbali mrefu baadhi ya wanafunzi waliokua wakisoma shule ya Sekondari Ilongero imezinduliwa rasmi leo Oktoba 25, 2024.

Akizungumza maara baada ya kukagua majengo na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo Waziri Silaa amesema hiyo ni sehemu tu ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu nchi nzima ikiwa ni pamoja na Mkoa wa singida.

Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule hiyo mpya iliyoanza rasmi januari 2023 ikiwa na idadi ya wanafunzi 483 hadi sasa kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa kuwa tayari Serikali imeweka miundombinu bora katika shule hiyo.
WhatsApp Image 2024-10-25 at 18.12.37_7b168b3c.jpg

WhatsApp Image 2024-10-25 at 18.12.38_ff6c838e.jpg
Akitoa taarifa ya Mradi wa shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Sekoutoure Tatu Njaku amesema ujenzi wa shule hiyo umeboresha mazingira ya Kufundishia na wanafunzi kujifunza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego kwa ujumla wake amesema kwa kipindi cha miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Singida unashule mpya za sekondari 33 ikiwa ni kuendelea kupunguza changamoto za wanafunzi kusoma umbali mrefu.
 
Na hicho kipande cha barabara ya vumbi kutoka igauri kwenda ilongero ukitokea singida mjini kiwekwe lami, iguguno kwenda nduguti yaliko makao makuu ya wilaya ya mkalama nako waweke lami. Ni aibu hadi miaka hii kwenda nduguti ukitokea iguguno usafiri ni wa shida, ni wa kutaiming magari yanayoingia huko si mengi barabara ni mbaya. Mheshimiwa yuko ukanda huo atakuwa kapita barabara za huko ni za ajabu ajabu na wakati kuna makao makuu ya halmashauri mbili huko, mkalama na ilongero
 
Waziri Habari, Mawasiliano na Teknilojia ya Habari, Jerry William Silaa ameweka jiwe la msingi Shule Mpya ya Sekondari Sekoutoure iloyopo Kata ya Ilongero Wilaya ya Singida kuashiria uzinduzi rasmi wa shule hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni moja.
Shule hiyo mpya iliyojengwa ililenga kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule ya sekondari Ilongero na kuwapunguzia adha wanafunzi kutembea umbali mrefu baadhi ya wanafunzi waliokua wakisoma shule ya Sekondari Ilongero imezinduliwa rasmi leo Oktoba 25, 2024.

Akizungumza maara baada ya kukagua majengo na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo Waziri Silaa amesema hiyo ni sehemu tu ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu nchi nzima ikiwa ni pamoja na Mkoa wa singida.

Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule hiyo mpya iliyoanza rasmi januari 2023 ikiwa na idadi ya wanafunzi 483 hadi sasa kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa kuwa tayari Serikali imeweka miundombinu bora katika shule hiyo.
Akitoa taarifa ya Mradi wa shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Sekoutoure Tatu Njaku amesema ujenzi wa shule hiyo umeboresha mazingira ya Kufundishia na wanafunzi kujifunza.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego kwa ujumla wake amesema kwa kipindi cha miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Singida unashule mpya za sekondari 33 ikiwa ni kuendelea kupunguza changamoto za wanafunzi kusoma umbali mrefu.
Jina lake la ukoo ni Silaa/Silaha/Si-raha/Slyaa/Slaa au linaandikwaje?Hebu ukiwa unachukua taarifa mpe kalamu aandike linavyotamkwa.Kubadili uandishi halali wa jina la mtu ni kosa.
 
Kwa idadi ya hayo Majengo (14) ukifanya makadirio ya shilingi milioni 50 Kwa Kila Jengo, unakuta gharama halisi ni kama milioni 700 hivi

Sasa hiyo bilioni 1 imetoka wapi au ndiyo kula Kwa urefu wa kamba??🙌
 
Kiongozi unaweza kuwa sahihu kabisa japo ujue shule sio majengo pekee;
1. Yaweza kuwa kwenye hayo majengo kuna maabara ya kueleweka inayo gharimu fedha nyingi
2. Madawati ya chuma ya kueleweka
3. Computer Lab ya kueleweka
5. Na kwa sababu ni mpya kuna vitabu vingi na vifaa kadhaa vimenunuliwa + Library
6. Ingefaa, ningependekeza waajiri kabisa na mwalimu wa Hesabu/Physics & Biology kwani hao ni hadimu
 
Kiongozi unaweza kuwa sawa kabisa japo ujue shule sio majengo pekee;
1. Yaweza kuwa kwenye hayo majengo kuna maabara ya kueleweka inayo gharimu fedha nyingi
2. Madawati ya chuma ya kueleweka
3. Computer Lab ya kueleweka
5. Na kwa sababu ni mpya kuna vitabu vingi na vifaa kadhaa vimenunuliwa + Library
6. Ingefaa, ningependekeza wajiri na mwalimu wa Hesabu/Physics & Biology kabisa kwani hao ni hadimu
Nimekupata boss
 
Back
Top Bottom