Hakuna binadamu yeyote aliye mkubwa kuliko CHADEMA

Hakuna binadamu yeyote aliye mkubwa kuliko CHADEMA

Nimeona niliweke hili ili kuondoa sintofahamu inayozunguka nchini Tanzania kwa sasa .

Hakuna haja yoyote ya mtu yeyote kupanic kwa sababu yeyote ile .

Chadema ni kama Jeshi , Hakuna kamanda yeyote ambaye ni mkubwa kuliko Jeshi lenyewe , Si Mbowe wala Mashinji ama labda Erythrocyte ambaye aweza kuushinda ukubwa wa Chadema .

Bila kujali yanayoendelea , na naomba niweke wazi kwamba hapa sijadili malumbano yanayojadiliwa na wengine , naweka angalizo kwamba CHADEMA ambayo inaongoza kata yangu kule Kyela na imefika mpaka kijijini kwetu Kajunjumele ni kubwa sana kuliko individuals .
You have just pressed the Panick button!!
 
Nimeona niliweke hili ili kuondoa sintofahamu inayozunguka nchini Tanzania kwa sasa.

Hakuna haja yoyote ya mtu yeyote kupanic kwa sababu yeyote ile .

CHADEMA ni kama Jeshi, hakuna kamanda yeyote ambaye ni mkubwa kuliko Jeshi lenyewe, si Mbowe wala Mashinji ama labda Erythrocyte ambaye aweza kuushinda ukubwa wa CHADEMA.

Bila kujali yanayoendelea, na naomba niweke wazi kwamba hapa sijadili malumbano yanayojadiliwa na wengine, naweka angalizo kwamba CHADEMA ambayo inaongoza kata yangu kule Kyela na imefika mpaka kijijini kwetu Kajunjumele ni kubwa sana kuliko individuals.
Well said mkuu, Chadema ya Makani na Mtei ni imani. Hata Mbowe akitaka asepe tu, Lissu, Lema na wengineo. wameondoka Kaborou, Zitoo, Arfi, Silaa, Kitila, Mgamba na wengineo bado tunasonga mbele
 
Ni wajibu wake si analipwa.mnalazimisha kumsifia mtu anatimiza wajibu wake!au iyo kaz anapiga ni wajibu wa nani kupiga?
Kuna mtu kakushikia bastola kwenye bichwa lako umsifie??
Tatizo lililopo ni nyie, akitokea mtu akamsifia kwa utashi wake eti mnafura kwa nini anamsifia?? Mbona kina lissu wanaponda nao??
Acheni JPM awatoe ashki majnun kama imezidi.
 
Wanaopaniki nafikiri ni maccm wenyewe...

Au wachanga kabisa wa SIASA.
 
Nimeona niliweke hili ili kuondoa sintofahamu inayozunguka nchini Tanzania kwa sasa.

Hakuna haja yoyote ya mtu yeyote kupanic kwa sababu yeyote ile .

CHADEMA ni kama Jeshi, hakuna kamanda yeyote ambaye ni mkubwa kuliko Jeshi lenyewe, si Mbowe wala Mashinji ama labda Erythrocyte ambaye aweza kuushinda ukubwa wa CHADEMA.

Bila kujali yanayoendelea, na naomba niweke wazi kwamba hapa sijadili malumbano yanayojadiliwa na wengine, naweka angalizo kwamba CHADEMA ambayo inaongoza kata yangu kule Kyela na imefika mpaka kijijini kwetu Kajunjumele ni kubwa sana kuliko individuals.
Huko kusambaa mpaka huko uliko na kwingine ni sawa kabisa Lakini hii ukubwa una mwenyewe kwa sasa. Zamani ukubwa ulikua wa wenywewe sasa ni mwenyewe tu.
 
