Hakuna mwanamke ninaye mchukia kama mama yangu

Wana JF.
Mkasa huu haunihusu mimi kwa namna yoyote ile.
Nime upata toka kwa mtu aliye kua akitoa ushuhuda na ulinitoa machozi sana.
Soma mwenyewe.

527501_10150736141294504_666929503_8827302_420595649_n.jpg

###############....MWANZO....######################################

Hakukuwa na mwanamke ambaye nilikuwa simpendi
kama mama yangu.

Yeye alikuwa masikini wa kutupwa huku uso wake ukiwa unatisha
kwa kuwa tu hakuwa na jicho moja.
Kila nilipokuwa nikimuona nilikuwa nikimkasirikia sana.
Alikuwa akijaribu kunionyesha mapenzi kama mtoto wake lakini
kwangu sikuwa nikitaka kumuona kabisa.

Kuna siku nilikaa nae chini na kumwambia kwamba
nilitamani sana kuwa na furaha katika maisha, akaniuliza kitu gani
kifanyike ili niwe na furaha, kiukweli nikamwambia kwamba kama
angekufa muda huo, hakika ningefurai milele.

Nikafanikiwa kusoma chuo na kwenda nchini Afrika Kusini
kusomea sheria, nilifurahi sana. Sikutaka kurudi nyumbani,
nikaoa huko huko na kupata watoto.

Katika maisha yangu yote hayo hakika sikumkumbuka kabisa mama
yangu, nilikuwa nikitamani sana afe ili niwe na furaha.

Nikafanikiwa kupata watoto wawili huku nikiwa nimejenga
nyumba ya kifaari na kuwa na utajiri mkubwa.

Kuna siku nikasikia mlango ukigongwa, watoto wangu wakaenda
kuufungua mlango, ALIKUWA NI MAMA YANGU amekuja
kunitembelea.

Watoto wangu wakaanza kulia kwani
walikuwa wakimuogopa sana mama yangu kutokana na hali
ya kukosa jicho aliyokuwa nayo, nikaamua kwenda
mlangoni, nilipomuona, alifikiri ningetabasamu, nikamfokea
kwa haira sana
"TOKA NYUMBANI KWANGU KINYAGO
WEWE UNAWATISHA WATOTO
WANGU
".

Kwa sauti iliyojaa upole, mama yangu akaniambia
"SAMAHANI BABA. NAFIKIRI NITAKUWA NIMEKOSEA NJIA" hapo hapo akaondoka.
Nikafanikiwa kutembelea nchini Tanzania, na moja kwa
moja nikaanza kwenda kwenye nyumba ile tuliyokuwa
tunakaa.

Majirani zangu wakaniambia kuwa mama yangu alikuwa amefariki kwa
kuwa tundu la jicho lake lilikuwa limeharibu hadi mishipa ya fahamu,

WALA SIKUHUZUNIKA KABISA ZAIDI YA KUTABASAMU. Hapo ndipo
waliponiletea barua ambayo aliiandika mama yangu na kunipa.
Barua ile ilikuwa imeandikwa hivi.

Mwanangu mpendwa.
Najua kwamba katika maisha yako ulikuwa ukinichukia sana
ila amini kwamba nilikuwa nikikupenda sana.
Ulipokuwa mtoto ulipata ajali, jicho lako likapasuka ila kwa kuwa
nilikuwa sitaki uishi maisha ya kuwa na jicho moja, nikaamua
kutoa jicho langu na kuwekewa wewe ili tu uweze
kuuona ulimwengu kwa macho yote mawili.

Sikutaka kujali ningepata matatizo gani lakini
niliamini kwamba wewe ndiye ungekuwa furaha yangu hasa
kila nitakapokuona unauangalia ulimwengu huu huku ukitumia jicho langu moja.
Mimi mama yako Mpendwa....

###########.....MWISHO...########################

Labda kwa namna moja ama nyingine ume waacha wazazi wako kijijini
wakiteseka huku wewe ukila maisha matamu mjini.
Unajua walitoa upendo kiasi gani kwako kukusaidia kufika hapo ulipo fikia?
Labda hawakukusaidia,....lakini unadhani kuwachunia ni adhabu inayo faaa kabisa?

Mungu na akufungue ufahamu wako,UITAMBUE AMRI YAKE PEKEE YENYE AHADI,....uwapende
na kuwaheshimu baba na mama yako ili upate heri na miaka mingi duniani.

God bless you.
Tht sounded like a bad dream, mhusika hana jinsi ya kukwepa dhambi ya mauti
 
Mungu atusaidie tu, manake kuna wazazi wengine kuwabeba ni Neema. Wana misimamo hao!!!!

