Hakuna Haja/Haraka ya kuwa na Mawaziri. Mheshimiwa Rais...

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,505
Asilimia 99 ya Wabunge ni wa CCM najua jinsi gani mheshimiwa Rais unapata changamoto kuchagua Mawaziri.

Mheshimiwa Rais wala usiwe na haraka. Chagua taratibu sana. Wapitie hawa wabunge mmoja baada ya mwingine. Then hata kama itachukua miaka 2 au 3 wala haina shida. Sisi hatuoni tatizo lolote

Na wakati mwingine hata hawa mawaziri ni mzigo tu. Kwa nini Makatibu Wakuu wasiendelee kuchapa kazi? Mawaziri mimi binafsi sioni hata umuhimu wao. Mpaka sasa wiki ya 3 hakuna mapungufu yoyote kiutendaji.

Na tunajua mawaziri hawa hawakuwa na lolote walifanyalo zaidi tu ya kutoa matamko, kutunisha matumbo na kutunisha mifuko yao.

Tuendelee kupiga kazi wewe endelea kuwapima na kuwachuja ikifika mwaka kesho teua wawili. Then endelea wachunguza wengine mpakan2022 hapo unaweza tena teua mmoja. Then 2023 mmoja, 2024 mmoja au wawili. Mwishowe 2025 unavunja baraza la mawaziri.
 
yesu anaumba mawaziri....
Hakuna haja ya mawaziri. Hawana tija yoyote, ni bora tubaki hivi hivi na Makatibu wakuu, Wakurugenzi wa Idara mbalinbali wizarani, Makamishna na wataalamu wengine. Mawaziri ni kuongeza gharama tu. Si waliomba ubunge?? wamepata. Sasa nini tena??
 
Mapungufu yapo Tanesco!.. Tangu uchaguzi uishe umeme unakatwa Kila siku wilaya hii ya Ilala- sijui maeneo mengine. Hakuna sababu yoyote inayotolewa kwa umeme kukosekana kwa masaa zaidi ya sita kila siku.

Waziri wa nishati hayupo na hivyo inaonekana watendaji wameamua kufanya hujuma waziwazi. Naamini hakuna aliyetangaza mgao wa umeme na mvua hizi.
 
Hii nchi mbumbumbu zimejaa kila kona!Unaelewa kuwa suala la mawaziri ni takwa la kikatiba na wala siyo takwa la utashi wa mtu?
 
Hakuna haja ya mawaziri. Hawana tija yoyote, ni bora tubaki hivi hivi na Makatibu wakuu, Wakurugenzi wa Idara mbalinbali wizarani, Makamishna na wataalamu wengine. Mawaziri ni kuongeza gharama tu. Si waliomba ubunge?? wamepata. Sasa nini tena??
Atakaekushangaa ni yule ambae hakumbuki mh. rais alishatamka kuwa katiba sio kipaumbele chake (tafsiri yake: katiba haina maana yoyote). Yale majukumu ambayo kikatiba yanatekelezwa na waziri yasubiri utashi tuu wa mtu mmoja?
 
Back
Top Bottom