Hakuna mgogoro kati ya CHADEMA na ITV

Habari zilizosambazwa hapa JF kwamba kuna sintofahamu kati ya CDM na ITV si za kweli na katika kudhihirisha hilo leo asubuhi habari ya Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Dr Wilbroad Slaa kwenda polisi na kugoma kutoa maelezo imepewa uzito mkubwa kwenye taarifa yake ya habari.Kiongozi huyo mbali ya kupewa muda mrefu lakini pia ITV imeonyesha kundi kubwa la wafuasi wa CDM likimshangilia Dr Slaa na kusukuma gari lake.Pia ITV jana usiku ilionyesha kwa muda wa kutosha hotuba ya Waziri Kivuli wa sheria Tundu Lissu bungeni.

Source:Habari za ITV

Hivi Chadema kuna wasemaji wa chama wangapi ninayemjua mie ni Tumaini Makene, ambaye alichukuwa nafasi ya Marehemu Regia, saizi kuna mpya anaitwa Molemo.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Chadema kuna wasemaji wa chama wangapi ninayemjua mie ni Tumaini Makene, ambaye alichukuwa nafasi ya Marehemu Regia, saizi kuna mpya anaitwa Molemo.

Rafiki mambo vipi.
Acha hizo bana.Kamanda yeyote akipata habari anazimwaga jamvini kwa maslahi ya watanzania wote.Haiwezekani kila kitu kumsubiri Tumaini Makene.Hii JF ni ya wote mkuu.Hii sio mali ya Makene wala CDM pekee.Mimi kama raia huru nina haki ya kuleta taarifa nikizipata.Jumamosi njema rafiki.
 
Last edited by a moderator:
Hivi Chadema kuna wasemaji wa chama wangapi ninayemjua mie ni Tumaini Makene, ambaye alichukuwa nafasi ya Marehemu Regia, saizi kuna mpya anaitwa Molemo.

Ndani ya CHADEMA kuna msemaji rasmi wa chama. Wanachama wengine ni wasemaji wasio rasmi. Hatuna haja ya kusubiri hadi Sekretarieti ikae (Au msemaje aje) na kutoa msimamo wa chama kwa mambo madogo madogo! Kule kwenu naona mmemwachia Nnauye Jr kila kitu (kuanzia Lumumba hadi kwenye mashina ya Namtumbo, Namanyere, nk) na sasa hadi ameingia kwenye Madroo ya Ofisi ya Katibu Mkuu wake (Mukama)!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Ndani ya CHADEMA kuna msemaje rasmi wa chama. Wanachama wengine ni wasemaje wasio rasmi. Hatuna haja ya kusubiri hadi Sekretarieti ikae (Au msemaje aje) na kutoa msimamo wa chama kwa mambo madogo madogo! Kule kwenu naona mmemwachia Nnauye Jr ona sasa hadi ameingia hadi kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wake (Mukama)!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com

Pamoja sana kamanda.Hii ya Nape kuingilia majukumu ya Mukama imenisikitisha sana.Hii siyo demokrasia hata kidogo.Aheshimiwe huyu Mzee ingawa hajui kitu.
 
Rafiki mambo vipi.
Acha hizo bana.Kamanda yeyote akipata habari anazimwaga jamvini kwa maslahi ya watanzania wote.Haiwezekani kila kitu kumsubiri Tumaini Makene.Hii JF ni ya wote mkuu.Hii sio mali ya Makene wala CDM pekee.Mimi kama raia huru nina haki ya kuleta taarifa nikizipata.Jumamosi njema rafiki.

Mkuu mie nimeuliza tu kwa nia njema tupo pamoja Kamanda Molemo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Molemo.
Nashukuru kwa taarifa, kwani niliuzunika sana niliposikia ITV 'wamefanya' mambo ya ajabu, nikajiuliza sasa nitaangalia station ipi?
 
Mkuu Molemo.
Nashukuru kwa taarifa, kwani niliuzunika sana niliposikia ITV 'wamefanya' mambo ya ajabu, nikajiuliza sasa nitaangalia station ipi?

Pamoja sana mkuu wangu
 
Back
Top Bottom