Hakuna haja ya kugombana na watangazaji wa mpira, badili kwa kiingereza utanishukuru

Hakuna haja ya kugombana na watangazaji wa mpira, badili kwa kiingereza utanishukuru

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,470
Nimeona kuna mjadala mkali unaendelea mitandaoni kuhusiana na baadhi ya mashabiki wa Simba kuamini kuwa Simba haipati matokeo mazuri pale mechi zake zinapotangazwa na mtangazaji wa Azam TV, Gharib Mzinga.

Binafsi, mimi siwakubali hawa watangazaji woote. Kwanza wote wana chembechembe za uto na wengine wanaonyesha mahaba yao wazi wazi. Kuna huyo anaitwa Kambole sijui, ukisikiliza utangazaji wake utadhani anatangaza kwenye Yanga TV. Anasahau anatakiwa awe "balanced".

Kuna yule alitangaza game ya kwanza ya Al Masry vs Simba. Aisee, alishindwa kabisa kuficha furaha yake pale Simba ilipokuwa inafungwa hadi inashtua. Imefika wakati uongozi wa Simba utilie maanani haya mambo na iwasiliane kiofisi na Azam kama ambavyo uto wanafanya.

Kuna yule/wale wanatutangazia kiarabu. Hivi mbona kuna watu nchi hii wanadhani mpira ni kwa ajili ya watu wa imani fulani? Juzi nilimsikia roporopo mmoja anamkataa mzabuni wa Simba JayRutty eti kwa sababu hakufunga mwezi wa Ramadhani? Kuna hii ya kupeleka misaada kwenye vituo vya dini moja. Mifano ipo mingi ya hii tabia. Tunafumba macho ila siyo kwamba hatuoni. Anyway, hii ni mada nyingine najua wengi mtaacha mada kuu mtajikita kwenye hili.

Binafsi mechi za kimataifa nacheki DSTV, nikiangalia Azam TV kama nipo home naweka kwa lugha ya kiingereza. Watangazaji wa kiingereza hawana mambo mengi. Zama za huyu anampasia huyu, anapeleka kwa yule ni enzi za radio, wao wamevuka nazo hadi kwenye vioo. Yaani kina Ateba wakukwaze na mtangazaji tena akukwaze? Hayo maisha mimi siyawezi.

Kwanza watangazaji wa kiingereza wanakupa analysis ya matukio, wachezaji, timu au mchezo kisomi bila kuwa na upendeleo na hawana maneno meengi.
 
Malipo hapa hapa duniani manara alimdhalilisha baraka MPENJA akimshutumu kuwa ni simba na wana yanga wakajaa kwenye mfumo kweli wakaanzisha vita naye nasikia mpaka kwenye derby walimkataa MPENJA hakuna laana mbaya kama ya ubaguzi.
 
Na hilo nilinotice Mpenja alikuwa hatangazi mechi za Yanga kabisa, sijui siku hizi. Itafika wakati na sisi tutawapa Azam kina Kisugu na GB64 watutangazie mechi zetu maana hawana tofauti na hawa watangazaji wao
 
wew ukitaka kuuelema mpira msikilize gharib mzinga
 
Hii inchi watu sijui ni stress za maisha au uwelewa mdogo, hao uliowataja Simba na Yanga kukataa watangazaji wote ni wajinga, mtangazaji anaathiri vipi mpira unaochezwa? Wachezaji wala hawamsikii na hata benchi la ufundi sasa ana mchango gani kwenye final results kama sio ujinga ni nini?

Mimi naangalia mpira ingawa ni mechi chache zikitangazwa na hao lakini sioni huo ushabiki wa waziwazi naona wanaripoti matukio ya uwanjani na hata likifungwa goli wanasherehesha sawa tu.

Pia na wewe una matatizo nilikuwa naona una uwelewa wa mambo kumbe unaanza kuwapa watu mashaka juu ya hilo, sasa lugha ni dini au? na kiswahili na kiingereza na lugha nyingine wanazotumia wanakuwa kwenye mlengo wa dini? Maana watangazaji wetu wa kiswahili huwa wanatumia vijimaneno vya kuchombeza vya lugha tofauti tofauti kulingana na ufahamu wao, wanaingiza kiingereza, kifaransa, kihispaniola, kiarabu n.k

Nimewahi cheki mechi za Mzinga anajitahidi kuanalyse matukio na profile za wachezaji na benchi la ufundi na timu kwa ujumla

Mpenja sioni shida ndiyo style yake ya kutangaza sio lazima aige wengine, hamna template imewekwa duniani kwamba wote mfuate hii ndiyo kanuni.
 
5imba mna tatizo vichwani 😂
Mtangazaji wa TV anatangaza tukio linaloonekana, kushinda na kufungwa yeye hausiki

wew ukitaka kuuelema mpira msikilize gharib mzinga

Hii inchi watu sijui ni stress za maisha au uwelewa mdogo, hao uliowataja Simba na Yanga kukataa watangazaji wote ni wajinga, mtangazaji anaathiri vipi mpira unaochezwa? Wachezaji wala hawamsikii na hata benchi la ufundi sasa ana mchango gani kwenye final results kama sio ujinga ni nini?
Nadhani hao mashabiki wanaongelea na kudhani ana gundu dhidi ya Simba. Huo ni mtazamo wao maana sijamfuatilia.

Pia kumbuka mtazamaji kumsikia mtangazaji ni sehemu ya burudani anayotaka aipate akiangalia mpira. Akiona anapata kero na kwamba mtangazaji ni kama anaisimanga timu yake ni sahihi kumkataa.
 
Nimewahi cheki mechi za Mzinga anajitahidi kuanalyse matukio na profile za wachezaji na benchi la ufundi na timu kwa ujujumla
Analysis ya Mzinga na hao waswahili wengine ni tofauti na ile inayofanywa na watangazaji wa kiingereza. Hapa siongelei kutoa data za huyu kocha amefundisha timu hii na timu hii. Sijui nilielezee vipi tofauti yao ila naijua vizuri na ndiyo inayonivutia huko.
 
5imba mna tatizo vichwani 😂
Mtangazaji wa TV anatangaza tukio linaloonekana, kushinda na kufungwa yeye hausiki
Sawa Simba tuna matatizo, lakini ujue kwenye kesi vyura mliyomshtaki Semaji la Kafu AMEWASHINDA! Na kule KAS mlikoenda tutawashinda pia!
 
Sawa Simba tuna matatizo, lakini ujue kwenye kesi vyura mliyomshtaki Semaji la Kafu AMEWASHINDA! Na kule KAS mlikoenda tutawashinda pia!
Mkishinda CAS zile mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 vinafutika
Kweli mbumbumbu ni mbumbumbu
 
Mkishinda CAS zile mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 vinafutika
Kweli mbumbumbu ni mbumbumbu
Kweli hazifutiki na ukweli kwamba Simba ni timu ya nne bora Afrika nzima kwa sasa hazifutiki!
 
Ukisikia shabiki anasema mimi Yanga damu au Simba damu ujue huyo ni FALA.

Shabiki anayejitambua hana muda wakuwashambulia Watangazaji wa mpira.
 
Back
Top Bottom