Hakuna mwanamke ambaye hajawahi ‘kujiuza’


Ishu sio uchumi, ishu ni ile hali ya mwanamke kutaka kukukomoa bila sababu ya msingi, mwanamke kumpa pesa ni kawaida, kumnunulia chakula ni kawaida ila asikuigizie au kuwa na hila. Mwanamke atahitaji kula, tunachokataa sisi ni ile hila ya mwanamke kutaka pesa zitumike kwa israfu, kukukomoa au bila sababu ya msingi au kutaka kukuibia kinamna bila hata uhalisia.
Mfano jana mimi nilikuwa mitaa ya DDC Mlimani park, mwanamke wangu amekuja nisalimia anatokea Kinondoni Hananasif, na ana gari yake. Amekuja tumepiga makange na geji ya mafuta ipo chini, bila kuomba nikamuongezea mafuta kiduchu ya 30k karidhika, karidhika jioni karudi home. Tunachokataa sisi ni ile "njama" baadhi ya wanawake wanawake wanatuletea. Manipulative behaviour zinaonekana tuu, wanaume sio wajinga.
 
Kwahiyo hii ni pamoja na mama yako mzazi,dada yako na mkeo sio?
 
Mwanamke akija kwako low key unamdharau na kumuona cheap, kwahiyo slay queen ametake over ili usimdispise! Mwanamke akija na high class look na mindset ana expect vitu vikubwa kutoka kwako!! Sio kukukomoa tu!
Huyo mwanamke wako tayari atakuwa anamaanisha na anajua wewe ni mwanaume wake na wala hana njaa za kishamba na ndiomaana anaridhika kuwekewa mafuta ya 30k, kuna watu kukuheshimu labda umuwekee full tank! Kwahiyo kila mtu ana vipaumbele vyake! Japo kwa hali ya kawaida kama mna mutual connection,feelings wala hakuna ukomoaji, binafsi naweza kuja na nisile wala nisiombe mia yako, inategemea kama unajikuta kwakweli nakukomoa vzr tu, asante..
 

Hakuna mwanaume amekupenda na hajui kuwa unahitaji upkeep, anafahamu unahitaji kusuka, kuvaa na fedha ya matumizi. Hiyo "high class look" ni sawa ila isiwe manipulative, mwanamke hazuiwi kuwa na "high expectation" popote ila ziwe na uhalisia, zisiwe za kuigiza. Sio kwa sababu upo "high class look" ndio ulete maigizo, kuwa halisi, mwanaume anajua unahitaji mahitaji, yanatakiwa kuwa halisi sio maigizo na israfu katika matumizi.
 
Tasnia ya mapenzi/mahusiano inapitia mageuzi makubwa, Gen Z hamna uvumilivu kabisa mnatutoa kimasomaso kaka zenu. Zamani tulikua tunahudumia na tunaichapa fresh hatukua tunasema 'tunanunua', kununua ni kama ile unaichapa one time unaweka dau mezani na wanakua na centers zao kama Malindi, Red Stone au Black Diamond.

Vijanaa wana hoja wasikilizwe.
 
Dahh ni kweli, kwa bahati mbaya upande huu tuanelewa mambo tofauti! Tatizo ni ku expect too much!!🙌🏾
 
Jamnii nimepamiss Rs na Bd, ila malindi si ilikuwa eneo la biashara? Kwani bado papo?

Poleni kwa kupelekeshwa gen zee😆
 
Dahh ni kweli, kwa bahati mbaya upande huu tuanelewa mambo tofauti! Tatizo ni ku expect too much!!🙌🏾

Hiyo "High expectations" high self esteem ndio mara nyingi inawafanya mnaonekana hamna uhalisia, mna hila, na kupelekea msieleweke. Ukiwa halisi, utaeleweka tuu na mrija utakufikia. Utakula pesa ya mwanaume kwa muda mrefu na bila purukushani. Una mahitaji yako halisi yaseme kwa uhalisia wake. Sio uongeze sifuri mbele.
 
Holoholo naomba nishauri kitu hapa .. Tukiandika mada za namna hii tunahitaji tafakuri ya kina sana kwakuwa ukishasema "WOTE" ni pamoja na mama zetu na Dada zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…