Hakuna mwenye CCM, kinachofata kitaduwaza wengi

Hiki chama mwanzoni tuliaminishwa kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi!

Ila kwa awamu kadhaa sasa kimeingia kwenye mikono ya watekaji wabaya na makatili kupitiliza.
Watekaji wa kwanza walikuwa ni matajiri na wafanyabiashara wakubwa (akina Rostam Aziz, Lowasa, and Co. Ltd), Baadaye wakaja Sukuma Gang wakishirikiana kwa ukaribu na Mataga na waimba mapambio! Na kwa sasa chama kipo mikonono mwa Wakojan na Msoga Gang!!

Yaani ni bandika bandua! Hatupewi kabisa wasaa wa kupumzika! Na hawa watekaji wote wapo kwa ajili ya maslahi yao tu! Na siyo kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Katiba Mpya ya Wananchi kwa sasa haikwepeki.
Bila katiba mpya ni kupoteza muda tu.
 
Samia anajua NGOs hakijui Chama wala serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.Jamani hata Ridhiwani anakuwa Waziri!No,hii haikubaliki,hatuwezi kuchezewa namna hii,viongozi wenye uchungu na nchi hii mko wapi?
kwani sio mtanzania?
 
Wasukuma walituharibia sana nchi yetu. Wazee walidharirishwa sana, vijana tulibambikiwa kesi za kumtukana jiwe. Yaani mambo yalikuwa hovyo kabisa.

Tunaomba Mungu mbali na kutukomboa lakini wale waliohisika wakamatwe.

Hii hata Sabaya katika utetezi wake anasema alikuwa anatumwa na yule muovu shetan
Kuwa kichaa sio mpaka usijuwe kutumia smartphone
 
Anayefikiri CCM ina wenyewe anapoteza Muda na huenda haijui CCM.
Kama CCM ina wenyewe basi familia ya Nyerere ndio wenye chama....
Ila ikiwa mwanzilishi wa hili Taifa familia yake haipo popote basi tulieni muone kitatokea.

Endeleeni kubwabwaja sasa
 
Anayefikiri CCM ina wenyewe anapoteza Muda na huenda haijui CCM.
Kama CCM ina wenyewe basi familia ya Nyerere ndio wenye chama....
Ila ikiwa mwanzilishi wa hili Taifa familia yake haipo popote basi tulieni muone kitatokea.
Uko busy kuhangaika na tu thread uchwara wiki hii yote.

Kunywa maji utapata stroke kwa stress
 
Mwenye CCM ni mwenyekiti na CC yake. Ukishika hapo vizuri mambo mengine yote mtelezo.

Labda uzingue saaaana kiasi cha TPDF na kaunda suti (wazalendo uchwara) waanze kujiuliza kama unahatarisha nchi.
Huwa najiuliza kila wakati,kuharibu ama kuhatarisha nchi ni kufanya tendo lipi?Hao wanaoilinda nchi isiingie hatarini ni akina nani na hupatikanaje?Wanapatikanaje na wanasimamiwa na nani?Wao ni super Tanzanians?
Mwl.Nyerere alipambana na wanaotaka kuharibu nchi kwa miaka zaidi ya 24,Mzee Rukhsa naye akajitahidi kwa miaka 10,alipokuja Mr Clean BM na ukweli na uwazi tukadhani tumepata wa kuwaangamiza kabisa maana tuliamini tutaambiwa ukweli.Adui aliendelea kuwa tishio.
Alipoingia Mzee wa Anga kwa kasi,ari na nguvu mpya tukaaminishwa kuwa tunaenda mbele kumbe?
Hawa maadui wa nchi hii wakavuka enzi zote hizo wakiwa salama hata lilipokuja hadi linaondoka Bulldozer/tingatinga,adui yule yule bado yupo pale pale.
Je,bado wale wanaosemekana wanailinda nchi wapo imara?Nchi hii imelindwa kama tunavyoaminishwa?Je,tunamfahamu au tunaelekea kumshinda adui wa taifa hili?
 
Anayefikiri CCM ina wenyewe anapoteza Muda na huenda haijui CCM.
Kama CCM ina wenyewe basi familia ya Nyerere ndio wenye chama....
Ila ikiwa mwanzilishi wa hili Taifa familia yake haipo popote basi tulieni muone kitatokea.
Unaonaje ukifafanua.
 
Wasukuma walituharibia sana nchi yetu. Wazee walidharirishwa sana, vijana tulibambikiwa kesi za kumtukana jiwe. Yaani mambo yalikuwa hovyo kabisa.

Tunaomba Mungu mbali na kutukomboa lakini wale waliohisika wakamatwe.

Hii hata Sabaya katika utetezi wake anasema alikuwa anatumwa na yule muovu shetani.
Hujitambui ebu Rudi wakati wa kikwete uone watu wangapi waliumizwa
 
Wasukuma walituharibia sana nchi yetu. Wazee walidharirishwa sana, vijana tulibambikiwa kesi za kumtukana jiwe. Yaani mambo yalikuwa hovyo kabisa.

Tunaomba Mungu mbali na kutukomboa lakini wale waliohisika wakamatwe.

Hii hata Sabaya katika utetezi wake anasema alikuwa anatumwa na yule muovu shetani.
Mmmh basi sasa,msimsingizie Magufuli kwa kila kitu,mkosee maisha wenyewe toka mwanzo mje mpeleke hasira zenu kwa magu.
 
Anayefikiri CCM ina wenyewe anapoteza Muda na huenda haijui CCM.
Kama CCM ina wenyewe basi familia ya Nyerere ndio wenye chama....
Ila ikiwa mwanzilishi wa hili Taifa familia yake haipo popote basi tulieni muone kitatokea.
Ngoja tusubiri tu
 
Back
Top Bottom