Hahahaha we mpuuz kweli..chademo ni taasisi ya wapi ,usiipake mafuta namna hiyo .Saccos ya kikundi fulani unaiita taasisi. Khaaa...na ukomeWaku,amani ya Bwana iwe pamoja nanyi.
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema ni taasisi imara ambayo imejijengea uwezo, himaya ya kitaasisi tangu pale mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini mwaka 1992 hadi sasa.
Chadema kama taasisi haimtegemei mtu/kiongozi mmoja ama kundi la watu wachache wenye maslahi yao binafsi ndani ya chama ili iendelee kuwepo, bali hutegemea nguvu ya UMMA na wanachama kwa ujumla wao, na hapa ndipo nguvu ya taasisi inapoonekana, hakuna wakuliteteresha/liyumbisha Chadema kwa kuondoka mwenyewe ama kufukuzwa na chama.
Kwa nyakati tofauti tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992, Chadema imepata kuwa na viongozi wengi na wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya chama, Chadema imepata kuwa na viongozi ndani ya chama wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuweza kushawishi Jamii juu ya agenda za chama/taasisi na hatimae kueleweka vyema kwa UMMA.
Pamoja na hao viongozi kuwa na ushawishi ndani na nje ya chama, kuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja; lakini bado hawakuwa juu ya chama ama wakubwa kuliko chama/taasisi. Walipokwenda kinyume na taratibu za chama aidha walifukuzwa ama walijiondoa wenyewe na chama /taasisi ikaendelea kuwepo na pengine kuimarika zaidi. Mfano mzuri ni akina M1&Co, walipotimuliwa baada ya kwenda kinyume na maadili na taratibu za chama bado Chadema haikutetereka bali iliimarika mara dufu. Kuelekea uchaguzi mkuu 2015 aliondoka Dr.Slaa Chadema haikupasuka kama miccm ilivyo tarajia na hatimae Chadema kwa chini ya UKAWA ilipata takriban 6m kwa nafasi ya Urais na idadi kubwa ya wabunge na madiwani hali iliyopelekea Chadema /UKAWA kuongoza baadhi ya halmashauri nchini ikiwemo Dar es salaam.
Hili swala la Lowasa kwenda tofauti na mtazamo/ misimamo ya chama /taasisi haikubaliki, aitwe mbele ya kamati kuu ajieleze ni agenda zipi alienda nazo ikulu na kwani nini afanye jambo hilo kuwa siri? Kwa nini hakushirikiana na viongozi wa Chadema ili wawe na agenda ya pamoja? Apewe nafasi ya kusikilizwa asipotoa maelezo yanayo jitosheleza, milango iwe wazi kwake iwe ni kwa hiari yake ama kwa nguvu ya UMMA ili kulinda maslahi cha chama/taasisi na chama bado itabaki salama.
Kusifia serikali pale inapofanya jambo jema kwa wananchi wake siyo vibaya, ila kwa hali ilivyo hivi sasa kila raia amekata tamaa mtaani hali ni mbaya changamoto lukuki, maisha kwa ujumla ni magumu mno...! Usalama wetu upo mashakani, huduma za Jamii hairidhishi, ajira, mikopo elimu ya juu balaa tupu, uhuru wa vyombo vya habari, kujieleza, bunge kabatini, unapataje ujasiri wa kupongeza serikali kwa hali hiyo?. Unless otherwise atueleze alienda ikulu kwa maslahi yake binafsi na yale yote aliyoyaongea ni maoni yake binafsi.
Mungu ibariki Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Africa kwa ujumla.
Thubhuthuuu...weeeee watazitapika walizozilambaKama ni taasisi na wanataratibu zao wajaribu tuone kumfukuza mamvi!!
Ni kweli kabisaa..hii naaminiCHADEMA inamtegemea TL.
Ndio Chadema ni taasisi na wana kanuni /taratibu zao, anaye kwenda tofauti lazima aadhibiwe kulingana na taratibu na kanuni hizo, nimesema apewe nafasi ya kusikilizwa na kamati kuu, amini usiamini ikionekana anastahili kufukuzwa ndani ya chama na hatimae kufukuzwa, Chadema bado itabaki salama, hakuna mkubwa kuliko Chadema.Kama ni taasisi na wanataratibu zao wajaribu tuone kumfukuza mamvi!!
