Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,828
- 831,054
Unazaliwa, unaambiwa ujivunie ukoo wako. Unafundishwa historia ya babu zako, ukoo uliotoka, na majina makubwa ya familia. Lakini kadri unavyokua, unaanza kuuliza swali gumu: Mbali na jina, kuna nini kingine?
Kwa familia nyingi, hakuna ardhi. Hakuna nyumba. Hakuna biashara. Hakuna akiba. Hakuna hata mwongozo wa maisha. Kile kilichobaki ni jina—jina lisilolipa karo, lisilonunua chakula, wala halizuii machozi.
Wazazi walipambana kivyao, maisha yakawapiga, na wakabaki na jambo moja la kupitisha kwa watoto wao: utambulisho wa ukoo. Lakini mtoto haishi kwa utambulisho pekee. Anaishi kwa fursa, malezi, elimu, na misingi.
Ndipo maumivu huanza. Unapokua mtu mzima, bado ukoo unakukumbuka—sio kukusaidia, bali kukudai. Michango. Sherehe. Mila. Majukumu. Lakini ukianguka? Kimya. Ukiomba msaada? Wanakumbusha jina lako, sio mchango wao.
Sentensi hii si lawama tu, ni kilio cha kizazi. Kilio cha vijana wanaoamua kuvunja mzunguko. Wanaosema:
“Kama hatukuachiwa mali, basi sisi tutakuwa mali kwa watoto wetu.” 🥲
Ni kizazi kinachochagua kujenga, hata kama kilianza na sifuri. Kujifunza, hata bila mwalimu. Kuweka misingi, hata bila mfano. Ili siku moja mtoto asiseme tena, “Hatuna cha kurithi zaidi ya jina la ukoo.”
Labda hatukubahatika kurithi mali. Lakini tuna nafasi ya kurithi maamuzi mapya. Na huo ndio urithi wa thamani kuliko wote.
✍🏽 .... Almasi Nillan