Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,336
- 10,896
Habari wakuu!
Mtaniwia radhi kwa maneno makali na machungu nitakayoyatoa hapa. Lengo ni kuweka mambo sawa na kutufanya tujiandae mapema.
Hakuna jambo baya kama Baba kumtegemea Mtoto. Ni jambo la aibu tena aibu kubwa sana. Ni dalili ya laana na kuendekeza ujinga katika jamii. Ni fedheha kubwa sana Baba kumtegemea mtoto kiuchumi.
Baba bora ndiye huamua kwa kiasi kikubwa Future ya watoto wake. Hupigana kufa na kupona ili watoto wake watimize ndoto zao. Zamani kidogo Baba ndiye humsaidia mtoto wake wakiume kutafuta maisha kwa kumuongezea mtaji. Kama haitoshi Baba ndiye huhusika kwa asilimia mia moja katika ishu ya Kutoa Mahari kwa kijana wake. Hii ni kutokana na kuwa Kijana wake anaenda kuongeza ukoo wake.
Biblia inatuambia kuwa Mzazi mwema ni yule anayeacha urithi kwa watoto wake hata vizazi vitatu. Andiko hili linatoa chachu na ari kwa wanaume kufanya kazi kwa bidii kusudi wawapatie watoto na wajukuu wao urithi mwema. Pia maandiko hayo hayo matakatifu yanatuambia "Heri mtu asiyeamini kuliko yule ashindwaye kuhudumia watu wa kwao" Huyo ni paulo.
Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la Baba Jinga. Baba wenye kutoa sababu lukuki pindi linapokuja suala la majukumu yao. Wababa wengi wanakimbia majukumu yao. Kijana unayesoma sasa hivi ikiwa unamawazo ya kusaidiwa na watoto wako uzeeni ujue upo kwenye kundi la Baba Jinga. Hujui thamani ya jina "Baba".
Watu wengi hutegemea watoto wao. Huu ni ujinga na kuendekeza uvivu usiovumilika. Ujana wote unashindia pombe, unavaa nguo za gharama, unatembelea magari mazuri bila kuwekeza alafu uzeeni unaanza kusumbua watoto.
Wababa wa zamani licha ya kuwa hawakuenda shule lakini walijua kuwekeza kwenye kilimo, kwenye ufugaji na mambo mengine. Ndio maana ule msemo wa Jungu kuu halikosi ukoko ulikuwa ni halisi. Lakini kwa sasa Wababa wengi wanazembea sana. Unakuta mtu hafanyi kazi akiwa kijana mwenye nguvu anaanza kukurupuka akiwa na miaka 45+ huko. Hivi uliona wapi Watu wakipanda wakati wa mavuno. Uzee ni msimu wa kuvuna kile ulichokipanda.
Kama ulipanda zinaa basi utavuna maradhi kama ya mgongo, mfumo wa mkojo, magonjwa ya zinaa. Kama uliwekeza kwenye pombe basi jiandae kisukari, Shinikizo la damu. Hapa ndipo penye lawama hapa. Unakuta unaumwa halafu hauna hela ya matibabu. Ukicheki nyuma hukuwekeza. Kazi kulia lia kwa watoto. Amini amini nakuambia Hata utoe laana ya namna ipi haiwezi kufanikiwa na wewe mwenyewe utakuwa shahidi.
Hata Biblia haimtambui Mgane kama ni sehemu ya kupewa msaada. Mwenye haki ya kupewa ofa za uzeeni ni Mjane(Bibi). Babu(Mgane) Hatambuliki kwani ni Baba yaani anamuwakilisha Mungu. Sasa kama Mungu anapewa msaada sijui kwa kweli.
Vijana tunaoenda kuwa Baba tuwekeze jamani. Maisha ni mara moja. Umri unakimbia mbaya sana. Leo miaka 25 unasema muda upo unashangaa miaka 40 hii hapa ndio unashtuka. Usipende makubwa wakati wa kutafuta. Wenzako wananunua gari nawe umo. Wenzako wananunua Iphone sijui ngapi nawe umo. Wakati wewe ukifanya hayo ukifikiri ndio maisha wenzako wananunua hekari tatu kwa laki tisa. Baada ya miaka ishirini unashangaa wanamiliki si chini ya heka 50 unaona kama waliiba pesa kumbe ni akili. Wakati wa uzee wanaweza kuwarithisha watoto mashamba. Wewe unaanza kupiga mizinga watoto ujinga tuu.
Nabii Ibrahimu aliweza kutoa mahari kwa kijana wake Isack. Lakini leo ni Wababa wangapi wangiambiwa watoe hata ng'ombe kumi tuu kama mahari watakavyoanza kushikana mashati. Ujinga ni kutegemea watoto ilihali wewe ndiwe uliwaleta duniani.
Inatakiwa uwategemee watoto kwa kuendesha miradi yako uliyowaachia ili waweze kujikimu wa na familia zao. Huku wewe ukimsubiri Israeli mtoa roho kwa shauku kubwa. Hata Israel huwaogopaga wazee wa hivi. Kwani wamevipiga vita vizuri mwendo wameumaliza na mali wamezitunza. Sula la imani sitaliongelea kwa leo.
Vijana tupambane kwa kweli kupunguza Baba Jinga.
Nawasilisha.
Povu lolote linaruhusiwa nguo zipo nyingi za kufua