Haha,kweli kabisa.
Lakini kwa kua ni mzazi wako inabidi ujifunze tu
kumvumilia kwa tabia zake zote au ujifunze jinsi ya
kwenda nae sambamba asikuharibie mambo yako lakini pia
usimdharau kiasi cha kumtukana kama huyu jamaa.

Kesi kubwa hua unaanzia pale wamama wanapotaka wakuchagulie mke duh.
 
Dah mkuu, thanks. Niliwahi kuisoma hii siku za nyuma, lkn kila ninapokutana nayo tena inagusa sana.. Asante tena na ubarikiwe.
 
Nashukuru kuniongezea hamu ya kumpenda mamangu.Nikikumbuka kupatikana kwangu!!Mama alinambia nusu afe alipo jifungua mimi.

Ni kweli nimejitaidi kumfurahisha kwa mengi lkn simjafikia yeye kwa malezi yake kwangu.
 
Tht sounded like a bad dream, mhusika hana jinsi ya kukwepa dhambi ya mauti

Sio kweli,dhambi pekee isiyo sameheka ni kumkufuru Roho Mtakatifu.
The rest zimekwisha lipiwa,the moment you forgive your self,ukaomba
msamaha kwa Mungu pia,.....ur good to go.
 
Hakuna kama mama na ukitaka upate ufalme wa duniani jaribu kuwa karibu na wazazi wawili hakika ni mafanikiwa tosha
 
Nashukuru kuniongezea hamu ya kumpenda mamangu.Nikikumbuka kupatikana kwangu!!Mama alinambia nusu afe alipo jifungua mimi.
Ni kweli nimejitaidi kumfurahisha kwa mengi lkn simjafikia yeye kwa malezi yake kwangu.

Mimi kilicho niliza ni kupiga picha ya kukuzwa na single parent (mama),...
All the way from kuwa house girl(dada) hadi leo alipo fikia then nije
kumtupa,......i'll never forgive myself.

Help me God.
 
Mie hata sijaisoma
maana navyompenda mama yangu hata siwezi elezea lol
mom is treasure ,
wife wangu nlikuta ana mtoto , i loved they was he love those kids, nlijali na kuheshimu ,
mama always ni wapenzi wa kweli kwa watoto wao
:A S-heart-2:mama ni hadhina:A S-heart-2:​
 
mom is treasure ,
wife wangu nlikuta ana mtoto , i loved they was he love those kids, nlijali na kuheshimu ,
mama always ni wapenzi wa kweli kwa watoto wao
:A S-heart-2:mama ni hadhina:A S-heart-2:​

Wow,i like this.
Unconditional love.
 
Wow,i like this.
Unconditional love.

mkuu,
hakuna kitu kizuri kama kuona mama anatabasamu,
na
watoto ni wazuri always, " bahati mbaya my mom passed away when i was little boy , "

i feel my late mom's love when i see my wife smile with my kids ,

thanks for this thread , i have never tell anyone about this ,
 
Mie hata kama nimelala
nikashtushwa na kisu kifuani kwangu
kufumbua nikamkuta mama

najua si yeye, namwamini kuliko labda hata ninavyojiamini mwenyewe.

Na kila siku nasema, huwezi mpenda mama yako kama anavyokupenda yeye(ukiachia hao wenye matatizo ya kiakili)

na ukitaka pata hisia hii, pata watoto ndio utampenda mama kuliko awali.

Thank u for sharing bro.
Ni experience nzuri sana.

I'll love my mum always.
 
Mie hata kama nimelala
nikashtushwa na kisu kifuani kwangu
kufumbua nikamkuta mama

najua si yeye, namwamini kuliko labda hata ninavyojiamini mwenyewe.

Na kila siku nasema, huwezi mpenda mama yako kama anavyokupenda yeye(ukiachia hao wenye matatizo ya kiakili)

na ukitaka pata hisia hii, pata watoto ndio utampenda mama kuliko awali.

Hilo halina ubishi kwani shida shughuli aliyopata tangia ukiwa tumboni mpaka unakuja kujua kula mwenyewe?
 
Mimi kilicho niliza ni kupiga picha ya kukuzwa na single parent (mama),...
All the way from kuwa house girl(dada) hadi leo alipo fikia then nije
kumtupa,......i'll never forgive myself.

Help me God.

Pole sana.Kwakweli siku utakayo mtupa hata Mungu hatakupa furaha maishani.God wll be with you
 
Hakuna kama mama kumkana mamayako ni sawa kumka mwenyezi Mungu ,hebu fikiri kama mama yako angekutupa ungali mtoto je ungefika hapo ulipo leo fikiria hilo tu utapata jibu lake ,mie nafikiri huyo jamaa hakuwa na akiri timamu ,
 
Back
Top Bottom