Hakuna haja ya kuwa na Bunge la bajeti

Hakuna haja ya kuwa na Bunge la bajeti

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,981
Reaction score
51,150
Hakuna haja ya kuwa na vikao vya Bunge kujadili bajeti ya serikali kama mhimili wa utawala unaweza kutumia fedha zilizo nje ya bajeti bila ya kuomba kibali cha bunge wala kulitaarifu bunge.

Kama maamuzi ya vikao vya Bunge la bajeti hayaheshimiwi kuna haja gani ya kuwa na vikao hivyo? Huo ni ufujaji wa fedha za walipa kodi na walalahoi wavuja jasho wa nchi hii.
 
Hakuna haja ya kuwa na vikao vya Bunge kujadili bajeti ya serikali kama mhimili wa utawala unaweza kutumia fedha zilizo nje ya bajeti bila ya kuomba kibali cha bunge wala kulitaarifu bunge. Kama maamuzi ya vikao vya Bunge la bajeti hayaheshimiwi kuna haja gani ya kuwa na vikao hivyo?

Huo ni ufujaji wa fedha!!
Nimeshangazwa na mazungumzo ya kununua ndege nyingine mbili kubwa na kwamba pesa yake iko tayari!
Kila nikiyakumbuka ya Mv Dar es salaam napata hofu
 
Hakuna haja ya kuwa na vikao vya Bunge kujadili bajeti ya serikali kama mhimili wa utawala unaweza kutumia fedha zilizo nje ya bajeti bila ya kuomba kibali cha bunge wala kulitaarifu bunge. Kama maamuzi ya vikao vya Bunge la bajeti hayaheshimiwi kuna haja gani ya kuwa na vikao hivyo?

Huo ni ufujaji wa fedha!!
Naunga mkono hoja yako kwa asilimia 100.....

Ni heri tu TZ yetu ijulikane kuna mhimili 2 tu ya dola, yaani Executive na Judiciary.

Kwa kuwa tumemuona Bwana yule majuzi alipokwenda pale gereza la Ukonga, akimwambia Kamishna wa Magereza kuwa atamletea bilioni 10 za kujengea nyumba za askari......

Tulimshuhudia pia Bwana huyo mwezi June mwaka huu alipokwenda kusali kwa mzee wa Upako aka Mzee wa Bapa, naye akimuahidi kuwa atamjengea barabara ya lami toka Mandela Road hadi kanisani kwa huyo Mtumishi wa Mungu.

Tumemshuhudia pia Bwana huyo akiamua tu kujinunulia ndege za Bombardier kadri anayojisikia yeye mwenyewe!

Kwa hiyo hoja yako ni ya msingi kabisa kuwa hatuna sababu ya kuwa na Bunge ambalo kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu ndiyo mhimili unaopitisha Bajeti ya nchi ikiwa Bwana yule ndiye anajiona kuwa ndiye Waziri wa Fedha na wakati huo huo kuwa ndiye Financial Controller wa pesa zote za nchi yetu!
 
Bunge lenyewe limejaa vimeo halijitambui hata zaidi ya vikao vya bajeti sioni umuhimu wa bunge kuwepo...linatia hasara tu walipa kodi
 
Hakuna haja ya kuwa na vikao vya Bunge kujadili bajeti ya serikali kama mhimili wa utawala unaweza kutumia fedha zilizo nje ya bajeti bila ya kuomba kibali cha bunge wala kulitaarifu bunge. Kama maamuzi ya vikao vya Bunge la bajeti hayaheshimiwi kuna haja gani ya kuwa na vikao hivyo?

Huo ni ufujaji wa fedha!!
Hata barua inahitaji rubber stamp. Wacha wale posho kwa kutugongea mihuri miswada yetu.
 
Bunge lenyewe limejaa vimeo halijitambui hata zaidi ya vikao vya bajeti sioni umuhimu wa bunge kuwepo...linatia hasara tu walipa kodi
Bora tubakie na watawala ambao kwa vitendo wameonesha kwamba si lazima sana kufuata mipango ambayo serikali yenyewe wanaipeleka Bungeni. Wabunge wetu hata tu kuinua mdomo na kuuliza serikali kutumia hela ambazo hazijapitia bungeni si kulidharau bunge? Wanashindwa!
 
Mwisho wa sifa upo karibu sana, wanafinzi wamenyimwa mikopo ili ndege inunuliwe, kunatofauti gati na kauli ya Mramba enzi zake kuhusu ndege ya Rais.
Hata mimi nasikitika kwa hili la Wanafunzi
 
Bunge lenyewe limekubali kutiwa kwapani na mhimili wa utawala!!
Kati ya ujinga Bunge hili lililofanya ni kukubali kutoonyeshwa live. Sasa kama hatujui wanachojadili kuna haja gani ya kuomba budget approvals kwa bunge ambalo halionekani?
 
Back
Top Bottom