Maagano ya Ukoo Yalitoka Wapi

Maagano ya Ukoo Yalitoka Wapi

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
131
Reaction score
267
Maagano ya Ukoo Yalitoka Wapi

Chanzo cha maagano ya ukoo kwa kifupi

Katika biblia, Yohana 8:36 inasema, “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
Hebu tujiulize, ni kwa nini Bwana Yesu alipokuwa anakata roho pale msalabani, alisema neno moja tu. Alisema “imekwisha” (Yohana 19:30). Hakusema “yamekwisha”. Ukilifahamu hilo, utajua ndiyo sababu kwa nini, katika biblia, huwezi kuona maneno kama laana za ukoo, laana za kifamilia, laana za mababu, laana za mapepo, vifungo vya kikabila n.k. Ni kwa sababu, hayo yote yamejumuishwa katika hicho kitu kimoja kilichokwisha pale msalabani, nacho ni “dhambi”, yaani “dhambi ilikwisha”, yaani “kuwa huru kweli kweli”.

Dhambi ndiyo mzizi wa matatizo. Yaani, dhambi imefananishwa na ugonjwa wa ukimwi, ambao vijidudu vyake vinafanya kazi moja tu, nayo ni kwenda kushambulia kinga ya mwili, basi, havileti madhara mengine yoyote mwilini. Havisababishi kutokwa na vidonda. Havisababishi kutapika.

Havisababishi kuugua. Havisababishi kukohoa. Hapana. Lakini vinaua kinga ya mwili. Ile kinga ikishakufa, ina maana kuwa mwili hauna ulinzi tena. Hapo ndipo kila aina ya ugonjwa unapata nafasi ya kuingia mwilini. Mara malaria, mara kifua kikuu, mara mkanda wa jeshi, mara homa ya ini, n.k. Na hivyo ndivyo mwisho wa siku vinakwenda kummaliza mtu.

Dhambi nayo ndivyo inavyofanya kazi, Adamu na Hawa walipoasi pale Edeni, dhambi iliingia ndani yao (Mwanzo 3:6, 3:23). Dhambi hiyo ikaimaliza kinga yao yote ya ulinzi Mungu aliokuwa amewawekea pale Edeni. Ghafla mambo mabaya yote yakaingia. Uuaji ukaingia, dhuluma ikaingia, magonjwa yakaanza, uchawi ukaanza. Laana zikaingia. Vita vikaingia. Matabaka yakaingia. Na matambiko yakajitokeza.

Ndipo maagano yote ya ukoo yakatokea huko huko n.k. Na hili likawa ni tatizo lisilokuwa na tiba kwa vizazi na vizazi, kwa karne na karne. Ni kwa sababu kinga ya ulinzi wa Mungu, haikuwepo tena
. Dawa ya dhambi haikupatikana kwa zaidi ya maelfu ya miaka, kama vile dawa ya ukimwi ilivyochukuwa muda mrefu kupatikana.

Dhambi ya asili iliondolewaje
Bwana Yesu alipokuja miaka takriban 2000 iliyopita, hakuja kushughulika na katawi kamoja cha dhambi, labda tuseme maagano ya ukoo, au laana za kifamilia, au uchawi. Hapana. Angefanya hivyo, tatizo lote lisingeondoka.

Bwana Yesu alikuja kuung’oa mzizi wote wa dhambi, kiasi kwamba mtu aking’olewa mzizi huo ndani yake, basi hakuna vimelea vyo vyote vya laana yo yote ile itakayomwandama. Alifanya hivyo kwa kufa msalabani kwa ajili yetu. Na akasema, “imekwisha”.

Dhambi zilizotendwa baada ya kifo cha Yesu Zinaondolewaje

Baada ya Bwana Yesu Kristo kufa msalabani, binadamu wameendelea kuasi na kutenda dhambi mbalimbali. Hiyo ni pamoja na kufanya maagano ya ukoo
. Jambo ambalo baadhi ya watu hawafahamu, ni kuwa, kwenda kuombewa au kufanyiwa maombi fulani ya muda mrefu labda tuseme ya kufunga, na kukaa milimani na kutumia masaa mengi kuomba na kukemea, ndiyo kunaondoa laana na maagano ya ukoo au maagano ya kifamilia.

