Habari zilizosambazwa hapa JF kwamba kuna sintofahamu kati ya CDM na ITV si za kweli na katika kudhihirisha hilo leo asubuhi habari ya Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Dr Wilbroad Slaa kwenda polisi na kugoma kutoa maelezo imepewa uzito mkubwa kwenye taarifa yake ya habari.Kiongozi huyo mbali ya kupewa muda mrefu lakini pia ITV imeonyesha kundi kubwa la wafuasi wa CDM likimshangilia Dr Slaa na kusukuma gari lake.Pia ITV jana usiku ilionyesha kwa muda wa kutosha hotuba ya Waziri Kivuli wa sheria Tundu Lissu bungeni.
Source:Habari za ITV
Source:Habari za ITV