Hakuna kilimo cha umwagiliaji,hakuna ajira,hakuna mvua za uhakika,unakamataje vijana wasio na kazi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Isitoshe hawana ardhi,hawana mitaji na wala hawakopesheki maana hata dhamana hawana na pia hata wazazi wao nao ni masikini kama wao.

Kama haitoshi,ukianza tu kabiashara chako TRA/Manispaa hao na kila aina ya tozo!Vyuo vyetu havina hata mafunzo ya ujasiriamali kwa wahitimu wake!Yaani hata hujaandaa sera rafiki kwa vijana hawa kujiari teyari umeanza kuwaandama!!

Sasa vijana hawa unawakamata kwa kipi hasa?Umejenga/umehamisisha ujenzi wa viwanda na wakakataa kufanya kazi?Umetoa mamilioni kwa kila kijiji wakakataa kuchukua mikopo hiyo?Kwenye jimbo ulilokuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 20, umetengengeneza fursa ngapi za ajira kwa vijano katika hilo jimbo?

Kama kweli una uchungu na vijana hawa,ni kwanini basi usisitishe ununuzi wa mashangingi na sitting allowance za wabunge na badala yake fedha hizo ukaagiza zitolewe kama mikopo kwa vijana au kwa kila kijiji?

Mh.,kuna maeneo unatakiwa uende taratibu na nyie mlio karibu yake mshaurini vizuri huyu mh.wetu.

Otherwise,as a nation,we are heading for trouble under this new regime!!
 
Isitoshe hawana ardhi,hawana mitaji na wala hawakopesheki maana hata dhamana hawana.

Kama haitoshi,ukianza tu kabiashara chako TRA/Manispaa hao na kila aina ya tozo!Vyuo vyetu havina hata mafunzo ya ujasiriamali kwa wahitimu wake!Yaani hata hujaandaa sera rafiki kwa vijana hawa kujiari teyari umeanza kuwaandama!!

Sasa vijana hawa unawakamata kwa kipi hasa?Umejenga/umehamisisha ujenzi wa viwanda na wakakataa kufanya kazi?Umetoa mamilioni kwa kila kijiji wakakataa kuchukua mikopo hiyo?Kwenye jimbo ulilokuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 20, umetengengeneza fursa ngapi za ajira kwa vijano katika hilo jimbo?

Kama kweli una uchungu na vijana hawa,ni kwanini basi usisitishe ununuzi wa mashangingi na sitting allowance za wabunge na badala yake fedha hizo ukaagiza zitolewe kama mikopo kwa vijana au kwa kila kijiji?

As a nation,we are heading for trouble under this new regime!!

Hivi unaweza kueleza ni kwanini wakina mama (tena wanaoishi kwenye mazingira hayo hayo wanayoishi vijana) hawaonekani wakicheza pool asubuhi?
 
Hivi unaweza kueleza ni kwanini wakina mama (tena wanaoishi kwenye mazingira hayo hayo wanayoishi vijana) hawaonekani wakicheza pool asubuhi?
Jiulize ni kwanini biashara hizi hawazifanyi huko vijinini na wanakimbilia mijini.Pia jiulize kama wana uhakika na biashara zao hizo huku mijini na zaidi jiulize mgambo wa jiji/miji huwa wanawafanyia nini na pia jiulize huyu mama ntilie ana sera gani iliyoandaliwa ambayo ni rafiki kwake inayompa uhakika wa biashara yake hiyo.
 
Ukikaa na kuandika mtandaoni muda mrefu na maneno mengi unaingiza sh ngapi? Sisi vijana siku hizi tu wavivu sana, tunasingizia kila kitu, hatutaki kufanya kazi, hatutaki kulima, maofisini ni kuchati na rushwa kwa kwenda mbele.

Umeajiriwa juzi leo unataka umiliki gari nyumba nzuri, huku maofisini ni Facebook, whatsapp, badoo na Instagram.

Kila kukicha tunalalamika hakuna fulsa, hakuna ajira, huku wageni wakizidi kujinyakulia maeneo na rasilimali zetu.

Wageni wanachukua maeneo wanalima wanatajilika sie tunalalamikia serikali, vijana tuamke tufanye kazi, tuache uvivu.

Tutengeneze hata vinyago tuuze tumekalili ni kazi ya wamakonde, kulima wasukuma.

Kijana wa Tanzania amka fanya kazi kwa maendeleo ya kwako, familia yako, jamii yako na Tanzania yako
 
Mh president katika siku ambazo sijamuelewa ni leo,nimewaza sana yale yalikua akilini mwake au kuna mtu kamshauri?vitu vya ajabu sana aisee,nimkumbushe tu kua yeye ni mkuu wa nchi na maelezo aliyoyatoa leo napata mashaka kama hayatomsumbua baadae.
 
Rais amesema haiwezekani kijana asubuhi anacheza pool wakati wazee na wakina mama "wapo shambani".. so kazi zipo huko mashambani shida uvivi tu.. tanzania tutakufa tukilalamika tu
 
Back
Top Bottom