Wengine wanadhani kutoa sadaka fulani maalum ndiyo kunaondoa maagano ya kiukoo. Hapana. Mtu anaweza akafanya hivyo na bado hayo mambo yasiondoke ndani yake, kama ikiwa bado yupo nje ya wokovu.

Kama mtu hajakusudia kweli kuokoka, mambo hayo hayawezi kuondoka, yataendelea kumfuata tu. Ni lazima kuokoka. Ukisema mimi na dhambi basi, nimeamua kujitwika msalaba wangu na kumfuata Yesu popote atakapotaka mimi niende, sirudi nyuma tena. Ukatubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote.

Kisha ukatii agizo la ubatizo kwa jina la Yesu Kristo, sawasawa na Matendo 2:38, ili upate ondoleo la dhambi zako. Na kuanzia wakati huo, ukawa unaishi maisha ya mkristo aliyeokoka, siyo tu maagano ya ukoo yatafutwa juu yako, bali pia hata na yale maagano mengine usiyoyajua ya kipepo yaliyokuwa juu yako, yote hayo yatafutwa.

Hakuna haja ya kuhangaika kwenda kuombewa huku na kule. Ukifika kule kila mmoja atakuambia hiki, mwingine kile. Kumbuka kuwa wokovu ni muujiza mkubwa, ambao unatokana na neema ya Kristo tunaoupata bure bila kujisumbua, wala kugharamia chochote, Wewe ni kutii tu. Pale ulipotubu tu, fahamu kuwa vyote vimefutika. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuvunja maagano ya ukoo.

Biblia inasema ulipo moyo wa mtu ndipo ilipo hazina yake (Mathayo 6:21, Luka 12:34). Kama huna madhabahu maalum unajichelewesha bure, ni lazima ujue madhabahu yako ni ipi na ukishaijua utatenda sawasawa na madhabahu hiyo. Unaweza ukawa umeokoka lakini umeshikiliwa na magonjwa sababu ya madhabahu iliyokushikilia.

Kama maisha yako ya wokovu yapo mbali na Kristo, halafu unatafuta njia mbadala ya kuondoa tatizo hilo, kumbuka hayo mambo yalishafwa na mababu zamani, na yakashindikana. Hivyo, na wewe pia usijaribu kuyarudia hayo hayo, bali mkaribishe Yesu maishani mwako, awezaye kuondoa mzizi wote wa dhambi na laana zake zote. Na kukufanya kuwa kiumbe kipya. Na hakika atayavunja maagano yote ya ukoo, babu zako, na mababu zako waliyoingia na kuapa iwe ni katika afya, au mafanikio, au furaha, vyote vile, vitakwisha ndani yako.
 
Kwanza...
TUkiwa tumeikaribisha sabato. Ni vyema kuwekana sana kwenye mambo madogo madogo ambayo watu hawajapata kuyaelewa

Dhambi ni nini?

Msalabani Y3su alifuta madeni yetu. Katika lugha ya nyingine wanaita dhambi lakini katika uhalali wake wanaita deni

Mambo mengi ambayo bimadamu anafanya yanakuwa kwa mkono wa yule mwovu. Hivyo katika mikono ya mwovu unaandikiwa madeni. Hilo deni linatafsiriwa kama dhambi

YEsu kifo na ufufuko wake ni kutufutia madeni yetu yote ambaye yule mwovu ametuandikia.
Ukimpa nafasi mwovu basi anakuelemea kwenye mifupa yako
Soma Zaburi...6:2, 32:10, 34:20, 35:10...nk

NDio maana sala aliyosema Yesu ya Lord Prayer...anasema tusamehe madeni yetu, hakusema tusamehe dhambi zetu. Hili neno lina maana kubwa sana

Biblia inatafsiriwa kila siku kwa hiyo ukitafsiri neno sivyo kuna mambo mengi hutaweza kuyajua
 
Pili

NIni maana ya maagano?

MAagano unaweza ukawa hujayafanya wewe ila ukayabeba kiimani.
Mfano tumeona watu wengi kipindi hiki wakitumia vitu kama mafuta ya mwamposa.
Yesu ametusasa tuishi katika ROHO (spiritual). Ingawa tuko katika mwili asili yetu sio ya kimwili. Mwili ni nyumba na ndani yako kuna Roho ambayo ni ya Mungu.
Tumeyapa maisha ya kimwili nguvu, kuliko ya kiroho ndio maana unakuta mtu anahangaika na mambo ya mwili mda wot3 anazungumzia sex ukimuliza imekusaidia nini? Hamna kwa sababu anatimiza haja za kimwili...hapa nitakuja kuandika zaidi

Ila ukitumia mafuta ya mwamposa kwa imani yanakuponya basi unabeba imani ya mwamposa. Unasahau kuwa uponyaji unatoka kwa Bwana, na sio katika vitu ambavyo sio.

