Hakuna Komandoo wa shida: Kuwa Mshauri na kuomba msaada unapokwama

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,814
Watu wengi huamini kwamba mtu anayebeba matatizo ya wengine yeye hana ya kwake. Hali hii humfanya mhusika akipata tatizo ashindwe kusema.

Fikiria mtu aliyekushauri uache bangi, siku akikuambia ameangukia kwenye kuvuta utamwelewa?

Tunapenda kusema mtu akiwa na depression aseme. Lakini akisema atasaidika? Au ndo mtamgeuza topic vijiweni?

Unamshirikisha rafiki yako unayemuamini, kesho yake unaikuta story yako kwenye group la whatsapp au page za udaku. Badala ya kupunguza depression unaongeza.

Wengine hawapokei simu. Lakini ukifanya "maamuzi magumu" wanaandika caption ndefu kwamba ungesema. Sasa ningesema wapi na hukupokea simu mwezi mzima?

Ndio maana mara nyingi mtu huamua kukaa na matatizo yake mwenyewe. Maana akisema na asiposema yote ni sawa tu. Tena akisema inaweza kumuathiri zaidi kuliko asiposema.

Joel licha ya kuwa MC alikua pia Mshauri nasaha (Counsellor) na Inspirational speaker. Kupitia semina zake amesaidia watu wengi kuzishinda changamoto za maisha, lakini yeye ameshindwa kuzishinda.

Tunasahau kwamba watu wanaobeba matatizo ya jamii nao ni binadamu. Wanaweza kupitia magumu pia.

Daktari bingwa wa macho anaweza kuugua macho pia. Mwalimu anaweza kufanya mtihani wa somo analofundisha na akafeli. Mshauri wa mahusiano nae anaweza kupata changamoto za mahusiano. Afisa kilimo anaweza kulima na mazao yakafa. Daktari wa magonjwa ya akili anaweza kuugua afya ya akili.

Nje ya taaluma zao, vipawa vyao, ushawishi wao kwa jamii, bado ni binadamu.

Washauri nao wanahitaji kushauriwa. Madaktari nao wanahitaji kutibiwa. Walimu nao wanahitaji kufundishwa. Wauguzi nao wanahitaji kuuguzwa.

Wahubiri nao wanahitaji kuhubiriwa. Wote ni binadamu. Mahitaji yetu ya kihisia yanafanana.

Hakuna komandoo wa shida, aliimba Hamza Kalala. Sio kwa sababu nafanya kazi BOT basi siwezi kuishiwa.

Sio kwa sababu mimi ni daktatri, hivyo siwezi kuugua. Sio kwa sababu nafundisha basi siwezi kufeli.

Bado mimi ni binadamu. Nikikwama nisaidie.

FB_IMG_1684955534044.jpg



Source: Facebook Page ya Godlisten Malisa
 
Nlivoanza kufanya kazi hospitali ndo nligundua kumbe watu wanatembea na mashida kibao.

Hapo ndo nkatambua kua, tungechimba shimo alaf kila mtu atupe shida zake humo, kila mmoja wetu angekumbatia za kwake baada ya kuona wanayopitia wenzake.

Hii kazi ni rare kukutana na mtu mwenye hana matatizo. Kuamka mpaka kulala unaskiliza shida tu.

Sometimes wacha tujitungue tu na mitingo.

Personally i thnk n wakati muafaka kuwe na matherapist wa kutosha nchi hii ili watu waweze ku access hizo services kwa gharama nafuu. Afya ya akili ni jam!
 
Back
Top Bottom