Hakimu mlevi azua tafrani mbeya

Msongoru

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
306
24
na Moses Ng’wat, Mbeya




HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo katika mji mdogo wa Tunduma uliopo Mbozi mkoani hapa, Godfrey Munisi, ameonja joto la jiwe baada kukamatwa wilayani Nakonde nchini Zambia alikokwenda kunywa pombe na kuanzisha vurugu.

Habari ambazo zimethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Elige Mlimila, zimesema kuwa tukio hilo limetokea juzi saa 2 usiku kwa saa za Zambia (sawa na saa 3 kwa Tanzania).

Habari zilizopatikana zilieleza kuwa, baada ya hakimu huyo kuvuka mpaka na kuingia nchini Zambia, alikwenda katika baa ya Lwambazi na kuanza kunywa pombe na baada ya muda alianza kutoa maneno ya kashfa yaliyoambatana na matusi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mlimila, hali hiyo iliwakera baadhi ya wanywaji waliokuwamo katika baa hiyo ambao walitoa taarifa polisi.

Alisema, polisi wa Zambia waliokuwa katika doria, baada ya kupata taarifa hiyo, walimkamata na kumpeleka katika kituo cha polisi cha mji wa Nakonde, Zambia.

Hata hivyo, Watanzania waliokuwapo katika mji wa Nakonde, baada ya kushudia tukio la kukamatwa kwa hakimu huyo, walitoa taarifa kituo cha polisi Tunduma, ndipo jitihada za kumtoa mikononi mwa polisi wa Zambia, zilipofanyika.

Alisema, Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduma aliwasiliana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Nakonde nchini Zambia bila ya mafanikio.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, baada ya polisi kushindwa kumnusuru hakimu huyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, alimwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbozi, kuwasiliana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nakonde.

Matukio ya viongozi wa umma kuvunja sheria za mipaka yamekuwa sugu ambapo Januari mwaka huu, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ileje mkoani hapa, alikamatwa na askari wa nchini Malawi kwa kile kilichodaiwa kuvuka mpaka na kufanya kazi nchini humo kinyume cha sheria za kimataifa za mipaka, hususani kwa majeshi.

Aidha, Jeshi la Polisi mkoani hapa limesema litalitolea ufafanuzi suala hilo pindi taratibu za uchunguzi zitakapokamilika.
 
Ha.. haaaa..haaaaaa!!! Tehe te..heeete...mmmh!

Ama kweli miiko ya UONGOZI haipo tena `inji hii`! Yalienda na Nyerere yote

wadau!!

Mi sishangai, but kwanini hawa wasiwe mfano kwa kuiaibisha nchi kiasi hicho?

Nyie wanasheria, si mnasema sheria ni msumeno? Na ukate basi kama

ndivyo!
 
Atakuwa alifuata totozi za kizambia buku 4 sawa na kwacha 10,000 umechukua mzigo kiulaini na watoto wa kule mzee acha tu.
 
Atakuwa alifuata totozi za kizambia buku 4 sawa na kwacha 10,000 umechukua mzigo kiulaini na watoto wa kule mzee acha tu.

We mzee angalia hii mambo!!

Nakuaminia Fidel, maana wewe huvungi kwenye fani, duh kila mtu

na idara bwana!! Sasa ukienda na buku 10 za Bongo mzee, si

utawapata watano wakufanyie massage kucha?

Angalia utaua watoto...te..he..te..te hee heeee!!

 
Back
Top Bottom