Maagano ya mwamposa unayabeba wewe katika kutumia vitu na kuvipa imani. ...hapa ndio unaona imani za kurithi
 
Tatu

Yesu alihubiri nini?
Hapa sikiliza kwa makin

Yesu alihubiri kuwa kuna maisha baada ya kifo.

Je maisha haya utayapata baada ya kifo?
Ndio na hapana. Ukifa kisha ukafa hutaishi.
Ila unatakiwa uishi ili hata ukifa kimwili bado utaemdelea kuishi kiroho.

Maana yake nini?
Anza kutafuta uhai ukiwa katika mwili hata pale mwili utakapokufa basi utaendelea kuwa hai.

.......

La kuongezea. Kumekuwa na contradiction au ukinzani mwingi kwenye baadhi ya vipengele kwenye Biblia ni kwa sababu baadhi ya vitabu ni vya mpinga Kristu

mfano. Paulo na barua zake zote kuweni makini kuzisoma kwa sababu ukweli wake umetengenezwa kibindamu..

Yesu aliitwa Nazare maana yake ni Kweli. SOMA Yohana 14.6..."Yesu akawaambia Mimi ndimi njia ya kweli na uzima, mtu haji kwa baba ila kwa mimi"

HIli neno lina maana kubwa sana.
Ni kwamba hutamwona Mungu pasipo huyu Yesu. Alikuwepo toka enzi na enzi hata pale alipokuja kwa Musa akamwambia "Mimi Niko ambaye Niko"

Kwa wakati wote huu amekuwa ndio njia ya kumwoma Mungu. Hakuna yeyote ambaye atamwona Mungu isipokuwa kupitia Yesu...Soma Mathayo 11:27

Sisi sote tunatakiwa kufanana na Yesu. Hapa tukifanana nae tutakuwa kaka na kaka. Kifupi Christo ni jina tu ila sisi sote ni Kristo ndio unaona watu wanajiita wakristo, sio kwamba wanatoka kwa kristo hapana ila tumepata kufanana na kuwa Kristo. Mfan mimi ni Gily Christo....Yohana 8:42

Kifupi. Ukiwa Gily Christo ndio namna pekee utakuwa na uwezo wa kumuona Mungu. Lakini nikibaki kuwa Gily Gru sitamuona Mungu at all

Nanukuu ....." Baba yangu ni baba yenu ingawa baba zenu sio baba yangu...
Ila katika Bible unaweza soma mfanano huu kupitia...Yohana 20:17
 
MWisho

Mpinga Kristu amekuwa anafanya kazi kubwa sana miaka na miaka kupotosha ukweli.

Ukweli nasema....

Ndio maana Yesu alikataa kutoa jina lake kwa Musa. Akamwambia :I am who I am...

LEo hii unakuta majina hata kwenye Biblia yanatafsiriwa. Jina la mtu halibadiliki kamwe

Yani wewe John ukienda popote duniani utabaki kuwa John. Hii ni moja ya mbinu ambayo anatumia kuharibu

Mungu hana aka wala jina lake halibadilishwi badilishwii.

Cha kuongezea hayo majina adonoy na mengi ambayo walokole wanayaita maana yake ni Bwana kiswahili. Sio majina ya Mungu ingawa wakristu wa sasa wanapiga kelele jehova hivi jehova vile.

Jina la Bwana ni lipi?
Jina la Bwana ni takatifu sana sana sana ndio maana hata wayahudi hawakulitaja hovyo hovyo.
It was too sacred to pronounce hivyo sitalitaja ingawa mnaweza ku google ukauliza wayahudi walimwitaje Bwana

Mimi naendelea kutumia Bwana. Au Holy One na Mungu nitamwita Holy of Holies. .

Sijui niseme nini cha ziada hapa kuongezea....wapendwa wangu katika Bwana, mimi nawapenda sana na nimependa kuwafundisha kidogo Ukweli. Ukweli unaishi nawe yule mwenye kuelewa anatelewa. Roho ws Bwana awaongoze. .
 
Back
Top Bottom