Kuna mtu kakushikia bastola kwenye bichwa lako umsifie??
Tatizo lililopo ni nyie, akitokea mtu akamsifia kwa utashi wake eti mnafura kwa nini anamsifia?? Mbona kina lissu wanaponda nao??
Acheni JPM awatoe ashki majnun kama imezidi.
Hujajibu swali we kilaza.Narudia swali langu,"anapiga kazi" iyo kazi kama siyo yeye wa kuipiga ni jukumu la nani kuipiga iyo kazi?
 
Huo ndio ukweli wenyewe aliondoka Dr Warid, Dr Slaa, Arfi, Zitto na genge lake lote la PM7 na Chadema iko imara kabisa.

Chadema ni taasisi isiyo na wanachama waamini watu, iko na wanachama waamini itikadi, Falsafa na sera zake.

Kusubiri Chadema ianguke kisa tu kiongozi fulani atatoka ni sawa kusubiri Bombardier bandarini.

Nyie mnaojifariji kuwa kutetereka kwa Chadema kama taasisi mtachoma sana mahindi kwa mwanga wa Mbalamwezi

Kama Uimara wa Chadema hautegemie Mtu Mbowe asingenyofoa kipengele cha Uenyekiti Chadema kwa kigezo cha kutaka kuimarisha Chama
 
Wamiliki wa Chadema wanajulikana.....hao wanaweza kuamua nani awe mgombea urais nk nk...hata kama siyo mwanachama...
 
Nimeona niliweke hili ili kuondoa sintofahamu inayozunguka nchini Tanzania kwa sasa.

Hakuna haja yoyote ya mtu yeyote kupanic kwa sababu yeyote ile .

CHADEMA ni kama Jeshi, hakuna kamanda yeyote ambaye ni mkubwa kuliko Jeshi lenyewe, si Mbowe wala Mashinji ama labda Erythrocyte ambaye aweza kuushinda ukubwa wa CHADEMA.

Bila kujali yanayoendelea, na naomba niweke wazi kwamba hapa sijadili malumbano yanayojadiliwa na wengine, naweka angalizo kwamba CHADEMA ambayo inaongoza kata yangu kule Kyela na imefika mpaka kijijini kwetu Kajunjumele ni kubwa sana kuliko individuals.
MAKARAI mmepaniki, kumbe hampendi watu wanaotofautiana itikadi watembeleane,wewe ni Mtanzania wa wapi? au unaweza kuwa mkimbizi toka Malawi unatusumbua akili zeu hapa mana najua kwa Mtanzania halisi anapenda kuona watu wakishirikiana,wakisalimiana,wakisaidiana,wakishauriana lakini kwa hili la Lowassa kwenda Ikulu imekuwa ni hoja isiyo na kikomo,why.....why......???????
 
Huko kwenu ccm , inaitwa CCM ya Magufuli , ushindi Alipata 100% ! Eti hakuna hata kura 1 iliyoharibika huku zaidi ya wajumbe 100 hawakujua kusoma wala kuandika .

Huyu Mbowe unaye mmilikisha chadema hajawahi kushinda uenyekiti kwa 100% na wala hajawahi kuita chama CHADEMA YA MBOWE .
Kwani ulikuwa ni uchaguzi wa CCM au ulikuwa ni mtihani kwamba hadi Mjumbe ajue kusoma na kuandika? Mbowe atashinda vipi uchaguzi wakati haufanyiki?
 
Chadema itaendelea kuwepo wanaodhani chadema ni MTU mmoja ni wavivu wa kufikiri
 
Chadema kyela nawaona sana mishirikiana kwenye misiba na kwenye sherehe ipinda chadema imepamba moto
 
Chadema kyela nawaona sana mishirikiana kwenye misiba na kwenye sherehe ipinda chadema imepamba moto
Usalama pekee wa ccm Kyela ni kufuta mfumo wa vyama vingi tu , vinginevyo wajiandae kukunja mikeka
 
MAKARAI mmepaniki, kumbe hampendi watu wanaotofautiana itikadi watembeleane,wewe ni Mtanzania wa wapi? au unaweza kuwa mkimbizi toka Malawi unatusumbua akili zeu hapa mana najua kwa Mtanzania halisi anapenda kuona watu wakishirikiana,wakisalimiana,wakisaidiana,wakishauriana lakini kwa hili la Lowassa kwenda Ikulu imekuwa ni hoja isiyo na kikomo,why.....why......???????
Umeelewa topic ?
 