Nakuhakikishia mkuu, Chadema ni kubwa kuliko mtu, rejea kuondoka kwao M1 &Co na Dr.Slaa, chama ilizidi kuimarika zaidi.Mkubwa kuliko chama yupo acha kujidanganya na hizo nadharia zako.
Ni kweli aliye enda ikulu ni Lowasa, lakini kumbuka anatoka ndani ya taasisi /chama na chama ina mitazamo, agenda na misimamo yake juu ya serikali ya Magufuli, kwa kuwa Lowasa anatokea ndani ya taasisi/ chama, kinachoonekana kwa miccm ni kuwa Chadema inaunga mkono yanayo tendwa na serikali ya Magufuli. Ikiwa Lowasa alienda ikulu kwa maslahi na agenda zake binafsi hilo halina shida, aliyoyaongea ichukuliwe kama ni maoni yake binafsi.Umeshasema chadema ni taasisi na aliyeenda ikulu siyo CHADEMA, ni Edward Lowassa ambaye ni mtu siyo taasisi.
Mbona mnamuinganisha Liwassa na Chadema?! Lowasa na chadema ni tofauti.
Hata ikatokea siku Tundu Lissu akaondoka Chadema, hutoamini Chadema itaendelea kuwepo.CHADEMA inamtegemea TL.
Ukomo wako wa kufikiri unaishia hapo...! Chadema ni chama/taasisi kubwa na imara ndio maana kila wakati nyie miccm na viongozi wenu hampati usingizi kwa kulihofia, mnatumia nguvu nyingi na rasilimali nyingi kupambana na Chadema lakini bado hamfanikiwi. Taasisi zikiwa huru chaguzi zote nchini ccm hata kitongoji hamtaongoza, mtabaki historia kama chama cha Kanu nchini Kenya.Hahahaha we mpuuz kweli..chademo ni taasisi ya wapi ,usiipake mafuta namna hiyo .Saccos ya kikundi fulani unaiita taasisi. Khaaa...na ukome
Huo ni mtazamo wako, kama una uthibitisho/ ushaidi juu ya hayo uyasemayo mimi siyajui.Thubhuthuuu...weeeee watazitapika walizozilamba
Chadema Inamtegemeaje huyo TL?! Watu hamuelewi nini, TL na wabunge wote pia viongozi wote wa chadema huitegemea chadema, sio kinyume chake?! Wasingepata fulsa walizo nazo bila chadema hivyo ni wao huitegemea chadema na sio kinyume chake. Hata wanavyoongea ni kwasababu ya kinga ya ubunge bila hivyo wangekuwa jela siku nyingi.CHADEMA inamtegemea TL.
Wewe bila TL hamna hoja ya maana na chama ndiyo kinakufa na tena mshukuru TL alivyoshambuliwa maana hamna kitu kingine mtakacho ongea zaidi ya kutumia propaganda ya kushambuliwa TL. Na kwasababu kama hiyo mnaeneza propaganda eti Tanzania kuna uvunjaji wa haki za binaadam hili tukio mlilipanga vizuri sasa sijui akipona mtakua mnaongea nini.Chadema Inamtegemeaje huyo TL?! Watu hamuelewi nini, TL na wabunge wote pia viongozi wote wa chadema huitegemea chadema, sio kinyume chake?! Wasingepata fulsa walizo nazo bila chadema hivyo ni wao huitegemea chadema na sio kinyume chake. Hata wanavyoongea ni kwasababu ya kinga ya ubunge bila hivyo wangekuwa jela siku nyingi.
Hahaha kwani chadema ilianzishwa na kusajiliwa baada ya TL kushambuliwa?! Mbona ni huyo TL ndiye aliyejiunga na chadema na siyo chadema iliyoomba kujiunga na TL.Wewe bila TL hamna hoja ya maana na chama ndiyo kinakufa na tena mshukuru TL alivyoshambuliwa maana hamna kitu kingine mtakacho ongea zaidi ya kutumia propaganda ya kushambuliwa TL. Na kwasababu kama hiyo mnaeneza propaganda eti Tanzania kuna uvunjaji wa haki za binaadam hili tukio mlilipanga vizuri sasa sijui akipona mtakua mnaongea nini.