Hakuna fao la kujitoa, Bunge limethibitisha

Hakuna fao la kujitoa, Bunge limethibitisha

Itakuwa zaidi ya uendawazimu kutumia fedha za Mashirika ya Pension kujenga viwanda. Wanaochukua uamzi huo baada ya miaka kumi tu watakuja kutamani kujifunga mawe shingoni na kujitosa baharini. Je, wameshapata majibu sasa kwanin sera/programu za Import Substitute, EPZ, Rural Industrialization etc zimefeli vibaya?

mkuu mbona ndio kinacho endelea
 
Dhuluma kubwa. Poleni sana mtakaoathirika na sheria kandamizi
 
Mungu aangilie kati,linatugusa wengi,tuajiriwe mpaka lini? Watupe haki yetu tukafanye yetu.55 Leo? Fikiria una 25-30,kweli mateso bila chuki.
 
hivi wabunge wakimaliza miaka mitano huwa wanapewa mafao yao?
 
Matatizo ya FAO LA KUJITOA yanaweza kutatuliwa kwa njia 2

A - Kuanzisha Online Petition, Watanzania/Wafanyakazi wanaohusika watasain na hii ni meseji kwa Serikali....Hii Sheria inaweza kubadilishwa...Sheria sio Biblia au Quran

B TUCTA kwenda Mahakamani au Kama TUCTA wamewekwa mfukoni, wafanyakazi wajikusanye, wachange, waajiri lawyer

Au Chama cha Siasa kijitolee wanasheria na wapeleke kesi mahamani...ACT WAZALENDO, CUF, TLP,CCM ASILI akina NAPE, etc
 
Kama ni kweli basi hiki ni kitanzi kingine kipya kwa wafanyakazi; at age of 55 to 60 eti ndiyo unipe pesa zangu Kha!!
 
Twaaafa, hili janga la taifa kwa sisi wafanyakaz ni dhuluma ya hali ya juu,
 
Kama Una Baba yako, Mama Yako, Bibi Babu, Dada Na Hata wewe Mwenyewe na Wanyonge Wote Serikali ya Awamu ya Tano Imekaribia kuleta Mkong'oto Huu Huu hapa (Kilio na kusaga Meno)

Kuna mswada unakuja na kwa Bunge letu la Wangapi wanakubali Waseme Ndiyooooo "Ndiyoooooo" waliosema ndiyo wameshinda "Utapita"

MSWADA HUO Unaenda kuua wastaafu Na sisi Tunao karibia kustafu

Ni hivi Mafao ya wastafuu yatakuwa hivi Tega sikio, utalazimika kulipwa 38% tu na 62% utakuwa unalipwa kila Mwezi (monthly) hapa ili unielewe nikupe mfano. kama ilikuwa ulipwe milioni 100 kama hela yako ya kustafia maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi.

Ukistafu na umri wa miaka 61 utakula hicho kiasi cha million 38 kigingine utalipwa kidogo kidogo kila mwezi

Ubaya wa hili siku ukifa tu kila kitu kimekufa malipo kila mwezi nayo yanakufa. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma wakati ungepewa yote ungewaachia miradi familia wakaishi hata kama haupo

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu. Yaani LPF, NSSF PPF sijui nani sijui nani itafungwa na kubaki mifuko miwili tu (Vibarua vinaenda kuota nyasi)

4. April 2018 sheria itaanza kutumika Yaani Mwakani Kuna kilio kikuu kwa watumishi wa mifugo na wastafuu

My Take

Kwa ufupi bila kupindisha muswada huu utaumiza watumishi wote ,Bunge Mkafanye kazi yenu, sasa Hiki ni kipimo chenu cha kudhibitisha Mpo huru na kwamba ni muhimili unajitegemea ,Wabunge wetu msipoliona hili kuwasemea watumishi basi Mtawasononesha watumishi

Yaani Ufanye kazi miaka 61 ukitumikia umma uzeeni uporwe haki itasikitisha

Alloyce Nyanda
Mtozi
 
Back
Top Bottom