Hakuna haja ya Nyerere Day

“Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu” – Mwl. J.K Nyerere ,
 
Labda nikujibu kwa mfano ndo utaelewa kuna wachezaji zaidi ya 5000 lakini mchezaji bora huwa mmoja tu ambaye anasaidiwa na wachezaji zaidi ya mia mbili ili yeye awe bora kama hukunielewa kuwa muwazi
 
Nyerere naye alikuwa binadamu pamoja na mazuri yake kuna mapungufu ambayo alifanya lakini usiseme hakufanya kitu mkuu, fikiria mpya.
 
hana llte zaidi ya kutuachia nchi mbovu inayoitwa jamhuri ya muungano ni kiini macho tu!
 
Mkuu hoja hizi ni nzito sana....wasubiri wenyewe waje.
 
Labda kwa sababu ni mkristo....

CC FaizaFoxy
 
Kwako wewe huyo Mohammed Saidi ni nani hasa mpaka uamini alichoandika,

Nenda Maktaba kasome history ya Tanzania utaelewa umuhimu wa Nyerere, Kambona, Bibi Titi Mohammed na wengineo.

Tatizo unaongozwa na mihemko.
Kwani mtu usipokuwa na dini huwezi kumuomba Mungu wewe binafsi!!

Wimbo wa taifa ni sala ya pamoja kwa wenye dini,wapagani, Wakristo kwa waislamu.


Punguza Mihemko ndugu, Tanzania ni yetu site.
 
Mleta uzi unaujua msemo usemao nabii hakubaliki kwao?. Mwalimu alifanya mengi ambayo yanaifanya Tanzania ibakie kama ilivyo hivi sasa. Maono yake yaliondoa kabisa ukabila na ukanda. Kama tusingekuwa na mawazo na mitazamo yake, leo hii ni makabila machache sana ambayo yangekuwa yamestawi kiuchumi na mengi mengine yangekuwa ni makabila yenye kuwatumikia hao wachache.
Kiuchumi hakufanikiwa lakini ni marais wachache sana walioasisi nchi za Afrika ambao wanaweza kujisifu kwamba walifanikiwa kiuchumi.
Ni jukumu la hawa viongozi wa sasa kutumia rasilimali watu yenye elimu, kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi nzima na ule wa mwananchi mmoja mmoja.
 
Yaani wewe ukiisha msoma huyo Mohammed wako baaaaasi. ...Dunia yako inaishia kwa huyo bwana, na kwingineko hawajuhi lolote kuhusu Mwl. Nyerere?
Hawa ni wale vijana wa mwendokasi, akili za kufikiria mambo kwa undani, wamezipata katika miaka ya karibuni.
 
Well, nijuavyo jina sahihi ni Nyerere Death Day.

Sioni sababu ya kutosherehekea siku ya kifo cha Nyerere kama kilivyowekwa rasmi kitaifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…