Hakuna fao la kujitoa, Bunge limethibitisha

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Katika Bunge linaloendelea, Naibu Spika amethibisha kuwa Sheria iliyotungwa na Bunge inakataza FAO la Kujitoa

--TAMKO ZITO Fao la Kujitoa----Soma zaidi ....Tamko zito fao la kujitoa

TUCTA wanayo hii habari?

Wafanyakazi mnayo hii habari?

Watanzania tuendelee kulala

Wacha Pesa zijenge viwanda, baada ya miaka 10 vife

Hivi Watanzania wenzangu...Sababu zipi ziliua viwanda?

Je...Bidhaa za Tanzania zina ubora wa kutosha?

Mfano..Kuna Siagi (butter) Tanzania?
 
Haya ndio maisha bora kwa kila mtz..yaani fao la kujitoa tunanyimwa haki yetu as if hii sio hela yetu..kodi wameshindwa kuitumia ipasavyo wamehamia kwenye akiba ya mfanyakazi..so sad aisee
 
Kama hazina ubora ni wajibu wetu kuziongeza ubora, kama tunawapa wageni soko la kuuzia bidhaa zao kwanini tushindwe kujipa soko wenyewe? Hii laana ya kutukuza vya wageni na kudharau vyetu itatuisha lini?

Vitu vingapi vinatoka nje na havina huo ubora na bado tunanunua tena bei ya ghali.
 
Tatizo sikujitoa mimi nadhani tatizo ni kutokuwepo kwa pensheni kwa waliopoteza kazi mpaka wapate kazi nyingine
 
Kama hazina ubora ni wajibu wetu kuziongeza ubora, kama tunawapa wageni soko la kuuzia bidhaa zao kwanini tushindwe kujipa soko wenyewe? Hii laana ya kutukuza vya wageni na kudharau vyetu itatuisha lini?

Vitu vingapi vinatoka nje na havina huo ubora na bado tunanunua tena bei ya ghali.
Hakuna mtu anaetukuza vitu vya nje...watu wanaangalia ubora...
Hivi mfano ni watu wangapi wa level chini wakienda kwenye manunuzi wanaulizia ni cha nchi gani...hakuna..watu wanaangalia ubora ni jinsi wanunuzi wa nyuma wanavyoisemea hiyo bidhaaa
 
Kama hazina ubora ni wajibu wetu kuziongeza ubora, kama tunawapa wageni soko la kuuzia bidhaa zao kwanini tushindwe kujipa soko wenyewe? Hii laana ya kutukuza vya wageni na kudharau vyetu itatuisha lini?

Vitu vingapi vinatoka nje na havina huo ubora na bado tunanunua tena bei ya ghali.

Wewe na nani muongezee Ubora? Una maamuzi serikalini wewe

Kama Una kiwanda ongezea ubora

Unajua kwa nini viwanda vilikufa?.....

Je Mashirika ya UMMA NSSF na Magereza kujenga viwanda unaona ni faida, tupo kwenye Ujamaa?

After 10 hard years Viwanda hivi vitakufa tena....

TUCTA wamelala usingizi wa pono, pesa za wafanyakazi zinadhulumiwa

Serikali inatumia pesa za wanachama wa NSSF au PPF kwa ruhusa ya nani...Ubabe tu, Udikteta tu
 
Hatari aiseeh. Bora nisikatwe tu maana hakuna jipya, hela ni yako masharti kibao.
Wanasheria watusaidie hili ili uwepo mkataba kati ya mchangiaji na mfuko wa jamii anaoupendelea.
Eti bora usikatwe! Halafu bombadia tuzipate kwa pesa ipi? Na vipi hizo flyover na interchanges, zijengwe vipi? Au nafikiri kodi zinatosha kutoa huduma muhimu kwa jamii pamoja na kulipa deni la taifa (zaidi ya mil 50 - kila mtanzania na mil 1 yake)? SG railway ijengwe vipi wakati hata mikopo ya wahisani karibu itasitishwa kwa kupoteza sifa za kukopesheka?

Kwa huyu mkuu wa awamu hii ambaye ni 'omniscient mortal' (mwanadamu anayejua yote) na overambitious, lazima mafao yetu yatumike. Hebu fikiri ni pesa nyingi kiasi gani zinazokusanywa toka kwa michango ya wafanyakazi walio chini ya umri wa miaka 55!

Awamu hii ni janga la kitaifa (japo mkakati dhidi fao la kujitoa ulianza awamu iliyopita). Wanasheria na vyama vya wafanyakazi washauriwe kupinga huu udhalimu mahakamani. Hii itaisaidia awamu hii kuwaangalia wafanyakazi kwa jicho la tatu linaloangalia maslahi ya mtu binafsi. Haiingii akilini serikali kutumia mchango wangu, haki yangu, kama ipendavyo huku mimi katika umri wangu mdogo ninaamini mafao yangu yangeweza kuwa mtaji wa kuajiri watanzania wengine wengi wakaendelea kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii!

Wanasheria tusaidieni!
 
Halafu kuna mwehu anaipigia kura ccm.
Kwenye hii nchi wendawazimu ndio wengi kuliko wenye akili timamu.
Amini usiamini.
Na mtu yeyote anayejiunga na chama hicho akili zake hubadilika kabisa.
Nakupa mifano
Tazama matamko ya mawaziri
1. Hakuna kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa.