Wakuu amani ya Bwana iwe pamoja nanyi.

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ni taasisi imara ambayo imejijengea uwezo, himaya ya kitaasisi tangu pale mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini mwaka 1992 hadi sasa.

CHADEMA kama taasisi haimtegemei mtu/kiongozi mmoja ama kundi la watu wachache wenye maslahi yao binafsi ndani ya chama ili iendelee kuwepo, bali hutegemea nguvu ya UMMA na wanachama kwa ujumla wao, na hapa ndipo nguvu ya taasisi inapoonekana, hakuna wakuliteteresha/liyumbisha CHADEMA kwa kuondoka mwenyewe ama kufukuzwa na chama.

Kwa nyakati tofauti tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992, CHADEMA imepata kuwa na viongozi wengi na wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya chama, CHADEMA imepata kuwa na viongozi ndani ya chama wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuweza kushawishi Jamii juu ya agenda za chama/taasisi na hatimae kueleweka vyema kwa UMMA.

Pamoja na hao viongozi kuwa na ushawishi ndani na nje ya chama, kuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja; lakini bado hawakuwa juu ya chama ama wakubwa kuliko chama/taasisi. Walipokwenda kinyume na taratibu za chama aidha walifukuzwa ama walijiondoa wenyewe na chama /taasisi ikaendelea kuwepo na pengine kuimarika zaidi.

Mfano mzuri ni akina M1&Co, walipotimuliwa baada ya kwenda kinyume na maadili na taratibu za chama bado CHADEMA haikutetereka bali iliimarika mara dufu. Kuelekea uchaguzi mkuu 2015 aliondoka Dr.Slaa CHADEMA haikupasuka kama miccm ilivyo tarajia na hatimae CHADEMA kwa chini ya UKAWA ilipata takriban 6m kwa nafasi ya Urais na idadi kubwa ya wabunge na madiwani hali iliyopelekea CHADEMA /UKAWA kuongoza baadhi ya halmashauri nchini ikiwemo Dar es Salaam.

Hili swala la Lowassa kwenda tofauti na mtazamo/ misimamo ya chama /taasisi haikubaliki, aitwe mbele ya kamati kuu ajieleze ni agenda zipi alienda nazo ikulu na kwani nini afanye jambo hilo kuwa siri? Kwa nini hakushirikiana na viongozi wa CHADEMA ili wawe na agenda ya pamoja? Apewe nafasi ya kusikilizwa asipotoa maelezo yanayo jitosheleza, milango iwe wazi kwake iwe ni kwa hiari yake ama kwa nguvu ya UMMA ili kulinda maslahi cha chama/taasisi na chama bado itabaki salama.

Kusifia serikali pale inapofanya jambo jema kwa wananchi wake siyo vibaya, ila kwa hali ilivyo hivi sasa kila raia amekata tamaa mtaani hali ni mbaya changamoto lukuki, maisha kwa ujumla ni magumu mno! Usalama wetu upo mashakani, huduma za Jamii hairidhishi, ajira, mikopo elimu ya juu balaa tupu, uhuru wa vyombo vya habari, kujieleza, bunge kabatini, unapataje ujasiri wa kupongeza serikali kwa hali hiyo?. Unless otherwise atueleze alienda ikulu kwa maslahi yake binafsi na yale yote aliyoyaongea ni maoni yake binafsi.

Mungu ibariki Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Africa kwa ujumla.
 
Kama ni taasisi na wanataratibu zao wajaribu tuone kumfukuza mamvi!!
 
Umeshasema chadema ni taasisi na aliyeenda ikulu siyo CHADEMA, ni Edward Lowassa ambaye ni mtu siyo taasisi.
Mbona mnamuunganisha Liwassa na Chadema?! Lowasa na chadema ni tofauti.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom