Hakuna mwanamke ninaye mchukia kama mama yangu

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Wana Jamii Forums.

Mkasa huu haunihusu mimi kwa namna yoyote ile. Nime upata toka kwa mtu aliye kua akitoa ushuhuda na ulinitoa machozi sana. Soma mwenyewe.

###############....MWANZO....###############
Hakukuwa na mwanamke ambaye nilikuwa simpendi kama mama yangu. Yeye alikuwa masikini wa kutupwa huku uso wake ukiwa unatisha kwa kuwa tu hakuwa na jicho moja. Kila nilipokuwa nikimuona nilikuwa nikimkasirikia sana. Alikuwa akijaribu kunionyesha mapenzi kama mtoto wake lakini kwangu sikuwa nikitaka kumuona kabisa.

Kuna siku nilikaa nae chini na kumwambia kwamba nilitamani sana kuwa na furaha katika maisha, akaniuliza kitu gani kifanyike ili niwe na furaha, kiukweli nikamwambia kwamba kama angekufa muda huo, hakika ningefurai milele. Nikafanikiwa kusoma chuo na kwenda nchini Afrika Kusini kusomea sheria, nilifurahi sana. Sikutaka kurudi nyumbani, nikaoa huko huko na kupata watoto.

Katika maisha yangu yote hayo hakika sikumkumbuka kabisa mama yangu, nilikuwa nikitamani sana afe ili niwe na furaha. Nikafanikiwa kupata watoto wawili huku nikiwa nimejenga nyumba ya kifaari na kuwa na utajiri mkubwa. Kuna siku nikasikia mlango ukigongwa, watoto wangu wakaenda kuufungua mlango, alikuwa ni mama yangu amekuja kunitembelea.

Watoto wangu wakaanza kulia kwani walikuwa wakimuogopa sana mama yangu kutokana na hali ya kukosa jicho aliyokuwa nayo, nikaamua kwenda mlangoni, nilipomuona, alifikiri ningetabasamu, nikamfokea kwa haira sana "TOKA NYUMBANI Kwangu kinyago wewe unawatisha watoto wangu". Kwa sauti iliyojaa upole, mama yangu akaniambia "Samahani baba nafikiri nitakuwa nimekosea njia" hapo hapo akaondoka.

Nikafanikiwa kutembelea nchini Tanzania, na moja kwa moja nikaanza kwenda kwenye nyumba ile tuliyokuwa tunakaa. Majirani zangu wakaniambia kuwa mama yangu alikuwa amefariki kwa kuwa tundu la jicho lake lilikuwa limeharibu hadi mishipa ya fahamu, wala sikuhuzunika kabisa zaidiya kutabasamu. Hapo ndipo waliponiletea barua ambayo aliiandika mama yangu na kunipa. Barua ile ilikuwa imeandikwa hivi.

Mwanangu mpendwa. Najua kwamba katika maisha yako ulikuwa ukinichukia sana ila amini kwamba nilikuwa nikikupenda sana. Ulipokuwa mtoto ulipata ajali, jicho lako likapasuka ila kwa kuwa nilikuwa sitaki uishi maisha ya kuwa na jicho moja, nikaamua kutoa jicho langu na kuwekewa wewe ili tu uweze kuuona ulimwengu kwa macho yote mawili. Sikutaka kujali ningepata matatizo gani lakini niliamini kwamba wewe ndiye ungekuwa furaha yangu hasa kila nitakapokuona unauangalia ulimwengu huu huku ukitumia jicho langu moja. Mimi mama yako Mpendwa.

###########.....MWISHO...###########
Labda kwa namna moja ama nyingine ume waacha wazazi wako kijijini wakiteseka huku wewe ukila maisha matamu mjini. Unajua walitoa upendo kiasi gani kwako kukusaidia kufika hapo ulipo fikia? Labda hawakukusaidia,....lakini unadhani kuwachunia ni adhabu inayo faaa kabisa? Mungu na akufungue ufahamu wako,uitambue amri yake pekee yenye ahadi,uwapende na kuwaheshimu baba na mama yako ili upate heri na miaka mingi duniani.

God bless you.
 
duh! Mkuu title ya sred nilijikuta nasisimka nkafungua!

Ujumbe uliopo ndani ni MZITO SANA na MUNGU wetu atuguse mioyo yetu ili tuwakumbuke wazazi wetu
 
Da mkuu its true nimeprove kuwa hakuna kama mama baada ya shemeji yenu kupata uchungu wa uzazi kujifungua na sasa kulea hakika tuwathamini wazazi
 
Wewe ushaniharibia furaha yangu kwa híi habari mbaya.

Pole sana Husninyo ni kukumbushana tu wajibu wetu kwa
wazazi.
Huyu jamaa ange msikiliza mama yake angempa historia ya
jicho lake,na angeweza kumlipia gharama za matibabu akapona
kabisa.
 
Last edited by a moderator:
duh! Mkuu title ya sred nilijikuta nasisimka nkafungua!

Ujumbe uliopo ndani ni MZITO SANA na MUNGU wetu atuguse mioyo yetu ili tuwakumbuke wazazi wetu

Ni kuomba tu.
Unaweza kujiapiza hutafanya kama jamaa,ukaja kuoa mke
asiye kuwa na ubinadamu na akakuweka kwenye chupa
matokeo yake wazazi unawaona kama vinyago.

Omba mke mwema,omba roho ya upendo na uvumilivu.
 
Pole sana Husninyo ni kukumbushana tu wajibu wetu kwa
wazazi.
Huyu jamaa ange msikiliza mama yake angempa historia ya
jicho lake,na angeweza kumlipia gharama za matibabu akapona
kabisa.

dah! Ahsante kwa kutukumbusha speaker.
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru kwa kututafsria hii story na kuiweka katika lugha yetu ya kiswahili. Nimeshaisoma mara nyingi ikiwa kwa kiingereza lakini haikuwa na msisimko kama hivi sasa.
 
nmeiona kwnye wall yko fb ckuielewa but huku ndo nmejua.. dah vry tochn story.!!!

Psssss,ishia hapo hapo usije mwaga mchele kwenye kuku wengi bana.
Mzima lakini?
Umepata lesson eh?Hope bi mkubwa hata juta kukupa support hadi
hapo ulipo fikia.
 
Tunashukuru kwa kututafsria hii story na kuiweka katika lugha yetu ya kiswahili. Nimeshaisoma mara nyingi ikiwa kwa kiingereza lakini haikuwa na msisimko kama hivi sasa.

Asante sana,ni kusambaza ujumbe tu tupate kukumbushana
mambo ya muhimu.
 
Back
Top Bottom