2.Hakuna binti kuolewa bila kua leaving ya form four (utadhani wanaolewa na serikali)

3. Kila mkoa uwe na viwanda 100, hilo ni agizo.

4.Tutawachukulia hatua kali za kinidhamu watumishi watakaoshindwa kuhudhuria mazoezi ya viungo.

5. Mtumishi anayeona mshahara haumtoshi aache kazi.

6. Sikuchaguliwa kuwaongeza watu mishahara
7. Fomu nilichukua mwenyewe.
Yaani kila mtu anakua kama yeye ndio kila kitu kwenye nchi ambayo ni yetu sote.

Majanga yanakuja kwa wapinzani ndio kituko zaidi, kwanza hawako serious kabisa, ni kama wanasafiri bila kujua wanaenda wapi wala hawajali, wanahisi wananchi hawana kumbukumbu wala hawaoni.

Kama kweli tungepat chama pinzani kizuri, nina hakika watanzania wasingeshindwa kupigana mpaka tone la mwisho ili kuiangusha hii kijani, lakini watu wakitazama kwa makini wanaona kila mtu ni mwana drama tu.

Haya mambo ili uweze kuyaona inatakiwa usiwe mwanachama wa chama chochote cha siasa kama mimi.
 
Itakuwa zaidi ya uendawazimu kutumia fedha za Mashirika ya Pension kujenga viwanda. Wanaochukua uamzi huo baada ya miaka kumi tu watakuja kutamani kujifunga mawe shingoni na kujitosa baharini. Je, wameshapata majibu sasa kwanin sera/programu za Import Substitute, EPZ, Rural Industrialization etc zimefeli vibaya?
 
Matatizo yote haya yameletwa na ccm kuwagandamiza wananchi wasio na hatia. Hapa wanatakà kukwiba hela zao. Ccm huwa ipo active kwenye kufisadi kuliko kuleta maendeleo ya watu
 
Kwenye hii nchi wendawazimu ndio wengi kuliko wenye akili timamu.
Amini usiamini.
Na mtu yeyote anayejiunga na chama hicho akili zake hubadilika kabisa.
Nakupa mifano
Tazama matamko ya mawaziri
1. Hakuna kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa.

2.Hakuna binti kuolewa bila kua leaving ya form four (utadhani wanaolewa na serikali)

3. Kila mkoa uwe na viwanda 100, hilo ni agizo.

4.Tutawachukulia hatua kali za kinidhamu watumishi watakaoshindwa kuhudhuria mazoezi ya viungo.

5. Mtumishi anayeona mshahara haumtoshi aache kazi.

6. Sikuchaguliwa kuwaongeza watu mishahara
7. Fomu nilichukua mwenyewe.
Yaani kila mtu anakua kama yeye ndio kila kitu kwenye nchi ambayo ni yetu sote.

Majanga yanakuja kwa wapinzani ndio kituko zaidi, kwanza hawako serious kabisa, ni kama wanasafiri bila kujua wanaenda wapi wala hawajali, wanahisi wananchi hawana kumbukumbu wala hawaoni.

Kama kweli tungepat chama pinzani kizuri, nina hakika watanzania wasingeshindwa kupigana mpaka tone la mwisho ili kuiangusha hii kijani, lakini watu wakitazama kwa makini wanaona kila mtu ni mwana drama tu.

Haya mambo ili uweze kuyaona inatakiwa usiwe mwanachama wa chama chochote cha siasa kama mimi.
Nmeipenda sn comment yako.
Nadhan itapendeza zaid tukiweka itikad za vyama Na kuangazia maslahi ya taifa
 
Hili suala linachanganya sana, maana kila huyo anasema kivyake. Mwanasheria mkuu alisema kuwa, muswada wa fao la kujitoa utafikiriwa kwa maana ya kuwasilishwa, na kama usingewasilishwa basi wabunge waamue nini kifanyike juu ya fao la kujitoa, soma hapa: Muswada wa Fao la kujitoa kusomwa bungeni na kauli hii ilitoka baada ya Abdala Mtolea mbunge wa Temeke kuhoji serikali kwa nini miswada mingine yenye marekebisho mepesi inawasilishwa halafu muswada wa fao la kujitoa, jambo ambalo ni zito hauwasilishwi. Nachokiona hapa ni sisi wahanga wenyewe kulala. Tunasubiri mpaka wansiasa watusemee hili, mwanasiasa hawezi kukusemea mtu kama haulalamiki. Tuamke, haiwezekani pesa ni zetu halafu kikundi fulani kiinazifanyia maamuzi, this is not acceptable in the eyes of the law.
 
Aisee! Itatubidi watanzania tuamke na kupaza sauti kwa umoja wetu, sisi wengine ni wahanga wa hiyo mifuko ya hifadhi ya jamii. Yaani kwa jinsi tunavyopata shida huku mitaani kama hatuna hazina zetu.. Huu uzalendo na utetezi wa wanyonge wanaohubiri sijauona kwakweli...hii ni dhulma iliyo ya wazi kabisa..PPF+serikali ya viwanda sintakuja kuwa sahau kwa hayo majanga niliyo nayo......ovaa
 
Back
Top Bottom